CHADEMA kuwasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika

Walikata rufaa Baraza Kuu hivyo ilibidi wapewe haki ya kusikilizwa kwanza. Baraza kuu limekaa na kutupilia mbali rufaa yao. Muwage mnafatilia mambo
Wamesoma rufaa zao humo barazani ambazo zina malalamiko yote. Ulitaka wasikilize vipi kwa kuongea kama kampeni?
 
Chadema kesho watawasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa Spika wa binge na Msajili wa vyama vya siasa

Aidha Halima Mdee na wenzake wanayo haki ya kuiomba mahakama irejee maamuzi ya baraza kuu

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia

Source BBC
enzi za mwendazake, mpeleka barua na barua yenyewe wangepotea.
 
Don't be negative, barua ya Chadema kuwafuta uanachama itapokelewa na Bunge kwa mikono miwili. Kama hawakwenda mahakamani, then Spika atawavua Ubunge na kuiarifu NEC nafasi hizo ziko wazi na Chadema wapeleke majina mengine 19.
P
Hivi mkuu kati ya bunge na NEC nani kisheria anatakiwa amtaarifu mwenzake?
Bunge hutoa taarifa kwa nec kuwa nafasi fulani ipo wazi au nec ndio huwataarifu bunge?

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Don't be negative, barua ya Chadema kuwafuta uanachama itapokelewa na Bunge kwa mikono miwili. Kama hawakwenda mahakamani, then Spika atawavua Ubunge na kuiarifu NEC nafasi hizo ziko wazi na Chadema wapeleke majina mengine 19.
P
Sio rahisi kiihivyo P,tuliona mienendo enzi ya awamu iliyopita
 
Wakienda Mahakama I wataruhusiwa kuendelea " kuingia" bungeni?
Katiba za vyama zimeweka wazi Katiba ya chama ndo ifuatwe, mahakama hauwezi jadili masuala ya vyama vya siasa au michezo, mahakama itahtaj rejea ya Katiba inasemaje na ndo utakua MWISHO wao. Halima ni mwanasheria hawezi fanya upuz huo.
 
Kwani hawajui huko ndio ofisini kwa Kibatala?

The game is over, na uzuri mama hataki magumashi, anahitaji maridhiano na Chadema hawezi kubariki uhuni huku kuna kikao cha maridhiano kati yake na team ya Chadema kinakuja.

Uhitaji rocket science kuelewa kwa nini Mbowe na mama walikutana kabla ya kikao cha baraza kuu.

Huu ndio muda mzuri wa Halima Mdee kututhibitishia jinsi alivyo mtupu kichwani kama ataendelea kuwapotosha wenzake. Hii shughuri imekwisha.

Kwa sasa utawala wa awamu ya sita una maslahi na Chadema kama chama na siyo kuwatumia mamluki wengine.

Hapa ndio mtaamini mama yuko vizuri kisiasa kuliko yule mgonjwa wa akili aliyeamini katika mabavu tu
Sasa wewe, mama na mahakama wapi na wapi? Rufaa yao ni mahakamani au kwa mama?? Ninyi ndo mnafanya sheria za nchi zipindishwe, wataenda mahakamani kusikilizwa we unaweka mambo ya mama it means wakishinda basi mama atatumia maamzi yake
 
Hayo ni mapigo ya chadema tunangoja majibu ya upande wa serikali huko bungeni. Tulia ana lipi la kusema katika hili.
 
Kwa kweli wanashangaza sana, CCM walitaka bunge la Chama kimoja, wakafukuza mawakala wa upinzani, wakachapisha kura bandia, wagombea wa CCM ndo wakawa sahihi kujaza fomu, wa upinzani hawajui kujaza, kupita bila kupingwa kwa CCM kukashamili, yote lengo ni bunge la Chama kimoja. Sasa leo, hawa wa Chadema wanatetewa na CCM? Kweli? Maajabu hayataisha duniani.
Mwizi hana adabu,akiamua kuiba nguo anaiba hadi za ndani halafu akifua anaanika nje sio uani.
Watu wanaona hii ilikuwa nguo yangu.
 
Haikuwa halali ila kwa sababu tulikuwa kwenye utawala dhalimu, iliwezekana hilo.

Ni sawa na hata hao wahuni wanaoitwa wabunge, waliweza kuapishwa na kutamkwa kuwa wabunge, kwa sababu dhalimu alikuwa ameamua iwe hivyo, na hakukuwa na wa kunyanyuka kumpinga kichaa mwenye panga mkononi huku wewe ukiwa huna chochote.
Utawala dhalimu ulishatoka sasa kaliungulumisheni mahakamani kupinga uchaguzi ule kama ushahidi upo wazi naamini na mama atawasikiliza na kulivunja bunge maana ni mpenda haki. 😁😁 au mmelizika na hali iliyowekwa na mdhalimu hata kama hayupo? Alokuambia piga magoti kwa saa 24 kafariki ndan ya saa 3 we bado umepiga magoti tu had zifike 24.
 
inawezekana usitambue Matokeo ya Uchaguzi Mkuu halafu ukatambua waliochaguliwa?…hata chanzo cha kuibuka kwa hao wabunge ni chadema kugomea kupeleka majina kwa kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi
Kwani Bunge limewahi kufutwa? Bunge ni chombo cha kikatiba. Usichanganye Bunge na wahuni walioingizwa na dikteta Magufuli kuwa wabunge.
 
Aliyepeleka ya mwanzo alipotea? Au ndo zile kwamba tega mgongo wakuseme.
Aliyetuma watu kuchana chana bendera za CDM kwenye mkutano wao mkuu wakati ule ni nani? dealing with very low entities. akwendeeee
 
Katiba za vyama zimeweka wazi Katiba ya chama ndo ifuatwe, mahakama hauwezi jadili masuala ya vyama vya siasa au michezo, mahakama itahtaj rejea ya Katiba inasemaje na ndo utakua MWISHO wao. Halima ni mwanasheria hawezi fanya upuz huo.
Katiba ya chama inasemaje ndo iwe hitimisho la yote? 😁😁 chama ni kikundi kinachorun kwa kufuata taratibu za usajili wa vyama kwa mjibu wa sheria, mi naamini katiba ya chadema haiwezi kuwa final say mahakamani. Mahakama haiamui kufuata katiba ya chama bali sheria na taratibu za nchi katika siasa.
 
Aliyetuma watu kuchana chana bendera za CDM kwenye mkutano wao mkuu wakati ule ni nani? dealing with very low entities. akwendeeee
😁😁 ukubwa ni jalala ndg yangu. Hilo suala hata akiagiza katibu mkuu wa chama au igp itaonekana ni rais kafanya. Magufuli alikuwa hadeal na vtu vidogo vya hvo.
 
Back
Top Bottom