CHADEMA kuwasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika

Aidha Halima Mdee na wenzake wanayo haki ya kuiomba mahakama irejee maamuzi ya baraza kuu

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia
Mbona vyama viko vingi, kwanini wasiende chapa ya jogoo wakakiongezee chati chama!!!
 
inawezekana usitambue Matokeo ya Uchaguzi Mkuu halafu ukatambua waliochaguliwa?…hata chanzo cha kuibuka kwa hao wabunge ni chadema kugomea kupeleka majina kwa kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi
CHADEMA haijawahi kutambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 wala wabunge wa Bunge la 2020. Aidha, wamesikika wakidai wao hawana mbunge kwenye bunge hilo. That’s clear.

Lakini taasisi ya Bunge na office bearers wake iko kikatiba na kisheria. Ndiyo wanayowasiliana nayo kikazi.

Katika sakata hili, CHADEMA ilikuwa inashughulikia waliokuwa wanachama wake waliokiuka msimamo na taratibu chama. Period. Haihusiki wala haina mamlaka katika masuala ya wabunge - ambao haina.
 
Katiba ya chama inasemaje ndo iwe hitimisho la yote? 😁😁 chama ni kikundi kinachorun kwa kufuata taratibu za usajili wa vyama kwa mjibu wa sheria, mi naamini katiba ya chadema haiwezi kuwa final say mahakamani. Mahakama haiamui kufuata katiba ya chama bali sheria na taratibu za nchi katika siasa.
Umepotoka ndugu, tafuta taarifa sahihi.
 
Hao ni SAwa na mtu kumpeleka mpenzi wake mahakamani eti kisa kamuacha. Hao wanalindwa na serikali lengo kuwahadaa wafadhili, hio kesi itaenda hadi October 2025 wakati wa uchaguzi, Ili wamalizie ubunge wao.
Wangekuwa wana maanisha wangewasimamishia ubunge kwanza hadi kesi iishe. Covid-19 ni michezo Kati ya Mbowe, CCM na serikali, Mbowe KILA siku anaitwa ikulu, na ikulu ni CCM. Na CCM ni adui wa Chadema, wewe shika jembe kalime.
 
Don't be negative, barua ya Chadema kuwafuta uanachama itapokelewa na Bunge kwa mikono miwili. Kama hawakwenda mahakamani, then Spika atawavua Ubunge na kuiarifu NEC nafasi hizo ziko wazi na Chadema wapeleke majina mengine 19.
P
Chadema waliwahi kukili kutoutambua uchaguzi uliolileta Bunge la JM wa Tanzania la sasa. Hii Barua yao ni ishara ya kuukubali uchaguzi mkuu uliolileta Bunge hili tukufu kwa awamu nyingine?

Tunakazi ngumu kama Taifa kupata chama cha upinzani kitakachoweza kuikosoa serikali badala ya kuendelea kujipigania kwa mambo yao binafsi ya kichama.
 
Chadema waliwahi kukili kutoutambua uchaguzi uliolileta Bunge la JM wa Tanzania la sasa. Hii Barua yao ni ishara ya kuukubali uchaguzi mkuu uliolileta Bunge hili tukufu kwa awamu nyingine?
Hii ya Chadema kama chama kutoa kauli za kutotambua matokeo ya uchaguzi, kutolitambua Bunge, na kutumtambua rais, huku unaliandikia Bunge barua rasmi za kiofisi, na Mwenyekiti wake na M/Mwenyekiti wakimtambua Rais na kufanya juhudi kubwa kumuona, kuzungumza nae kuhusu matatizo yao na Samia alivyo muungawana, sio tuu aliwakubalia, bali pia aliwakubalia kuwasaidia shida zao, fulani fulani, Lissu amesaidiwa, Mbowe anasaidiwa na Chadema inasainiwa na mfano mzuri ni kilichotokea baada ya Rais Samia kukutana na Lissu, mnajua Kilichopelekea na juzi kati kabla ya Kikao cha Baraza Kuu, Mwenyekiti wa Chadema, alibisha hodi Ikulu kumuona Rais Samia kwa ajili ya kumshukuru kwa jambo fulani, viongozi wa Chadema wanajua ila wana Chadema hawajui.
Tunakazi ngumu kama Taifa kupata chama cha upinzani kitakachoweza kuikosoa serikali badala ya kuendelea kujipigania kwa mambo yao binafsi ya kichama.
Chadema kama chama cha upinzani kilichosajiliwa ni kipo, lakini kama chama cha upinzani makini kinachosubiri kukabidhiwa nchi hii, kwa Chadema ni bado sana, hamna kitu pale!.
P
 
Hii ya Chadema kama chama kutoa kauli za kutotambua matokeo ya uchaguzi, kutolitambua Bunge, na kutumtambua rais, huku unaliandikia Bunge barua rasmi za kiofisi, na Mwenyekiti wake na M/Mwenyekiti wakimtambua Rais na kufanya juhudi kubwa kumuona, kuzungumza nae kuhusu matatizo yao na Samia alivyo muungawana, sio tuu aliwakubalia, bali pia aliwakubalia kuwasaidia shida zao, fulani fulani, Lissu amesaidiwa, Mbowe anasaidiwa na Chadema inasainiwa na mfano mzuri ni kilichotokea baada ya Rais Samia kukutana na Lissu, mnajua Kilichopelekea na juzi kati kabla ya Kikao cha Baraza Kuu, Mwenyekiti wa Chadema, alibisha hodi Ikulu kumuona Rais Samia kwa ajili ya kumshukuru kwa jambo fulani, viongozi wa Chadema wanajua ila wana Chadema hawajui.

Chadema kama chama cha upinzani kilichosajiliwa ni kipo, lakini kama chama cha upinzani makini kinachosubiri kukabidhiwa nchi hii, kwa Chadema ni bado sana, hamna kitu pale!.
P
Well said P
 
Back
Top Bottom