CHADEMA kuwasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake kwa Spika

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,878
141,811
Chadema kesho watawasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa Spika wa binge na Msajili wa vyama vya siasa

Aidha Halima Mdee na wenzake wanayo haki ya kuiomba mahakama irejee maamuzi ya baraza kuu

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia

Source BBC
 
Mkurugenzi wa kituo cha haki za binsdamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia

Source BBC
Kwahiyo siku zote hizo walikua Bungeni kihalali mpaka hiyo kesho itakapo pelekwa hiyo barua rasmi ya kuwavua uanachama kwa Spika?
 
Mnyika alishaandika barua kutokana na uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua ubunge. Baada ya C-19 kukata rufaa na Baraza Kuu kuridhia uamuzi wa Kamati Kuu wa kuwavua madam aka, hapo ndo Mnyika anaandika barua nyingine.
Unaweza kuleta nakala ya hiyo barua?
 
Kwanini CCM mmeumia ili hali mlitaka Bunge la chama kimoja?
Kwa kweli wanashangaza sana, CCM walitaka bunge la Chama kimoja, wakafukuza mawakala wa upinzani, wakachapisha kura bandia, wagombea wa CCM ndo wakawa sahihi kujaza fomu, wa upinzani hawajui kujaza, kupita bila kupingwa kwa CCM kukashamili, yote lengo ni bunge la Chama kimoja. Sasa leo, hawa wa Chadema wanatetewa na CCM? Kweli? Maajabu hayataisha duniani.
 
Watawashauri waende mahakamani ?
Kwani hawajui huko ndio ofisini kwa Kibatala?

The game is over, na uzuri mama hataki magumashi, anahitaji maridhiano na Chadema hawezi kubariki uhuni huku kuna kikao cha maridhiano kati yake na team ya Chadema kinakuja.

Uhitaji rocket science kuelewa kwa nini Mbowe na mama walikutana kabla ya kikao cha baraza kuu.

Huu ndio muda mzuri wa Halima Mdee kututhibitishia jinsi alivyo mtupu kichwani kama ataendelea kuwapotosha wenzake. Hii shughuri imekwisha.

Kwa sasa utawala wa awamu ya sita una maslahi na Chadema kama chama na siyo kuwatumia mamluki wengine.

Hapa ndio mtaamini mama yuko vizuri kisiasa kuliko yule mgonjwa wa akili aliyeamini katika mabavu tu
 
Chadema kesho watawasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa Spika wa binge na Msajili wa vyama vya siasa

Aidha Halima Mdee na wenzake wanayo haki ya kuiomba mahakama irejee maamuzi ya baraza kuu

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binsdamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia

Source BBC

Sasa hiyo mahakama kuu ndio itabadili sheria kuwa wabunge sasa wasiwe na vyama? Nchi hii haina independent candidates pengine mpaka tupate katiba mpya!
Ofisi ya Spika haina budi kuongoza kufuata sheria inazozitunga, na sheria iko wazi juu ya hili.
 
Wewe ndio unajiona una uwezo mkubwa wa uelewa?

Ungekua unaulewa ungejibu nilichokiuliza,maana hiyo comment ya ni swali nimeuliza,

Uwe unasoma comment na kuielewa kabla ya kukurupuka na kuanza kuharisha hovyo hapa.
Unauliza vitu vya kipuuzi ndio maana unajibiwa kulingana na upuuzi wako
 
Kwahiyo siku zote hizo walikua Bungeni kihalali mpaka hiyo kesho itakapo pelekwa hiyo barua rasmi ya kuwavua uanachama kwa Spika?
Walikata rufaa Baraza Kuu hivyo ilibidi wapewe haki ya kusikilizwa kwanza. Baraza kuu limekaa na kutupilia mbali rufaa yao. Muwage mnafatilia mambo
 
Chadema kesho watawasilisha barua rasmi ya kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa Spika wa binge na Msajili wa vyama vya siasa

Aidha Halima Mdee na wenzake wanayo haki ya kuiomba mahakama irejee maamuzi ya baraza kuu

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu mama Henga amesema lilipoishia baraza kuu la Chadema ndipo Mahakama kuu itakapoanzia

Source BBC
Ze baptist inaonekana una huruma sana kwa COVID-19 🤔
 
Katibu wa Bunge atatia kufuli ofisi yake.

Kwa kifupi tusubiri vituko na vioja kutoka kwa Spika na Katibu wa Bunge kuhusiana na hili sakata.
Don't be negative, barua ya Chadema kuwafuta uanachama itapokelewa na Bunge kwa mikono miwili. Kama hawakwenda mahakamani, then Spika atawavua Ubunge na kuiarifu NEC nafasi hizo ziko wazi na Chadema wapeleke majina mengine 19.
P
 
Huu mpira umerudishwa vizuri sana kwa CCM, kama bado wana nia ya kuwalinda hao wanawake ili waendelee kupoteza kodi za watanzania kuwalipa posho na mishahara ni juu yao.

Lakini ukweli umeshadhihirishwa na Baraza Kuu la Chadema, wao kama chama wameshamaliza kazi kwa upande wao.
 
Back
Top Bottom