CHADEMA kuwashirikisha NCCR na TLP baraza jipya la Mawaziri Kivuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuwashirikisha NCCR na TLP baraza jipya la Mawaziri Kivuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Jun 18, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  MWANANCHI: JUMAMOSI JUNI 18,2011

  Neville Meena, Dodoma
  BARAZA la mawaziri kivuli lililo na wabunge kutoka Chadema pekee, huenda likavunjwa na kuundwa jipya litakalojumuisha wabunge wa vyama vingine vya upinzani.

  Kambi ya Upinzani bungeni inaongozwa na Freeman Mbowe na Naibu wake, Zitto Kabwe sasa inafanya mazungumzo na wabunge wa vyama vingine vya upinzani ikiwa ni hatua ya kutaka kushirikiana.

  Ikiwa viongozi hao watafikia mwafaka, Mbowe atalazimika kufumua upya baraza lake la mawaziri ili kuwajumuisha wabunge wa vyama vingine vya upinzani.

  Mchakato wa kuwashirikisha wabunge hao ulianza kwa Mbowe pamoja na Zitto kukutana na wabunge wa vyama vya NCCR Mageuzi, David Kafulila na TLP, Augustine Mrema mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ofisi za Kambi ya Upinzani, bungeni, Dodoma.

  Katika kikao hicho, pia walialikwa Wabunge wengine wa upinzani, Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF) na John Cheyo (Bariadi Mashariki -UDP), lakini hawakuhudhuria kutokana na kuwa nje ya Mkoa wa Dodoma kikazi.

  Mnyaa alikuwa na safari ya kibunge nchini Angola na Cheyo alikuwa mkoani Shinyanga ambako alikuwa na katika shughuli zinazohusiana na masuala ya kilimo cha pamba na uuzaji wa zao hilo.

  Mwishoni mwa wiki hii Mbowe alikaririwa akisema kuwa mazungumzo hayo yameanza na kwamba wazo ni kuunganisha nguvu za wapinzani na kuwa na mtazamo mmoja wa masuala ya kitaifa kama vile bajeti ya nchi na mengine.

  "Niseme tu kwamba kweli tuliwaomba wenzetu kukutana nao. Kama nilivyoahidi wakati nilipotangaza baraza langu la mawaziri kivuli kwamba suala la ushirikiano na wapinzani wegine ni la muda, hivyo tumeona ni vizuri kuanza sasa," alisema Mbowe.

  "Mrema na Kafulila tulizungumza nao na tuliwaeleza nia yetu hiyo, sasa tunachosubiri ni mawazo kutoka kwao kwani sisi tayari tulishaweka hoja mezani, naweza kusema kwamba hapo ndipo tulipofikia hadi sasa," alisema Mbowe.

  Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema alisema wanatafuta fursa nyingine ya kukutana na wenzao hao ili kuendeleza mazungumzo, ikiwa ni pamoja na wale wa UDP na CUF ambao hawakuweza kushiriki katika kikao cha kwanza.

  Jitihada za kuwaunganisha wapinzani wote bungeni, zimekuja wakati kambi hiyo ikitakiwa kutekeleza jukumu la kutunga kanuni za kuiongoza, suala ambalo Mbowe alisema linapewa nafasi ya kwanza hivi sasa ili kuweka utaratibu wa uendeshaji.

  Kanuni za kambi rasmi ya upinzani bungeni lazima ziwatambue wabunge wote wa upinzani ikiwa ni pamoja na Kamati tatu za Hesabu za Serikali zinazoongozwa na wabunge wa kutoka upinzani.

  Kamati hizo ni ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ambayo hivi sasa inaongozwa na Mrema, Hesabu za Serikali Kuu (PAC), ambayo inaongozwa na Cheyo na ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), inayoongozwa na Zitto.

  Kwa maana hiyo, taarifa zozote za kamati hizo lazima zifike kwa kiongozi rasmi wa kambi ya upinzani bungeni kabla ya kuwasilishwa katika vikao vya Bunge na hilo ni miongoni mwa mambo ambayo mchakato wa sasa wa kuwaweka pamoja wabunge wa upinzani unalenga kulitekeleza kwa ufanisi.

  Mbowe alipotangaza orodha ya mawaziri kivuli, Februari, 13 mwaka huu alisema mawaziri hao 29 wanatoka Chadema tu kwa kuwa mawasiliano na vyama vingine yalikuwa bado hayajakamilika.

  Chadema ni chama cha upinzani pekee kilichotimiza masharti yatokanayo na kanuni ya 14 fasili ya (4) ya kuchagua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, hivyo kumpa Mbowe nafasi ya kuunda Baraza la Mawaziri Kivuli kutoka Chadema peke yake.

  “Ni matumaini yangu kuwa hapo siku za usoni na baada ya kuelewana na kuridhiana na wenzetu, nitaweza kuunda baraza litakaloweza kushirikisha vyama vingine kutoka kambi rasmi ya upinzani bungeni,” alisema siku alipotangaza baraza hilo.

  Hata hivyo, mmoja wa mawaziri hao, Leticia Nyerere aliyekuwa akiongoza Wizara Kivuli ya Mazingira alijiuzulu wiki iliyopita, akisema kuwa anawaachia wengine fursa ya kuongoza badala ya kung'ang'ania madaraka peke yake.

  Kafulila na Mrema

  Akizungumzia suala hilo, Kafulila ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kusini alisema:
  "Naona ni wazo zuri wala hakuna shida, kweli tumeshiriki katika kikao hicho, lakini nadhani bado ni mapema mno kusema ni nini kitakachotokea,"alisema Kafulila ambaye kabla ya kuhamia NCCR Mageuzi alikuwa mwanachama wa Chadema.

  Alisema binafsi haoni ubaya wa kushirikiana na Chadema ikiwa wapinzani wana malengo yanayofanana ya kuwawakilisha wananchi, lakini pia kuibana Serikali itekeleze wajibu wake kwa umma.

  Hata hivyo, alisema ushirikiano huo utawezekana ikiwa kutakuwa na maridhiano ya pamoja ya jinsi ya kuendesha kambi hiyo ili kulinda demokrasia na kuheshimu maoni ya pande zote hata pale kunapokuwa na mitazamo tofauti miongoni mwao.

  Kwa upande wake, Mrema alisena: "Siyo jambo baya, ni zuri tu kwani kushirikiana na Chadema hatujaanzia hapa (bungeni), tumeanzia kule katika Halmashauri ya Moshi, ile Halmashauri inaogozwa na Chadema kwa kushirikiana na TLP."

  Hata hivyo, alisema Chadema wamechelewa sana kutoa wazo hilo kwani fursa ilikuwapo tangu mwanzo na wakashindwa kuitumia kwa maelezo kwamba yeye (Mrema) ni kibaraka wa CCM.

  "Jamani hata kama wanaamini kwamba mimi ni kibaraka wa CCM basi wangewaheshimu wananchi wa Vunjo ambao walinipigia mimi kura na kunichagua kuwa mbunge, kule Moshi Vijijini mbona tuna ndoa na mambo yanakwenda vizuri?” Alihoji Mrema na kuongeza:

  "Kimsingi mimi sina matatizo, maana ushirikiano ni kitu kizuri sana hasa kwa maendeleo ya wananchi, sisi sote ni wapinzani kwa hiyo nadhani hakuna tatizo tukishirikiana na kuheshimiana."

  Alisema anasubiri vikao vinavyofuata ili kuona hitimisho la majadiliano yanayoendelea miongoni mwao.

  Kambi ya pamoja

  Wakati Chadema kikianza mchakato wa kuwashirikisha wabunge wengine wa upinzani katika kuongoza kambi hiyo, kumekuwa na tofauti za kimtizamo kuhusu masuala mbalimbali yanayojitokeza ndani ya Bunge.

  Miongoni mwa masuala hayo ni hoja inayotaka kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wengine wa umma. Chadema na NCCR-Mageuzi wanaonekana kuunga mkono suala hilo, hali CUF wakionyesha kuwa tofauti na msimamo huo.

  Tofauti hiyo ilijitokeza juzi wakati Mnyaa alipouliza swali kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihoji iwapo Serikali haioni umuhimu wa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaovunja Katiba kwa kutaka kufutwa kwa posho ambazo kimsingi zipo kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

  My Take: Ni mwanzo wa upinzani mpya bungeni au?? Hata hivyo siridhiki kuiunganisha CUF katika baraza jipya

   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  CUF-is gone,Lipumba ana kazi ya ziada
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapo sawa kwani sasa NCCR wamepoa watakubali tu
   
 4. k

  kazuramimba Senior Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwisha habari yao chadema.walidhani ni ujanja kuwapekeyao huku wakivipiga chini vyama makini kama CUF na TLP.Wanatapatapa hawana la kufanya mwishowao huoooo.!!!
   
 5. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukikua utaacha hizo sigara kubwa
   
 6. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wenye akili wanatazama mbali kwa mustakali wa Taifa, wewe unatazama umbali wa pua yako iliyo bantalala!
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,653
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Kazi ya Nape hiyo, misukule inajitahidi lakini wapiiiiiiiiii.
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Tahadhari ni muhimu saaana,ninapenda sana ushirika huu ingawaje tatizo langu bado liko palepale...kwamba CUF iliyokuwa inaikejeri CDM,leo wanaona CDM itawafaa?TLP kama chama sioni tatizo ila tatizo naliona kwa Mrema,huyu mzee katu sitakuja nimwelewe kamwe,ni zaidi ya kinyonga,ni zaidi ya popo,sidhani kama atakuwa na jema kwa CDM kwa 100%

  Ushauri wangu,ni kweli tumeyasikia mengi,tumeyaona mengi,nawashauri CDM wawe waangalifu sana na waanzishe chombo maalumu cha kufatilia na kuripoti ushirika huu kwa ukaribu sana ili badala ya kujenga tusije kulia kilio cha kusaga meno

  juzi kati tumetoka kuletewa thread humu ndani iliyokuwa ikisema- wakati sisi tunalala wenzetu wanakesha,amini usimini,tupende tusipende magamba yako kila mahali na nina uhakika hata kwenye ushirika huu wataingia ama phsically ama spiritually.... they are so opportunists!
   
 9. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni mkakati mzuri, na itapendeza zaidi mkifanikiwa kuwa pamoja...
  Hongereni CHADEMA kwa kutambua umuhimu wa kuungana na wapinzani wengine...
   
 10. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tunapongeza hatua mlizoamua kuzichukua CDM lkn tahadhari ni muhimu hasa kwa vyama kama CUF na TLP. NCCR wameonyesha kuwa katika njia moja nanyi hata kihoja. Umakini na busara za hali ya juu ni lazima vitumike katika hili. Twende nalo taratibu tusikurupuke.
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema si mlisema chama cha upinzani Tanzania ni kimoja tu, sasa imekuaje tena mnaanza mchakato wa kushirikisha vyama vingine vya siasa, miezi sita tu taingia kuundwa kwa Baraza la Mawaziri Kivuli mpo hoi, Chadema-JF, sijui mtaama Chadema wakiungana na CUF,NCCR Mageuzi, UDP, TLP
   
 12. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio muafaka na ni maana halisi ya upinzani. Upinzani siku zote lazima wawe kitu kimoja bungeni na hata nje ya Bunge. Na nje ya Bunge kupinga ufisadi, mabaya na maovu yote yanayofanywa na serikali ya ccm na kuleta mageuzi ya kweli na ya haki kwa watanzania.
  Na huo upinzani uendelee mpaka wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015. kitu rahisi na ambacho kinawezekana kwa watanzania kujikomboa
  ni kupiga kura moja. ni vipi basi ni mshikamo wa kweli na kuondoa tofauti kati ya viongozi wa upinzani na tamaa ya madaraka. vyama vyote
  kuingia mkataba wa kupiga kura moja na kufanya serikali ya mseto. Bila hivyo kuing`oa ccm itakuwa ni kitendawili. Rais inajulikana wazi
  kama atatoka cdm. Na baraza la mawaziri itategemea percentage za kura walizopata. ilo wala si jambo gumu kulitekeleza, na chama cha
  upinzani kitakacho leta utata kwa ilo ufahamu hao viongozi awalitakii mema taifa la Tanzania na ni waroho wa madaraka na kufuja rasilimali
  za watanzania kama wanavyofanya ccm kwa muda wa miaka hamsini waliokuwa madarakani. Kwenye nia pana njia. hoja yako hiyo ni
  muhimu sana, kwani tanzania inahitaji kuwakomboa maskini haswa wale wa vijijini ambapo wanafikia mpaka kufa kwa njaa. kwa maan hiyo
  nchi inaelekea wapi wakati Tanzania sio nchi maskini. na katika vyama hivyo cuf kina ugumuugumu kidogo, Mrema na Dovutwa tupilia mbali
  wapo wapo tu kupata mlo kwa kutua siasa na sio kuwatumikia wananchi. Hoja mbili kwa sasa zina sana kabla ya uchaguzi ujao. Katiba na
  vyama vya upinzani vipige kura moja bila hivyo itakuwa ni bra bra bra!!! ambayo aitusaidii watanzania halisi.
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Bila shaka CDM waliamua kwenda kivyao baada ya kuwepo mazingira fulani ikiwa pamoja na kile walichoita ndoa ya CUF na CCM. Kumetokea mabadiliko gani yanayohalalisha huo uhusiani leo hii?
   
 14. p

  police Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hureee!! mbowe kaangukia pua, ule mkakati wake wa kufanya cdm kuwa chama kikuu cha upinzani na kuponda vyama vingine tlp na cuf kwamba ni ccm b imemuumbua, sasa kaona hafiki bila mrema. kaona mrema anavyo pambana na halmashauri kamkubali, vile vile kafulila. mbowe acha uroho utashika vingapi wewe peke yako?
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mbowe ndio anaomba kuangana na TLP, NCCR, CUF, vipi mkuu utaama chama au utakubali na wewe ndoa
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hakukuwa na njia mbadala. kwani mtu kama sugu utamkabitdi wizara kweli? siatatunga mistari tu? sasa zito/mbowe mmeanza kuwa na akili.
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi sina ugomvi kabisa kwa vyama vya upinzani kushirikiana vyenyewe kwa vyenyewe -- na hata kuungana, iwapo sheria na kanuni zinaruhusu. Kinachonikera ni kwa chama cha upinzani kushirikiana au kuungana na chama kilichopo madarakani.

  Bila shaka CUF wamelitambua hili na Prof Lipumba -- ambaye naamini kabisa ni kiongozi ambaye angefaa kabisa kuwa rais wa nchi hii -- amejikuta njia panda kutokana na yaliyojiri huko Visiwani kwa chama chake.

  Na ndiyo maana juzi alionekana kumsapoti Mbowe alipokamatwa na polisi. CDM nawaomba wakutane pia na Profesa ili kuona taifa linaokolewa vipi kutoka kwa hao mafisadi, na ambao sasa pia wamekuwa wauaji wa raia.

  Huwa nawaza: Jee sasa hivi Profesa akitangaza kuhamia CDM -- itakuwaje? nadhani watakaochanganyikiwa sana sana siyo CUF, wala CCM -- bali ni CDM! Just think about it!!!!!
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..tatizo alikuwa Hamad Rashid.

  ..naona hata Lipumba sasa kumshtukia.

  ..hii itamaliza mizozo kati ya vyama hivyo na watabakia kuelekeza mashambulizi kwa CCM.

  ..Hamad Rashidi yeye atabakia kupigania posho na akiwa ameungana na wana CCM.
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Umbali kwenu unaanzia wapi? Kwani hapo mlipogombania na kutowa kejeli mlikuwa hamjuwi kuwa kuna mbali ya kutizama?
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hamadi Rashid sie alieleta Serikali ya Mseto kule Zanzibar ambako mlitowa matusi ya nguoni, mlisahau msemo wa Waswahili " Msitukane wakunga na bado hamjazingoa.
   
Loading...