Chadema Kuwasha Moto Ukonga, Ufisadi Mtaa wa Mongolandege kuwekwa hadharani

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Wadau wa JF nawasalimu na habari za siku kadhaa.

Nimekuwa busy kidogo tunapoelekea mwisho wa mwaka lakini harakati za kukijenga chama chetu pendwa, tumaini la watanzania zinaendelea kama kawaida kadri nafasi inavyopatikana.

Kesho tunatarajia kuwa na mkutano wa hadhara katika mtaa wa Mongolandege Kata ya Ukonga kuanzia saa nane kamili mchana (8:00).

Agenda kuu ya mkutano huo itakuwa ni kuwafahamisha wananchi wa Ukonga juu ya ufisadi mkubwa sana uliofanywa na wenyeviti wa serikali za mitaa ya Mongolandege na Mazizini, ambapo wote wawili wanatuhumiwa kuuza maeneo ya wazi yanayomilikiwa na serikali za mitaa husika.

Uuuzwaji wa eneo la serikali ya mtaa wa Mongolandege uliwahusisha Mwenyekiti wa mtaa(ccm), wajumbe watano wa serikali ya mtaa(ccm)na mtendaji wa serikali ya mtaa. Hadi wakati huu tulipoitisha mkutano wa hadhara tumeshazitia mkononi documents zote zinazoonyesha uuzwaji wa kiwanja hicho na aliyeuziw ameshajenga nyumba ya kuishi. Mwenyekiti wa mtaa tayari ameshajiuzulu baada ya kashfa hiyo lakini wajumbe wamegoma kujiuulu na wanalindwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala akimtumia katibu tarafa.

Katika mtaa wa Mazizini napo mwenyekiti wa mtaa(ccm) ameuza eneo la kiwanja cha ofisi ya serikali ya mtaa na wananchi wamekwisha mkataa japokuwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala kupitia kwa katibu tarafa anaendelea kumlinda, kama anavyowalinda wajumbe watano wa mongolandege.

Wadau wote wa maeneo ya jirani na Ukonga mnakaribishwa sana katika mkutano huo ambapo mgeni rasmi atakuwa mwenyekiti wa Vijana Chadema Taifa kamanda John Heche Suguta.

NB:
Diwani wa kata ya Gongolamboto ambaye pia ni meya wa manispaa ya Ilala akae mkao wa kulia kwakuwa baada ya hawa wenyeviti wa mitaa ni zamu yake, tunamalizia ku compile mafaili ya ufisadi wake katika manispaa ya Ilala, hasa kuhusiana na ardhi.

Wasalaaam Mwita Maranya, nimerudi tena kuwashika.
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
2,000
Wazee wa gongo.

Eee bana hii sera yenu mpya kuongeza uzalishaji wa pombe ya gongo imekuwa gumzo mitaani.
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Wazee wa gongo.

Eee bana hii sera yenu mpya kuongeza uzalishaji wa pombe ya gongo imekuwa gumzo mitaani.

Miaka yote zaidi ya saba uliyokaa Jamhuri ya Czech ukisoma haijakusaidia kabisa, na wala hauna tofauti yoyote na wanywa gongo wa Ziginali, Kiberege na Sanje.
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
2,000
Miaka yote zaidi ya saba uliyokaa Jamhuri ya Czech ukisoma haijakusaidia kabisa, na wala hauna tofauti yoyote na wanywa gongo wa Ziginali, Kiberege na Sanje.

Hahahahaha mkuu, hii gongo si mnataka kuihalalisha? Mbona unaipiga madongo tena?

Hahahahaha wazee wa gongo...
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367
2,000
Hahahahaha mkuu, hii gongo si mnataka kuihalalisha? Mbona unaipiga madongo tena?

Hahahahaha wazee wa gongo...

Wewe ni mk...du,wengine tumesomeshwa kwa gongo,heri yako wewe p.i.m.b.i uliyebarikiwa.kumbuka watu wanaotegemea gongo na watumiaji ni watz wenzetu na ndio maskini wapiga kura 2015.nategemea watafanya kweli na usiwalaumu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom