CHADEMA kuwapokea Lowassa, Rostam Aziz na Chenge

Acha mzaha mkuu...kwenye hii forum tunategemea watu wenye umakini wasio na mzaha,nakushauri kama una thread si lazima upost hapa JF..hata kusoma thread na post za wenzako ni heri pia..........
Mwambie akapost twiter au facebook
 
wajiunge cdm?ushindwe! Na ulegee! Hao mapacha watatu(r.a,cheng,e.r) nawashauri waanzishe bourgeoisie party,wampe ft karamag.tutawaenz kama waasisi wa hicho chama.

kama watakili makosa hacha waingie cdm kwan kuna viongoz makin mle hivyo hawataleta usumbufu hata kido na pakukimbilia hawana
 
CHADEMA wakikubali kuwapokea Lowassa, Rostam na Chenge (watu watatu) ni sawa na kuwafukuza wapiga kura au wanachama wengine wa CHADEMA zaidi ya laki tano (500,000) mimi mwenyewe nikiwepo. Hatupendi kitu kama hicho kitokee.
 
Jaman kama watakubali makosa tuwasamehe ni wa tz wenzetu ila tutawaomba robo tatu za mali zao zitolewe kwa wananchi na kwa hivyo tuta amin kuwa wamekili kweli makosa yao
 
itakuwa ndo kiama cha nchi hii, ccm hakurudki na chadema kutakuwa hakukaliki, dawa itakuwa ni kuwapiga mawe slaa na mbowe popote pale tutakapowaona. Km hawaamini wajaribu kucheza na akili na za watanzania haiwezekani cc tunajitotelea kwa hali na mali katika kuleta ukombozi halisi halafu wao watuletee upuuzi, hapa nimepandwa na hasira kwa ki2 nanachojua si kweli je ingekuwa kweli?

mimi ninafikiri kama hizi tetesi ni za kweli hazina ubaya kabisa hawa ni watanzania wenzetu wanaweza wakawa watu wazuri kabisa na wakasaidia kujenga nchi waliyoyafanya yalitokana na mfumo wa chama walichokuwepo cha 10% wanaweza wakaja huko chadema kwenu wakafanya kazi nzuri kabisa ya kujenga nchi na walioyafanya waliyafanya kama group kwa hiyo kama wakikuta huko chadema ni watu rushwa wataendelea tu , kwa hiyo hii ni nguvu kazi ya kutosha na wanaweza kusaidia kuonyesha loopholes zote za madudu ya ccm waliokuwa wanayafanya na kuziba njia zote za kuibomoa ccm kwa hiyo kama wakiungama na kujiunga chadema obvious watakuwa wamesoma sera na matarajio ya chadema ni sawa dr safari alivyohama cuf alikaa mda bila kujinga na chama chochote alikuwa akitafakari ni chama kipi mbadala kinamfaa hakuwa fisadi lakini alifanya kwanza tafakuri kwa hiyo hawa jamaa kama wanaamua kuja huko nafikiri watakuwa wamefanya tafakuri ya kina na kufahamu kabisa wanapokwenda siyo mjomba wao ni kwa watu serious nafikiri wakaribishwe wajenge nchi na wala sio kosa kumbuka kuna makaburu walijiunga na chama cha anc na wanaendelea kufanya kazi ya kujenga nchi yao walijiunga wakijua sera za anc zipo against na wao.
 
Hizo ni ndoto za mwendawazimu,hawa wezi hawawezi kujiunga CDM nani atawapokea?na wataanzia wapi?hivi mnafikiri CDM ni chama cha kina Slaa?CDM inatumia nguvu zetu wananchi,bila wananchi hakiwezi kudumumu.
 
Kuna tetesi kuwa baada ya kupewa barua zao Lowasa, Rostam na Chenge watapokelewa CHADEMA. Je kama ni kweli hizi tetesi wanajamii, huu si utakuwa usaliti tunaofanyiwa na hawa watu ambao sisi ndio tumewafikisha hapo walipo?
kuna kila dalili kuwa cdm damu moja na mapacha watatu kuthibitisha hilo someni tanzania daima ya leo
 
Hakuna ubishi wowote kuwa CCM wameazisha mkakati wa kupangua hoja hapa jukwaani. Isisumbue wajadilifu wanapoona hoja zimekaa kiaina. Wasameheni, wapuuzeni na tusonge mbele tukomboe taifa letu.
 
Kuna tetesi kuwa baada ya kupewa barua zao Lowasa, Rostam na Chenge watapokelewa CHADEMA. Je kama ni kweli hizi tetesi wanajamii, huu si utakuwa usaliti tunaofanyiwa na hawa watu ambao sisi ndio tumewafikisha hapo walipo?
haiweztokea CDM wakawapokea MAFSAD
 
Hakuna ubishi wowote kuwa CCM wameazisha mkakati wa kupangua hoja hapa jukwaani. Isisumbue wajadilifu wanapoona hoja zimekaa kiaina. Wasameheni, wapuuzeni na tusonge mbele tukomboe taifa letu.
kuna kila dalili kuwa cdm na mapacha watatu ni damu kuna makala zaidi ya tatu kwenye gazeti la leo nia na maudhui ya hizo makala ni kuwatetea mapacha watatu
 
Back
Top Bottom