CHADEMA kuwa na wabunge chini ya ishirini(20) ifikapo Jan 2016 - UTABIRI! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuwa na wabunge chini ya ishirini(20) ifikapo Jan 2016 - UTABIRI!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyami2010, May 14, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nionavyo mimi, kama CCM wakijipanga sawasawa bado ni Chama chenye nguvu, vijana wenye mvuto, hoja na mtandao mkubwa hapa nchini. Hakika ni chama cha KITAIFA!

  Hakuna asiyejua kuwa baadhi ya Majimbo yalianguka mikononi mwa CDM kwa sababu ambazo CCM wanajutia na wataendelea kujutia. CCM wakiwa serious na wakaamua kukomaa na wakaacha uchakachuaji wa wao kwa wao ndani ya chama chao, hakika CCM bado ni Chama cha wengi na hakina mwenyewe.

  Nisemalo haliko mbali sana, tumuombe Mungu tuwe hai na JF yetu iwe hai, kisha tuhesabu wabunge wa Majimbo wa CDM ifikapo Jan 2016.

  Mwenye maoni au mtazamo tofauti.........karibu!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haaaaa haaaaaa! CCM ipi unayoizungmzia ndugu? Kinachoiangamiza CCM ni kulea ufisadi na mafisadi na kutoa ahadi hewa! Unapodai "CCM ikijipanga" unamaanisha watawapeleka mafisadi mahahakani na kutimiza ahadi zao zote? Mtanzania wa leo si wa jana ndugu! You can't believe Dkt Mwakyembe alikuwa anaonekana shujaa jimboni kwake Kyela na walimwita Obama, sasa hivi wanamwita "msanii" hata hajamaliza mwaka tangu achaguliwe kuwa mbunge kwa mara nyingine! Salama ya CCM kwa sasa ni nguvu za dola, ndio maana "wazee wa intelijensia" hawaachi kurusha mabomu kwa hofu ya nguvu ya umma! Utafika wakati watu watazoea mabomu na hawataogopa tena! Hapo ndio utakuwa mwisho wa CCM!
   
 3. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Je utabiri wako Umetokana na Mungu wa mbinguni au umetoka kuzimu kama ule wa shekhe Yahaya? Hata kuzimu kwenye ulimwengu wa roho inajua kuwa CCM haipo tena madarakani.Haya yote unayoyaona ya magamba ni taratibu za kibinadamu roho wa uharibifu anazikamilisha kwenge ulimwengu wa mwili.
   
 4. m

  menny terry Senior Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  We usikute ni nape au Mkama ulietuma thread hii.Kafie mbele na CHAMA CHA MAGAMBA.Wananchi wameamka sasa hivi ikumbukwe kuwa Watanzania wengi waliamini vyama vingi ni vita ila sasa wamejua ukweli uko wapi.
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Naweza kukubaliana nawe kwa sababu nna uhakika wa chadema kuanza kusambaratika mara tu baada ya kumaliza ziara zao za mikoani.

  Natabiri; mwanzo wa kusambaratika chadema ni baada ya kikao cha bunge kijacho. Tutaona chadema wataanza kulumbana wenyewe kwenye kikao kijacho cha bunge na vuguvugu litaendelea hadi kukisambaratisha chama. Chokochoko baada ya vikao vya bunge zitaanza kuikumba chadema kupitia makundi ya safari na lingine mbowe na lingine slaa. Kila kundi litataka liwe na kauli zaidi ya lingine. Kwa upande mwingine, zitto hatakubali awachwe mkiani, mdee atanunuliwa kwa pesa ndogo tu, lema halikadhalika na lisu tayari kisha wekwa mfukoni. Duhh. Huu ni utabiri tu, inawezekana iwe au isiwe.
   
 6. O

  Omr JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utabiri wako sio sawa sawa, 2016 ni mbali sana, hata mwaka mmoja ni mwingi kwa hawa jamaa.
   
 7. T

  Triple DDD Senior Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna utabiri hapo, Makamanda wa CDM hawawezi kununuliwa, hilo ni hisia binafsi.
  Nia moja, wananchi tuko nao bega kwa bega. Kwani ww hata leo hii umeona CCm inawapa airtime
  CDM kwa TBC ikiwa hata mikutano yao haionyeshwi kabisa na ikionyeshwa ni wakitoka hotelin ia inageuzwa wakiongea
  na sio impact na meseji. Ila mchovu Nape mpaka mashairi yote anaonyeshwa na wote alionao kujisafisha na bado
  haitasaidia.

  Kama kweli walishinda kwa kuchaguliwa kwanini wanataka kurudisha Image kwa wananchi, while walikupa kura
  kwa image, hapo walichakachua matokeo na hawajui wasimamie wapi, Wanaiga mwendo wa CDm wakidhani ndio image.

  Uliona wapi chama Tawala kinanunua watu waende kwa mkutano, pikipiki, mikokoteni, magari na watu wanapewa pombe
  kuna kitu hapo. Ili waje kukusikiliza au wanakuchiora tu pale.
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa na fisi anayezengea mkono wa binadamu akidhani utaanguka auokote. Pumba Pumba___

  Join Date : 2nd December 2009
  Posts : 49
  Thanks 0Rep Power : 0

  Ulikuwa wapi kupata akili toka 2009 halafu una post 49. Kichefu chefu kingine hakuna utabiri subiri shubiri
   
 9. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Endelea kuishi kwa matumaini...
   
 10. B

  BELUSKONI New Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: May 14, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ya JK ndio mnayoizungumzia hapa? Kwani itafika 2016? Subiri siku 90 zipite ndio utajua.
   
 11. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndoto za mchana mbaya unaweza ukaota unananii ****. Kama ndio mpango wenu mkaanze upya hilo halipo
   
 12. p

  plawala JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lazima ulienda kwa shehe yahaya,huo mda ukifika utakanusha mwenyewe
   
 13. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wapuuzi kama hawa dawa yao ni kuacha thread zao zikae bila comments ili wajue kwamba wanaongea upu upu tu. Cha msingi kila mmoja wetu aweke kumbukumbu ya hii thread ili ikifika 2016 tukumbushe huyu mjinga wetu na utabiri wake wa kipuuzi..
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Bunge la chadema siku hizi liko uraiani na kwa maana hiyo wabunge wa chadema bungeni (huku uraiani) ni wengi mno. Hata hivyo wamepeleka wawakilishi wachache kwenye Bunge la Mama Makinda na wanahisa wenzake ili kudumisha 'umoja na mshikamano' wa kitaifa. Kwa hiyo hata kama atabaki mbunge mmoja huko kwa Makinda anaweza kuwakilisha vema..

  Kwa maneno mengine ninachosema ndugu yangu ni kwamba kwa chadema kupoteza viti Dodoma itatatokana na utendaji wa ccm huku mtaani ambamo ndiko bunge halisi la chadema limo. ajira, elimu bora, makazi bora na sio mbavu za mbwa, umeme, hospitali etc maana hivi ndivyo vinavyoongelewa na wananchi wenyewe kwenye bunge la wananchi (uraiani). Time will tell kama ccm wanaweza kutimiza haya, bila hivyo itakuwa ngumu sana.
   
 15. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  wewe ndo una maoni na mitazamo tofauti.... jikaribishe mwenyewe
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  RIP chama cha mafisadi.
   
 17. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Alishindwa sheikh Yahya Mtakuwa ninyi, utabiri wenu na wa Sheikh Yahya unaongozwa na nguvu za giza zinazofanya kazi CCM na sio Chadema.
   
 18. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mmezoea mambo ya kupiga ramli kwa waganga wa kienyeji nafikri amekuambia maji marefu, tumia ubongo kufikiri acha kutumia tumbo, mkama amewapa kazi ngumu hapa jf
   
 19. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hoja imefanyiwa marekebisho kidogo soma hapo kwenye box na kichwa cha habari, mtoa hoja alijichanganya
  mtoa hoja alichanganya mambo kidogo, nadhani ni mgeni hapa Tanzania, atakuwa ni mkenya wa hivi vituo vya redio, tatizo lake hajui hipi ni CDM NA CCM, na hajui vijana ni wapi na wazee ni wazee,
  maana vijana wengi bado wanakula msoto kutokana na hii serikali ya kikwete hivyo kuonekana wazee na vigogo wanaotumbua kodi zetu jamaa anadhani ndio vijana.
  tumsamehe taratibu ataelewa maana ameahidi kuwa hapa jamii forums
   
 20. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Wanachama wa CCM waliobakia ni wale wanaoneemeka na mfumo wa kifisadi na wale wenye matatizo ya akili.
  Unaweza ukajiuliza mwenyewe kati ya hayo makundi mawili hapo juu we uko wapi.
   
Loading...