Uchaguzi 2020 CHADEMA kuwa na nguvu baadhi ya miji michache tu Tanzania na kutokuwa na nguvu vijijini Tanzania ndio siri yao ya kushindwa uchaguzi ujao

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,888
Miaka yote Chadema imekuwa ikijijenga kwenye miji michache mno Tanzania

Ilichagua vimiji vichache tu kwa mikoa michache tu ya Tanzania na kujijenga na kuacha miji mingine ya mikoa.

Ukienda baadhi ya mikoa wanakosema Wana nguvu unakuta mkoa una miji mfano minne wanachagua mji mmoja wanajijenga hapo wanaridhika

Vijijini huko hawakuhangaika nako kabisa Hakukuwemo kwenye upanuzi wao na ndiko asilimia 80 ya wapiga kura wapo

CCM vijijini ndiko ilikupa kipaumbele ikijua walio wengi wanaishi vijijini hivyo kuhakikisha kila kijiji kina tawi la CCM na miji yote nchi nzima kuhakikisha kila mtaa una tawi la CCM active wakati Chadema Hilo hawana mataei hata kwenye miji yako sehemu chache tu na Ni machache yaliyo active mengi hata waliyokuwa wamefungua kipindi Cha Slaa na Lowassa yalishafungwa yamebaki machache tu active

Lisu alisema uchaguzi wa mwaka huu mgumu Ni kweli Ni mgumu kwa Chadema sababu kwa Mara ya kwanza Chadema inafanya uchaguzi bila kuwa na pesa chama hakina pesa na mgombea Hana pesa pili uchaguzi Ni mgumu kwa chadema sababu kinafanya uchaguzi bila kuwa na sera ya kueleweka kwa wananchi kuwa kinasimamia Nini

Tatu ni mgumu kwa Chadema kwa sababu Matawi mengi ya Chadema mijini yalishafungwa na Ni machache tu yaliyopo ndio yako active

Nne mwamko wa watu kea Chadema Kama chama Ni mdogo hata wagombea wa Chadema hawakinafi chama wanahangaika kujinadi wao as individuals

Hata ukiangalia humu jamii forums Chadema waliojaa humu wananadi zaidi watu wao Sio Chadema Kama chama!!! Na wagombea wanazunguka kujinadi Mimi Mimi mimi!!!! Umimi mwingi kuliko chama
 
Yaani baada ya kuona umasikini mwingi upo vijijini, ujinga mwingi upo vijijini, taarifa za kutosha na za maana hakuna vijijini, tume sio huru halafu eti vijijini ni nngome ya CCM!
 
1.Mlisema hakuna kufanya sisasa tangu 2015

2.Mkasema lazima upinzani ufe kabla ya 2020,

3.Mmetunga Sheria nyingi kuzuia Uhuru wa watu kupata habari,

4.Mmetunga Sheria ya msajili wa vyama vya siasa kudhibiti chadema

5.Mmeua, kuteka kuiumiza wafuasi wa chadema

6.Mmeua biashara za watu ambao Wana mrengo wa chadema kwa kutumia TRA

7.Mmeba bika kesi za uhunumu uchumi wanachama na wapenzi wa chadema

8.Mmeua matajiri wote walizokuwa sponsors wa chadema

10.Mmemfilisi na kumdhokfisha kiuchumi mwenyekiti wa chadema.

11.M meawafanyia fujo mgombea wa chadema ili asishindwe kupata wadhamini

12.Mmechhoma ofisi za chadema Arusha , Lindi na njombe,

13.Mmewarubuni kwa rushwa wabunge na madiwani wa chadema

14.Mmetumia hila na mahakama kuwapoka umeya kwenye Majiji

We YEHODAYA we waonee huruma chadema waliyo na wanayoyapitia Ni magumu.

Hata kama we ni ccm damu lakini kuwa na roho ya ubinadamu, hubiri amani na upendo, ili nchi ipate kubarikiwa
 
Kumbe unajua kuwa Chadema wana nguvu baadhi ya maeneo mkuu, sasa sihuwa mnasema wewe na mwenyekiti wako kuwa Chadema imekufa?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom