hugochavez
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,907
- 1,009
Kuna kautaratibu kanaanza kuzoeleka hivi sasa kwenye vyama vya siasa ka kuwa na mgombea urais wa kudumu. jambo hili ni hatari sana na ni tishio kwa ustawi na ukuaji wa demokrasia.
CUF ina mgombea wake wa kudumu prof Haruna Lipumba na sasa CHADEMA nayo inaonekana kuwa na utaratibu huo ambapo mh Edward Lowassa ndio mteule wa kudumu wa urais wa chama hicho.
Nimekaa nikitafakari na kujiuliza bila kupata jibu la wapi Tunaipeleka demokrasia kama Taifa.
Hivi karibuni, akiwa Kenya kushiriki mazishi ya waziri mmoja mwenye asili ya kimasai, Aliyekuwa mgombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chadema Edward Lowassa alieleza kuwa atagombea tena urais kwa tiketi ya chama hicho hali inayoashiria kuwa hii ni style mpya kwa nchi yetu ambapo tunakuwa na wagombea urais wa kudumu.
Maswali ya kufikirisha.
1. je hakuna vikao rasmi ambavyo vinahusika kuchakata wagombea wa urais na nafasi zingine za kisiasa kwenye vyama hivi? mfano kamati kuu ya chadema, baraza kuu la cuf, na mkutano mkuu wa vyama hivyo? unashauriwa na mkeo usiku asubuhi yake unatekeleza?
2. katiba za vyama hivi zinasemaje kuhusu suala la hili?
3. ndio aina ya demokrasia mpya kwa nchi yetu?
4. hizi kelele za kunyooshea wengine kuwa madikteta, kwanini tusingeondoa mabanzi kwenye macho yetu kwanza ndio tuwanyooshee wengine?
karibuni kwa mjadala. matusi NOOO