CHADEMA kuwa na hofu na Majaji wa Mahakama Kuu ni dalili mbaya, tunaashiria kuwa Mbowe ana makosa

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,165
4,581
Kama hana kosa kwa nini kuwa na hofu kuwa atatiwa hatiani kwa makosa ambayo hajafanya?

Jaji ni mwamuzi anayeangalia ushahidi wa pande zote mbili. Na anaamua kwa kufuata haki.

Tulipinga kwa nguvu zote Jaji Limuvanda kusikiliza kesi ya Mbowe. Sasa jaji Nsiyani naye tunakuwa na hofu nae.

Tutulize munkari tusibiri kuona mahakama ikienda haki tuache lawama za mapema.
 
Nenda kwenye pointi acha kujitoa ufahamu kisa shilingi 7000/-Jaji aliyekuwepo alipaswa kufanya nini baada ya hati ya mashitaka kuonekana kuwa na kasoro kisheria.Majaji ni matawi CCM ,mahakama ni matawi ya CCM haki haipo .Bila damu kumwagika
 
inamaana na huyu mpya hawana imani naye tena jamani sasa mbowe anateseka jela mjuwe bora kesi isikilizwe iishe ijulikane kama anatoka au anabaki
 
Nenda kwenye pointi acha kujitoa ufahamu kisa shilingi 7000/-Jaji aliyekuwepo alipaswa kufanya nini baada ya hati ya mashitaka kuonekana kuwa na kasoro kisheria.Majaji ni matawi CCM ,mahakama ni matawi ya CCM haki haipo .Bila damu kumwagika
jaji alitakiwa kumwachia mtuhumiwa ili akamatwe tena kesi ianze upya sasa kunatofauti gani kati ya kumwachia akakamatwa tena na kuwaambia wakarekebishe hati?
 
Mawazo ya KIJINGA ULIYONAYO kumkataa JAJI AU HAKIMU ni Jambo la kawaida kwenye Kesi pale unapoona mwenendo wa Kesi yako unakiukwa kwa makusudi ni Mjinga tu ndio ana Mawazo kama yako

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Wewe .mwenyewe jiulize, imekuwaje Jaji Elinaza alitamka waziwazi kuwa Hati ya mashitaka iliyoletwa na upande wa mashitaka ilikosewa Sana, sasa badala ya kuitupilia mbali kesi hiyo, eti yeye anasema kuwa ni LAZIMA kesi hiyo iendelee, bali anawaambia upande wa prosecutors, eti wakairekebishe!

Wewe uliwahi kuona wapi maamuzi ya aina hiyo yanafanywa, tena na Jaji wa Mahakama Kuu?

Hivi hapo kwa Mheshimiwa Mbowe kutaka kubadilishiwa Jaji, baada ya kuona dhahiri kuwa Jaji huo anafanya upendeleo wa dhahiri, ndiyo mnaita kuwa ni woga wa upande wa utetezi?
 
Ni Mbowe anashtakiwa, siyo CHADEMA.

Acha kupotosha. Halafu ni haki ya mtuhumiwa kumkataa jaji, na ni wajibu wa jaji kutafakari na kujitoa kwenye kesi yenye hisia hasi dhidi yake. Hata kesi ya Lema Arusha, Jamuhuri iliomba Hakimu ajitoe kwa sababu mke wa Lema alikuwa rafiki wa huyo Hakimu.

Linapokuja suala la kimahakama, ukiingiza siasa na kujitoa ufahamu, ambayo sometimes hauna, lazima utakosea.

Jamuhuri wameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye kesi hii. Wanabutua sana. Very weak!
 
jaji alitakiwa kumwachia mtuhumiwa ili akamatwe tena kesi ianze upya sasa kunatofauti gani kati ya kumwachia akakamatwa tena na kuwaambia wakarekebishe hati?
Hoja ni kwamba baada ya kusema hati ya mashtaka ina makosa ikarekebishwe maana yake tangia hapo hakuna mashtaka maana mashtaka yanaanzishwa na hati ya mashtaka. Kusema hati ina makosa na usimwachie si sawa.
Jaji alipaswa kutimiza wajibu wake kisheria, hayo mengine ya kukamatwa tena si yake.
 
Ni Mbowe anashtakiwa, siyo CHADEMA.

Acha kupotosha. Halafu ni haki ya mtuhumiwa kumkataa jaji, na ni wajibu wa jaji kutafakari na kujitoa kwenye kesi yenye hisia hasi dhidi yake. Hata kesi ya Lema Arusha, Jamuhuri iliomba Hakimu ajitoe kwa sababu mke wa Lema alikuwa rafiki wa huyo Hakimu.

Linapokuja suala la kimahakama, ukiingiza siasa na kujitoa ufahamu, ambayo sometimes hauna, lazima utakosea.

Jamuhuri wameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye kesi hii. Wanabutua sana. Very weak!
Chadema ni watu kama mimi na wewe.
 
Kama hana kosa kwa nini kuwa na hofu kuwa atatiwa hatiani kwa makosa ambayo hajafanya?

Jaji ni mwamuzi anayeangalia ushahidi wa pande zote mbili. Na anaamua kwa kufuata haki.

Tulipinga kwa nguvu zote Jaji Limuvanda kusikiliza kesi ya Mbowe. Sasa jaji Nsiyani naye tunakuwa na hofu nae.

Tutulize munkari tusibiri kuona mahakama ikienda haki tuache lawama za mapema.
Haki ni pamoja na kufungwa.....ama kuachiwa yote mkubali
 
Back
Top Bottom