Elections 2010 Chadema kuutwaa uspika?

Status
Not open for further replies.

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Kwa heshima ambayo Dr. Slaa imejijengea katika taifa letu na hata kwa wabunge wa Chadema na CCM kuna uwezekanno mkubwa kuwa Chadema watatoa spika wa bunge mwaka huu.

Dr. Slaa anao mtandao mpana ndani na nje ya chama chake. Pia kuna mtandao wa vijana ambao Zitto anao ndani na nje ya Chadema. Ni dhahiri kuwa uspika kutoka Chadema ni jambo la kutegemewa sana. Kama hii haitoshi, wabunge aina ya Mwakyembe, Sitta, Kilango Malecela na wapigaji wengine ndani ya CCM hawawezi kamwe kumpigia Anna Makinda kura ambaye ataendeshwa na wakubwa wa CCM wanaotetea ufisadi. Bado kuna wabunge wa Chadema waliokihama chama chao na kuingia CCM nao wanamtandao mpana ndani ya CCM. wote hawa wataleta kura za uspika kwa Chadema. Huu ni mwaka wa ushindi.
 
kweli? tusubiri tuone , taifa kwanza chama badaye, na huyu mama ana abdallah yeye anataka nini? hazeeki tu?
 
kweli? tusubiri tuone , taifa kwanza chama badaye, na huyu mama ana abdallah yeye anataka nini? hazeeki tu?

Kwanza wabunge wanawake wa CCM kwa heshima ya Dr. Slaa hawatampigia mwanamke. Anna Makinda atapata kura za mafisadi tu ambao hawakubaliki na wabunge wengi wa CCM.
 
pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Nahisi chichiem wamejikaaaaaaanga!
 
Siku 10 tu zimepita na tayari wana JF, the great thinkers wameishasahau kwamba ccm iliba uchaguzi. Kama ccm imeweza kuiba uchaguzi mchana kweupe mbele ya waangalizi wa kimataifa na kitaifa, watashindwaje kuchakachua uchaguzi wa spika ndani ya jengo? Hapa kumbe hakuna great thinkers ni polojo tu! Chadema watashinda uspika endapo tu kikwete ameamua kumpoza Dr. slaa katika mkakati wa kutibu madonda, vinginevyo forget it.
 
kawaida yetu kusahau mpema, shamaba la bib hilo.....
 
Siku 10 tu zimepita na tayari wana JF, the great thinkers wameishasahau kwamba ccm iliba uchaguzi. Kama ccm imeweza kuiba uchaguzi mchana kweupe mbele ya waangalizi wa kimataifa na kitaifa, watashindwaje kuchakachua uchaguzi wa spika ndani ya jengo? Hapa kumbe hakuna great thinkers ni polojo tu! Chadema watashinda uspika endapo tu kikwete ameamua kumpoza Dr. slaa katika mkakati wa kutibu madonda, vinginevyo forget it.

Huko bungeni kwani hakuna nguvu ya umma? Kusimamia uchaguzi wa spika kuna macho mengi yanaangalia. Nina imani haitakuwa rahisi kuchakachua. Kuiba kura uchaguzi wa wabunge na rais kunatokana na kukosa waangalizi wa kutosha wa kulinda kura. Huko bungeni kuna watu wengi wa kutosha kuzuia wizi wa kura.
 
huko bungeni kwani hakuna nguvu ya umma? Kusimamia uchaguzi wa spika kuna macho mengi yanaangalia. Nina imani haitakuwa rahisi kuchakachua. Kuiba kura uchaguzi wa wabunge na rais kunatokana na kukosa waangalizi wa kutosha wa kulinda kura. Huko bungeni kuna watu wengi wa kutosha kuzuia wizi wa kura.

mmeshaanza tena, uchaguzi wa rais mlisema mtashinda kwasababu mngelinda kura zenu lakini wapi!! Sasa mnaanza kujinadi na ushindi wa spika halafu mkiukosa nahakika mtadai uchakachuaji!!!!!
jamani sasa tumechoka na porojozenu!!!!
 
Kwa kuteua akina mama kwa nafasi za Uspika na Naibu wameogopa nguvu iliyo mbele!!!!! Au labda wamelenga udhaifu wa waswahili mbele za wanawake!!! Sijui ngoja tuone kwani kesho si mbali. Uspika ni Chadema tu Mwanamapinduzi Mabere Marando. Namuombea Mungu!!!!!!!!
 
mmeshaanza tena, uchaguzi wa rais mlisema mtashinda kwasababu mngelinda kura zenu lakini wapi!! Sasa mnaanza kujinadi na ushindi wa spika halafu mkiukosa nahakika mtadai uchakachuaji!!!!!
jamani sasa tumechoka na porojozenu!!!!

Kuna msemo wa Mungu si athmani. Kwanza idadi ya watakao kuwepo itajulikana vizuri kwa hivo ule uchakachuaji kama wa NEC itakuwa vigumu kufanyika. Kura zitalindwa na Makamanda wakuu.
 
kwa heshima ambayo dr. Slaa imejijengea katika taifa letu na hata kwa wabunge wa chadema na ccm kuna uwezekanno mkubwa kuwa chadema watatoa spika wa bunge mwaka huu.

Dr. Slaa anao mtandao mpana ndani na nje ya chama chake. Pia kuna mtandao wa vijana ambao zitto anao ndani na nje ya chadema. Ni dhahiri kuwa uspika kutoka chadema ni jambo la kutegemewa sana. Kama hii haitoshi, wabunge aina ya mwakyembe, sitta, kilango malecela na wapigaji wengine ndani ya ccm hawawezi kamwe kumpigia anna makinda kura ambaye ataendeshwa na wakubwa wa ccm wanaotetea ufisadi. Bado kuna wabunge wa chadema waliokihama chama chao na kuingia ccm nao wanamtandao mpana ndani ya ccm. Wote hawa wataleta kura za uspika kwa chadema. Huu ni mwaka wa ushindi.

i wish this was true!!
 
pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Nahisi chichiem wamejikaaaaaaanga!
tUWE REALISTIC JAMANI... HII PEOPLE'S POWER INATOKA WAPI... WANAOPIGA KURA NI WANACHI WA KAWAIDA AU WABUNGE?

TUTULIE TUSUBIRI MATOKEO, TO ME MARANDO WA TRICKY CHOICE
 
Hizo kura ni za siri au ni zile za kumhoji mbunge mmoja mmoja? Maana uchaguzi wa spika ni CCM versu UPINZANI; hakuna jinsi upinzani unavyoweza kushinda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom