Elections 2010 Chadema kuunda kambi ya Upinzani Bungeni

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
524
225
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema majina ya wabunge wa viti maalumu yatatangazwa wiki hii kwa ajili ya kuapishwa pamoja na walioshinda kwenye majimbo, ambavyo vitaamua ni chama kipi kitaunda upinzani rasmi bungeni.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu, alisema hivi sasa wapo katika mchakato wa kupitia majina ya wanawake wanaowania nafasi hizo yaliyotumwa kwao na vyama vya siasa vilivyopata wabunge wa majimbo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.


Majina hayo yanatakiwa kupitishwa haraka iwezekanavyo na Nec ili kufanikisha mchakato wa kuwaapisha wabunge pia washiriki kumthibitisha Waziri Mkuu atakayeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete wiki hii.
Aidha, majina hayo yanapaswa kupitishwa kabla ya kutangazwa kwa Baraza la Mawaziri ambalo pia huwahusisha wabunge wa viti maalum.


Kiravu alisema kuna nafasi 102 za wabunge wa viti maalumu wanawake na kwamba kila chama kitapata kulingana na idadi ya kura kilichopata kwa upande wa wagombea wabunge wa majimbo.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepata wabunge wa majimbo 186 ambapo mwaka 2005 walikuwa 205. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejizolea wabunge 22 ambapo mwaka 2005 kilipata watano tu. Chama cha Wananchi (CUF) kimepata wabunge (24) wakati NCCR-Mageuzi kimepata wabunge wanne.
United Democratic Party (UDP) na Tanzania Labour Party (TLP) kila komoja kimepata mbunge mmoja. Mwaka 2005 CCM kilipata wabunge 59 wa viti maalumu, Chadema waliambulia viti sita, CUF viti 13.


Kulingana na fomula ya kura za wagombea ubunge majimboni, CCM mwaka huu itapoteza viti maalum huku vyama vya upinzani vikiongeza idadi hiyo.


Ingawa CUF wana viti 24 vya ubunge majimboni ikilinganishwa na Chadema, uwezekano wa Chadema kuunda serikali kivuli na kuwa upinzani rasmi bungeni ni mkubwa kutokana na idadi kubwa kura za wabunge.


Chadema inakadiriwa kuwa huenda ikapata wabunge wa viti maalum kati ya 25 na 30 mwaka huu, hivyo kutimiza sharti la kisheria la kuwa na angalau wabunge 38 ili kuunda upinzani rasmi bungeni.Source : NIPASHE 8th November 2010
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom