CHADEMA kutumia Helkopta nne katika M4C kushambulia mikoa yote Tanzania

Kumbe unaakili yakuweza kuainisha mambo hivi ? kwanini usinge anza na ccm kuwaambia yafuatayo

1. safari moja ya JK na ujume wake inajenga visima vingapi ? ama hospitali ngapi .

2. Land cruiser V8 moja nisawa na dispensary 4 yapo mangapi kwenye serikali ya CCM?
3.kodi wachukue ccm lakini maendeleo yafanywe na CDM
4. milioni kumi sa msiba mlio zinge nunua madawati ya shule ngapi ?

Mbona haya madogo sana huyaoni ama ni sawa naule usemi unaosema nyani haoni kundule ?
 
Ni aibu kuonyesha udhaifu wa fikira zako hadharani.Unajua bei ya lita moja ya mafuta ya helkopta? safari moja what do u mean? ujenzi wa darasa moja ni kiasi gani? kisha rudi tujadili.
 
Nina wasiwasi kama umechangia cho chote!

Kila lengo lina objectives zake! Lengo la M4C siyo kujenga miradi ya maendeleo ni kutoa elimu ya uraia, haki na wajibu wa raia, kuelimisha wananchi wajibu wa serikali na kuelezea sera za CHADEMA.

Kujenga miradi ya maendeleo kunahitaji strategy tofauti na objectives zake ikiwa ni pamoja na kuandaa wataalamu wa kada mbalimbali.
 
SAM_2755_thumb%25255B2%25255D.jpg

Hii moja tu iliwasumbua, zikifika nne si watakoma....M4C forever VIVA CDM
 
Chadema mnawachangisha wananchi pesa sasa mnaanza kuzitafuna kwa njia tofauti ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi.

Duh na wewe unazitamani ,waombe basi na wewe mkasaidiane kutafuna.:baby:
 
jambo jema sana.

Lakini inabidi kuwa makini sana kwani ni rahisi sana kwa watawala kummaliza kiongozi wa upinzani anapotumia chombo cha anga kwa sababu visingizio ni virahisi mno. mathalani hali ya hewa, ubovu wa engine ya ndege iliyowabeba marehemu n.k, Kama nchi jirani vile huwananatumia sana hizi.
 
Ndio maana siku zote nasema kuna tofauti kubwa kimuundo na kiufanisi kati ya vyama vingine na CHADEMA. Wakati vyama vingine vikifanya kazi ya uchaguzi (CCM, CUF, TLP, UDP, PONA, UPDP, DP, ............................) na hivyo kuwa ni vyama vya msimu, CHADEMA inafanya kazi ya siasa. Kazi ya siasa si kusubiri uchaguzi, bali ni kazi ya kudumu kama uhazili, uhasibu, udaktari na kzi kama hizo. CCM na vyama vingine vinavyoendeshwa kiccmccm, vimerithi mfumo wa chama uchaguzi na mbaya zaidi vikawarithisha dhana hiyo watendaji wa serikali. Hivyo CHADEMA inaonekana inakwenda kinyume na siasa za kistaarabu (kwa mujibu wao). Swali kwa CCM, kama kazi ya siasa ni ya wakati wa uchaguzi kwa nini mnapokea ruzuku kila mwezi?
CHADEMA kanyaga twende, hayo ndio matunda ya kodi yetu. Hawa chama uchaguzi wanaopokea 2 billion kwa mwezi za kupika majungu kwenye vijiwe vya kahawa na zumna waachwe wasinzie.
 
piteni kila mkoa na kila wilaya,fungueni ofisi kila kona ya nchi hii ili tuepukane na dhana potofu ya kuwa Chadema
ipo mijini tu,bendera zetu zikianza kupepea kila kona MAGAMBA hawatapata usingizi,watabaki kuweweseka tu.
 
kutumia helikopta ni mbinu nzuri kwa ajili ya muda kuwafikia wengi? miaka mitatu iliyobaki ni michache
 
Chadema mnawachangisha wananchi pesa sasa mnaanza kuzitafuna kwa njia tofauti ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi.
Acha hizo CDM inajengwa kwa nguvu ya wanachama na wala si vinginevyo! Fikiri kabla haujapost
 
Chadema mnawachangisha wananchi pesa sasa mnaanza kuzitafuna kwa njia tofauti ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi.
We chezea nguvu ya umma, pressure inapanda, pressure inashuka, huna hata hoja. Utaangukia pua.
 
Kila siku hua nasema cheti sio kuelimika, embu eleza serikali ya Chadema ni ipi kufikia kufanya comparison?
Hukuelewa reasoning ya huyo jamaa. Ni kweli kama ulivosema kuwa cheti sio kuelimika, msemo unaanza na wewe.
 
Gari moja la mbunge ambalo ni mali ya mtu binafsi wala hata haimgusi kabisa mlipa kodi lina jumla ya visima vingapi? Na safari moja ya jk nje ya nchi huwa inagharimu visima vingapi? Na kasafiri mara ngapi kwa huu mwaka? Jibu ukilipata utaniambia, na ujue M4C haitumii hela za walipa kodi, bali ni mchango wa M4C kwa ajili ya kuimarisha chama na mabadiliko ya baadae/
 
Sisi ndio tuliotoa na tunaendelea kutoa ili zitumike helikopta zingine. Ninyi mafisadi wa kiccm ccm mmefilisi nchi na hamtaki watu waelimishwe. SASA kimenuka kila kona!
 
Gari moja la mbunge ambalo ni mali ya mtu binafsi wala hata haimgusi kabisa mlipa kodi lina jumla ya visima vingapi? Na safari moja ya jk nje ya nchi huwa inagharimu visima vingapi? Na kasafiri mara ngapi kwa huu mwaka? Jibu ukilipata utaniambia, na ujue M4C haitumii hela za walipa kodi, bali ni mchango wa M4C kwa ajili ya kuimarisha chama na mabadiliko ya baadae/
Kwaiyo kama JK anachezea hela basi ni haki na nyie mchezee? Unasema hizo hela sio za walipa kodi je ni za nani? Kwani hazichangwi na wananchi?
 
Alafu wewe unafikiri kwa makalio. CDM ina watu wanaomiliki helikopter. Ila kwakuwa wewe ni mchumia tumbo huwezi kuwa na fikra wala umakini wa cdm peoplessssssssssssssss!!!!!! Sasa tunatoa helikopter nyingi tu kazi ifanyike,na huu ndio wajibu halali wa chama chochote cha kisiasa.
 
Msifurahie tu kuona magari na helikopta..wanaotoa fedha zao kama chama kama hiki kikishika dola lazima warudishe faida. Na hapo sasa sio chama tena,ni kila mlipa kodi mpaka mkulima wa kijijini,ambaye mahitaji yake ya msingi yako wazi.. Tunasonga mbele au tunarudi nyuma?
 
Back
Top Bottom