CHADEMA kutumia Helkopta nne katika M4C kushambulia mikoa yote Tanzania

Safi hii... Kuna wananchi wanaotoa macho ila hawaoni.. chopa zikawafanye waone ili tuikomboe nchi hii!


Wapuuzi wanaotaka hela zikachimbe visima ni wa kupuuza... Kwa rasilimali tulizonazo hatuhitaji kuchangisha wananchi ili tuchimbe visima... Tatizo ni CCM, M4C isonge mbele tukingoe chama cha Mabwepande madarakani
 
Hilo swali ulitakiwa kuuliza toka mwanzo kabisa. Si lazima kila unapotumia helkopta au ndege maana yake matumizi yatakuwa makubwa maradufu ukilinganisha na magari. Hivi mnajua kuwa kuna uwezekano pia wa kutumia helkopta au ndege kwa lengo la kupunguza gharama? Nilipokuwa katika kampuni moja, kwa nia ya kupunguza matumizi tuliamua wafanyakazi wetu watumie ndege badala ya magari. Ukitaka kujua kama matumizi ya helkopta yatakuwa na manufaa zaidi kuliko kutumia magari au la ni lazima ufanye ulinganifu:

Ukitumia helkopta utatumia siku ngapi, na kwa magari utatumia muda gani.
Note: Unapotumia magari unatumia siku nyingi zaidi (fikiria time price, accommodation and meals, risk costs zinazoambatana na muda mrefu wa kusafiri, n.k.). Kubwa zaidi ni achievement vs time spent ambayo ndiyo hupima tija (productivity) ya hiyo program.

(
Mkuu unaweza kutuwekea kiwango kilichopatika, na bajeti ya hizo helkopta?
 
Suala siyo kuwa chama kichanga, muhimu ni kuwa unaenda kuleta nini na kuna impact gani. Kwa hiyo unataka kusema kuwa kwa vile kuna simu, redio na TV, hakuna sababu ya JK kwenda America na Ulaya? Hakuna sababu ya mawaziri kwenda mikoani, hakuna sababu ya RCs na DCs kwenda vijijini? Ritz, sit down and reason. Kama watu wangekuwa na hiyo reasoning kusingekuwa na haja ya kiongozi yeyote kufanya safari yeyote, wala kufanya mkutano, wala semina yeyote. Ritz JF ni shule nzuri ya kupima reasoning ya kila mmoja.

Bams,
Jiografia ya Tanzania ipo wazi kama chama mkiamua kujigawa kila sehemu kuwafikia wananchi na kuweka kambi mnaweza kuliko kuruka na helkopta kama watalii na kufanya mkutano wa dakika kumi na wanakijiji na kuondoka.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna uwekezaji bora zaidi ya elimu. Yaani kumkomboa mtu kifikra. Hata wewe unahitaji hiyo elimu ili uondokane na mawzo mfu kama hayo hapo juu.[/QUOTE

Ahsante sana mkuu, kumbe unajua kuwa elimu ni muhimu... Haya, hizo fedha zikajenge shule na kuziwezesha kupata vifaa. Sidhani kama M4C inampatia mtanzania elimu inayomuwezesha kufanya uvumbuzi wowote. Na mawazo yangu sio mfu mkuu.
 
Bams,
Jografia ya Tanzania ipo wazi kama chama mkiamua kujigawa kila sehemu kuwafikia wananchi na kuweka kambi mnaweza kuliko kuruka na helkopta kama watalii na kufanya mkutano wa dakika kumi na wanakijiji na kuondoka.
Nyie mliyejigawa kwa miaka 50 mmefanya nini?
 
Mi nawashauri watumie michango ya wananchi pia kuibua miradi ya maendeleo na kutatua kero ambazo CCM imeshindwa kuzitatua.

Kwa mfano, asilimia 50 ya michango ya wananchi iwarudie wananchi wenyewe kwa kuboresha miundo mbinu hospitalini, kusambaza huduma za maji, kujenga nyumba za watumishi kwa mfano walimu na madaktari.

Naamini kwa kufanya hivyo, kwanza wataonesha nidhamu ya pesa za walipakodi, na miradi mingi itasimama kwa pesa kidogo huku ubora wa miradi ukishinda mbali ile iliyosimamiwa na serikali ya CCM
.

Lengo lako si jema bali kudhoofisha M4C!

Matumizi bora ya fedha na nidhamu ya matumizi ni pale tu fedha zinatumika kwa kazi zilizopangwa!

Kama unataka kuishauri CHADEMA ijenge miradi ya maendeleo basi ni heri ungeshauri ianzishwe operation nyingine kwa lengo hilo!
 
Hivi oparesheni sangara na M4C ni kitu kimoja? nitoeni ukungu wakuu

Kati ya vitu CDM hawaeleweki ni katika uchoraji wa mistari katika oparesheni hizi. Nakumbuka ilianza Operesheni Sangara, kikaja kitu kinaitwa Vua Gamba Vaa Gwanda sasa kuna kitu kinaitwa M4C. Binafsi natatizika pia na operesheni hizi. Ninavyoelewa Operesheni Sangara ni Operesheni mama na endelevu ambayo ndani yake inabeba operesheni ndogo ambazo ni M4C na Vua Gamba Vaa Gwanda. Sasa sijui niko sahihi kiasi gan katika hili maana nimekuwa nikisikia maelezo mbambalii.

Mleta bandiko yeye anaichukulia Operesheni Sangara kama ndiyo M4C. Ni suala linalohitaji mjadala
 
Acheni kuwahadaa wananchi yaani ruzuku ya chama mikoani imesitishwaa kwa ukosefu wa fedha leo unasema unahelcopter4.watanzania watakuja kugundua huo upuuzi watawasusa.

nyege za kisiasa unalopoka lolota acha hazkufai
 
CCM mwaka hu watakufa kwa presha pamoja na watoto wao wanaofaidi nation cake ya nchi.
 
Ushauri wako ni mzuri. I have the same Idea. Lakini najua wengi watakupuuza. M4C kwenda na utaratibu wa kuacha walau mradi mmoja katika kijiji au eneo wanalofanya operesheni hasa maeneo ambayo kuna pro-CCM wengi na kwa kweli wanashida sugu (Mfano ya Maji) ingeweza kuwa na impact zaidi kuliko wengi wapingaji wanavyodhani.

Nakumbuka hapa JF kuna mdau aliwahi hata kuja na picha za Vyoo vyenye nembo ya CDM/M4C kama ushauri wake kwa CDM kushiriki kwenye huduma za kijamii kwa kujenga walau vyoo vya abiria wanaosafiri na mabasi yaendayo mikoani. Mfano; Dar - Mbeya, Dar - Mwanza na Dar - Arusha nk. nk.

Faida ya M4C kwenda Sambamba na Ufunguzi wa Miradi ya CDM
1. Itafuta kabisa propaganda chafu ambazo zimekuwa zikienezwa dhidi ya CDM kwamba fedha zinazochangwa kweli zinatumika kwa maslahi binafsi.
2. Itaacha kumbukumbu isiyosahaulika kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba, miradi hiyo itakuwa na nembo ya CDM/M4C na hivyo kila mtu atakuwa na scar kichwani zaidi fursa ya kukutana na neno CDM/M4C muda wote kuliko ilivyo sasa, operesheni ikishafanyika basi imetoka.
3. Itaonesha picha halisi ya utayari wa CDM kuwaletea wananchi maendeleo.
4. Ni moja ya njia ya kuwa mbadala wa CCM maana kwa kweli CCM inaonekana kushindwa kuwajengea miradi ya maendeleo wananchi.
 
Lakini ukitoa elimu ya uraia halafu ukaonesha mambo yanavyotakiwa kuwa kuna ubaya gani? kwa mfano unaenda kuanzisha M4C Mtwara huko ambako pamoja na kuichagua CCM, lakini bado hawana huduma ya maji, wewe unaenda kutoa elimu, kwa michango hiyo hiyo kidogo ya wananchi, unachimba japo kisima kimoja kwa wakazi ambao wameichagua CCM haijawapa maji, lakini CDM katika M4C yao wametupa maji, huoni kama maneno na matendo yako yanamatch?

Ninachokiona ni kuwa CHADEMA ADDICTED, yaani kusifia tu pasipo kutoa ushauri wa kitalaam kusaidia chama. Maana sijasema pesa zote zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo, bali nimesema sehemu ya pesa hizo ionekane ikifanya vitu kwa vitendo, na matendo hueleweka kuliko maneno
.
 
Nashukuru sana mkuu kwa kuunga mkono hoja, this is what we call innovation, doing the same thing in a different way for the betterment of tomorrow!
 
Lengo lako si jema bali kudhoofisha M4C!

Matumizi bora ya fedha na nidhamu ya matumizi ni pale tu fedha zinatumika kwa kazi zilizopangwa!

Kama unataka kuishauri CHADEMA ijenge miradi ya maendeleo basi ni heri ungeshauri ianzishwe operation nyingine kwa lengo hilo!

sidhani kama umefikira kabla ya kupost. suala langu liko wazi wala halihitaji nguvu nyingi. Ni kweli ni M4C, kwani maana yake ni kuongea tu? ukiongea halafu ukatupia mradi mmoja japo kwa interval ya 1:30, kwamba kila baada ya vijiji 30 tutakavyo pita, basi tunawaachia kitu watakachotukumbukia kwa maisha yao yote kuna ubaya katika hili?

Tatizo lako nakuona wewe ni mchumia tumbo, kwamba michango yote tuliyochanga, iishie kwa viongozi wa chama tu. Hii kwa mtu anayefikiri vizuri si sahihi. Ni busara kubwa kuacha mradi baada ya kuwahutubia. Na hii itasaidia uwajibikaji
 
Utasikia inteligensia ya anga la tanzania inaonyesha kuwa chopa za CDM zinaweza kuleta maafa na kuatarisha usalama wa anga.Stay tune
 
unajua watu wanashindwa kuelewa gharama za kutumia helcopta ni sawa na kutumia magari haswa kama unafanya kazi in remote areas kama vijijini, ikumbukwe inabidi wanachama kulala na kula kule! kwa hiyo gharama za malazi na chakula wakati chopper ni mafuta tu then kila mtu anasambaa kivyake! Pia katika kuepuka fitna za Magamba za kukataliwa kulala katika guest houses huko!
 
Ushauri wako ni mzuri lakini ukumbuke kwamba kabla hiyo hela haijaanza kuchangishwa budget iliandaliwa ambayo ni ya elimu ya uraia haijachangishwa ya miradi. CIVIC education is so important to tanzanians b'se ccm inatumia mwanya wa wao kutokuelewa haki yao kuwanyonya. Hela za maendeleo wanakula ccm (za kodi na misaada). washauri ccm wafanye hayo kabla hawajaondolewa madarakani baada ya elimu ya uraia.
VIVA CHADEMA

Ni juzi tu LIWALO na LIWE, ameonja joto ya jiwe mwanza. Hakuonja joto hilo si kwa kukosa maneno mazuri ya kuwaambia wana mwanza, la hasha bali ni kuchoshwa na kusikiliza maneno yasiyoendana na utendaji wa vitu halisi. Sh=ishauri pesa yote ielekezwe kwenye miradi ile inayowezekana, bali sehemu ya pesa hizo ndiyo ifanye miradi. Ili M4C inapotoka mahali, kwanza watu wameelimishwa lakini pia wamesaidia kutatua kero moja iliyokuwa sugu na CCM wameigeuza kuwa ya kuzoeleka. ubaya hapo uko wapi?
 
Matumizi ya helkopta ni makubwa sana safari tatu za hizo helkopta zinajenga visima vya maji vitatu. Kwa nini msiwapelekee wananchi hizo pesa kwa kupitia miradi, safari moja ya helkopta unajenga madarasa mawili.

Kodi mkusanye nyie VISIMA wachimbie CHADEMA wacha wachangishe waizunguke nchi ili 2005 tuchukue dora tukusanye kodi tujenge visima kumbuka michango ni ya CHADEMA ni ya hiali lakini KODI ni sheria na lazima.
 
Back
Top Bottom