CHADEMA kutotekeleza operation UKUTA ulikuwa ni mpango wa Mungu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,682
149,886
CHADEMA walipotangaza operation UKUTA watu wengi waliwabeza na kuwapuuza kwa kiasi kikubwa na hata walipotangaza kusitisha maandamano yao kejeli,vijembe na maneno ya kuwabeza viliongezeka lakini kumbe ulikuwa ni mpango wa Mungu watu waje wajionee wenyewe wakati ukifika.

Nina hakika viongozi wa CHADEMA wangeendelea na mpango wao bila kurudi nyuma ikiwemo kutowazuia BAVICHA kufanya maandamano kama walivyokuwa wamepania na yangetokea madhara ya watu kuumizwa na hata kupoteza maisha,viongozi wa CHADEMA wangesemwa sana na kulaniwa pengine kutoka katika kila pembe ya nchi hii.

Wakati ule watu wengi walikuwa na imani sana na huu utawala na walikuwa hawaoni kilicho mbele yao kiasi kwamba kumkoso mh.ilikuwa ni kama mtu umefanya kosa la uhaini.

Nakumbuka hata Zitto alikuwa ni mmoja wa watu aliobeza maandamano ya UKUTA na kupitia ukurasa wake wa facebook aliandila maneno fulani ya kuwakatisha tamaa /kuwabeza CHADEMA juu ya mpango wao wa kufanya maandamano lakini leo hii Zitto huyu ni miongoni mwa watu waliobadilika sana kimsimamo kutokana na aina ya uongozi wa mh.

Binafsi naona ni bora CHADEMA /BAVICHA hawakutekeleza azima yao na hivyo kujivua lawama ambazo wangezipata ila muda ndio umedhihirisha kuwa waliobuni ile operation wakati ule walikuwa ni watu wenye kuona mbali na walikuwa na nia njema na nchi yao kuliko hata wale waliowabeza kwani hata maandamano yao yalikuwa ni maandamano ya amani na si vinginevyo.

Mimi nasema tumefika hapa tulipo leo hii kwasababu tumekuwa ni slow learners wa siasa za CCM licha ya kututawala kwa miaka 40 sasa.

Kwanini tumekuwa ni slow learners wa siasa za CCM na haya ndio matokeo yake?

Kwa mfano,baadhi yetu tulipoamua kumuunga mkono Lowassa licha ya tuhuma alizokuwa nazo ni kuwa tuligundua kuwa ni bora Lowassa alie ndani ya CHADEMA kuliko Magu alie ndani ya CCM kwasababu kama ni tuhuma tu hata Magu hakukosa tuhuma.

Niliamini hata kama Lowassa angekuwa ndio Raisi wa nchi hii asingeweza kufanya mambo kinyume na msimamo wa chama kwasababu chama kingeweza kumdhibiti tofauti na taratibu na siasa za CCM ambazo mtu ukiwa Raisi basi ndio unakuwa Mwenyekiti wa chama Taifa hivyo unakuwa na power ndani ya serikali na kwenye chama pia.

Huu ni mfano mmoja wa siasa na taratibu za CCM zilizotugharimu lakini bado watanzania tumekuwa wazito kujifunza(slow learners) na ndio maana kila baada ya uchaguzi tunalia na kulalamika.

Nasema hivi kwasababu naamini kama Lowassa leo hii ndio angekuwa Raisi asingeweza kuwatisha wabunge wa CHADEMA waliodhaminiwa na chama kwasababu yeye sio mwenyekiti wa chama na hivyo Bunge lingeweze kumdhibiti hata kama UKAWA ingekuwa na wabunge wengi Bungeni.

Mfano mwingine.Bunge limejaa wabunge wa CCM kwasababu mpaka sasa tumeshindwa ku-learn kuwa ni makosa wabunge wa chama kimoja ku-dominate Bunge maana tumeshaona matatizo yake ila kwasababu sisi ni wazito wa kujifunza(slow learners),tukaona tumpe tu na wabunge wengi matokeo yake leo hii tunalia na sheria ya makato ya mshahara ya asilimia 15 kwa ajili ya Bodi ya mikopo na mambo mengine mengi.
 
Tundu Lissu alishawahi kusema huko siku za nyuma kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kudai kuwa hataguswa na udikteta wa huyu jamaa.

Anatekeleza udikteta wake kwa awamu, alianza na wapinzani.

Akaudhibiti mhimili wa Bunge

Amekidhibiti chama chake cha CCM.

Hivi sasa anatamani sana kumalizia kwa kuudhibiti mhimili wa Mahakama.

Iwapo wanasheria hawatatumia nafasi yao vizuri kwa kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wao wa TLS keshokutwa, hakika Taifa hili litaelekea kubaya sanaa........
 
Tundu Lissu alishawahi kusema huko siku za nyuma kuwa hakuna mtu ambaye anaweza kudai kuwa hataguswa na udikteta wa huyu jamaa.

Anatekeleza udikteta wake kwa awamu, alianza na wapinzani.

Akaudhibiti mhimili wa Bunge

Amekidhibiti chama chake cha CCM.

Hivi sasa anatamani sana kumalizia kwa kuudhibiti mhimili wa Mahakama.

Iwapo wanasheria hawatatumia nafasi yao vizuri kwa kumchagua Tundu Lissu kuwa Rais wao wa TLS keshokutwa, hakika Taifa hili litaelekea kubaya sanaa........
Unaweza kushangaa hata hao wanasheria maadamu nao ni watanzania wale wale bado wanaweza kuchagua watu wasiofaa alafu kesho na keshokuwa wakaanza kulalama.
 
Swala siyo slow learners swala ni wakati gani huu ukandamizi unakua umekugusa.
Mfano kijana mwenzangu alitangulia kumaliza chuo stashahada, ule mwaka aliokaa bila kazi alikua kila akimuona Magu kwenye tv anahamisha na anakua critical kwenye ishu mbali mbali. Baada ya kupata kazi amebadilika siyo yule ambaye anaweza kukuchambulia kauli za mwanasiasa na kuuona uongo wa dhahiri sasa hivi kila kinachofanywa kwake sawa tu.

Huo ni mfano mmoja kati ya wengi na katika maswala mbalimbali.
 
Back
Top Bottom