Chadema kutokubali uchaguzi mdogo Arusha Mjini kunazua maswali!

I read the topic submitted by the author, in between the lines, and therefore come up with the following opinions; as being among the citizens of Arusha urban, educated, patriotic and exceedingly in love with CHADEMA politics, i would like to inform Tanzanians, firstly, the CDM is a strongest opposition political party in Arusha region and the Northern zone in its generality, the reason of which it could not made the party being coward of not going to another by-election. Secondly, CHEDEMA, an accurate party, in its form and content, with intensive discussion and for the betterment of the marginalized Tanzanians, it could not just, think of a new by-election, but rather, think of very expensive and unnecessary costs the by-election will incur. Upholding the notion of unnecessary costs, the CDM party, has affirmative thought of referring the matter to the Court of Appeal of Tanzania, as to oversee the irregularities of the previous decisions made by the High Court Of Tanzania avoiding the what we so called "miscarriage of Justice" by seeing the provision of justice by the current final house of justice.
 
Naomba nikusamehe kwani unaonekana hujui kwa nini tuli appeal!
Maskini umenisikitisha sana, kumbe hujui kilichojili hadi sasa!

Wewe ni mvivu sana!
 
Osokoni kichwa chako sio kizima sana. Kama wewe ni wa sisiemu baki huko huko. Lakini kwa chama makini, watu makini, viongozi makini, wafuatiliaji makini, wapembuzi makini wa mambo, hawawezi kukubali kosa na kutumikia adhabu bila kuhoji ikiwa adhabu yenyewe imetokana na dhuluma. Ishu kubwa sio kushinda kwani hata leo ukiitisha uchaguzi chadema itashinda na imeshashinda hata uchaguzi mkuu wa raisi ( chukulia matokeo ya uraisi ambako mlimweka jk kimakosa kwa uroho wenu wa madaraka na hofu ya kuishi maisha ya udigidigi kwa mali za wizi mlizoiba na kuishi nazo) chadema ilishinda na mkachakachua leo inawakosti. Hivyo hatuwezi kukubali kuingia katika uchaguzi hadi tuone kwamba kilichosemwa kinadhihirika kwamba si cha kweli. Acha kutumwa na magamba yako. Utaumbuka osokoni.
 
uwe mstaarabu kisa cha kuniita gamba ni nini? wewe unayejiita cdm hata kadi huna hata katiba ya chama hujui inafanana je sisi kwa tarifa yako ndio waanzilishi wa chama na makala kama hizi ni changamoto kwa chama chetu sasa usipende kuexpose ujinga wako kwenye jukwaa hili!

ulichokiandika hakifanani na mwana CDM, mwanachama asiyejua chama kinafanya nini?

Bahati yako nakusamehe kwa sababu umeCOPY na kuPASTE
 
Nashikwa na kigugumizi kuchangia mada hii, Hivi majaji wa Kesi ya LEMA na wale walioamua kezi za Igunga na Sumbawanga tofauti zao nini, CDM wakishinda, jaji mzuri, wakishindwa, jaji wa CCM. Haya mambo yanakuaje? si tuachane na haya mambo ya vyama vingi? Haya mambo ya wazungu bwana, Afrika tunadandia gari kwa mbele.

wewe ndo unadandia gari kwa mbele! hizi kesi umezifuatilia mwenendo wake mpaka mwisho au umesikia hukumu tu na ukaja kuchangia???
hukumu ya lema ilivuja b4 na kama maamuzi yalitolewa na majaji mahakamani iliyovuja ilitoka wapi kama siyo huko juu kwa wanaojina wenye nchi? Igunga ulisikia hukumu kabla ya kutangazwa mahakamani? dats y 2nasema igunga ilikuwa ya haki but cyo arusha ambako hukumu ilijulikana usiku kabla ya kutangazwa mahakamani
 
I read the topic submitted by the author, in between the lines, and therefore come up with the following opinions; as being among the citizens of Arusha urban, educated, patriotic and exceedingly in love with CHADEMA politics, i would like to inform Tanzanians, firstly, the CDM is a strongest opposition political party in Arusha region and the Northern zone in its generality, the reason of which it could not made the party being coward of not going to another by-election. Secondly, CHEDEMA, an accurate party, in its form and content, with intensive discussion and for the betterment of the marginalized Tanzanians, it could not just, think of a new by-election, but rather, think of very expensive and unnecessary costs the by-election will incur. Upholding the notion of unnecessary costs, the CDM party, has affirmative thought of referring the matter to the Court of Appeal of Tanzania, as to oversee the irregularities of the previous decisions made by the High Court Of Tanzania avoiding the what we so called "miscarriage of Justice" by seeing the provision of justice by the current final house of justice.

naomba nikurekebshe kdogo CHADEMA NI CHAMA TAWALA ARUSHA !!!!!!!
 
Huyu nae asahau ubunge, si anajifanya mfalme wa Arusha, atakula jeuri yake sasa. Na mahakama imewafumba midomo, imeonyesha kuwa sheria ni sheria,wa CCM pia wameenguliwa,
 
Hukumu ile ina mtego kwa Lema. Labda mwenzetu unaamka. Ile hukumu ilikuwa na makosa. Yaani kosa tofauti hukumu tauti. Pole sana kwa kutoelewa, ubarikiwe.
 
ulichokiandika hakifanani na mwana CDM, mwanachama asiyejua chama kinafanya nini?

Bahati yako nakusamehe kwa sababu umeCOPY na kuPASTE

wewe huna akili tena ni mjinga sana!! soma makala uelewe uchambue uchangie usi attack personalities attack issues!!
 
Mkuu Osokoni,
1. Naona umeamua kuweka habari kutoka kwenye Nipashe pasipo mwisho wa habari yenyewe kuweka source. Hii imetufanya wengi wetu tudhanie kuwa ni wewe ndio uliyeiasisi na kuiweka na hivyo kupokea mashambulizi mengi. Tungeendelea kuamini hivyo kama isingewekwa habari yanyewe, tarehe ya kuandikwa na jina la Mwandishi. Hata hivyo, tutaichangia mada kama ilivyo.

2. Kwa waliokuwepo pale Viwanja vya NMC siku ile ya Jumamosi ya tarehe 08. 04. 2012, watakubaliana nami kuwa 'kipande nilichonukuu' ndiyo haswa msingi wa CHADEMA na Lema kukata rufaa. Wananchi wa Arusha mpaka Mh Mbowe alipooa kauli ile walikuwa na AMRI na NIA ya kuingia tena kwenye uchaguzi na walidhamiria kulinda kura zao (kutokana na uzoefu walioupata kutoka Arumeru Mashariki juma moja tu lililopita) . Lakini Mh. Mbowe alieleza kuwa, "kuyakubali maamuzi yale ya Mahakama na Kukubali Kuingia Kwenye Uchaguzi Mdogo, Hata Kama Una uhakika kwa Kushinda, utakuwa umemaanisha kuwa, unakubaliana na mwenendo mzima wa mashtaka na shauri lenyewe. Kwamba CHADEMA na Lema, ni chama cha kuwadhalilisha wanawake; na ni chama cha ubaguzi. Lakini pia, hukumu ile ya kibaguzi na kionevu, itatumika kama rejea ya mahakama (Judicial Precedence) katika kutolea maamuzi siku zijazo. Watoto wetu wataonewa na kugandamizwa. Wataporwa Haki zao. Kuikubali hukumu ile, kutamaanisha kuwa wananchi maskini wa kitanzania, wataenda tena kugharamia uchaguzi ule mdogo (sikumbuki vizuri, ila nadhani alisema ni 4bn). Hukumu ile, haisemi hatma ya Mh. Lema kama anaruhusiwa kugombea au la. Amepewa hukumu ya kosa ambalo si la kwake"

3. Ukisoma makala hii tu kwa juu juu bila ya kumfahamu Mwandishi Mwenyewe wa Makala na aina ya uandishi wake utakuwa unakosea. Kwa wale ambao hawafahamu ni kuwa, uandishi wa habari wa Tanzania wa habari za kiuchunguzi/makala au michezo unafanana. Kwamba kuna waandishi wenye kambi ya Simba na Yanga. Na waandishi wa habari za Siasa, nao wako kwenye kambi hizo pia. CCM, CHADEMA, CUF n.k. Makala na habari za Muhibu Said tangu akiwa anaandikia gazeti la Mwananchi kama freelancer, zilikuwa zinaonyesha dhahiri upande aliopo. Na kwa muda wote, alikuwa akiripoti habari zilizohusu Chama Cha Wananchi (CUF). Alizunguka katika misafara yote ya Pr. Lipumba na hata lile tukio la yule mtoto inayesemekana kuiba sanduku la kura na kupigwa risasi na Mkurugenzi wa Temeke, ni yeye ndiye alikuwa anaripoti. Na hata alipojiunga na Nipashe, ameendelea kuandika, kwa asilimia kubwa, habari zinazomhusu Lipumba na chama cha CUF.
Hivyo, sikushangaa kusoma makala kama haya kutoka kwa mwandishi mwenye 'calibre' ya Muhibu. Ni nani amesahau namna Novatus Makunga (aliyewahi Kugombea Kura za Maoni Ubunge kupitia CCM) alivyokuwa anaripoti kampeni, upigaji kura na hata kuwasilisha matokeo ya awali katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Arumeru Mashariki?

- Ni Makunga aliyekuwa kila akiripoti habari za Sioi, anaweka picha za kampeni za urais mwaka 2010 kuonyesha watazamaji wa ITV kuwa wale walikuwa ni wahudhuriaji wa mikutano ya kampeni wa Sioi.

- Ni Makunga ambaye wakati akiripoti kuhusu watu waliojitokeza kwenye kupiga kura, alieleza kuwa " waliojitokeza kwenye upigani wa kura ni wazee tu, na vijana hawakuwepo, tofauti na wakati wa mikutano ya kampeni walikuwa wengi", wakati mtangazaji mwenzake, Asraj Mvungi 'akielezea kuwa Vijana walijitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, kama ilivyokuwa katika mikutano ya kampeni'.

- Ni Novatus Makunga huyu huyu, miezi michache baadaye, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai!

Kama Great Thinkers ( GT), inatupasa kuthink Critically.

sasa wewe umetumia akili kutafuta ukweli wa jambo na kutafuta mwandishi hivo ndivo jf inatakiwa kuwa sio kumshambulia mleta mada shambulia mada yenyewe you deserve to be a great thinker!!
 
Nimeelewa baada ya kupitia post za watu ambao kichwani zimejaa kuwa kama Lema asingekata rufaa basi hiyo ingejulikana ni.kweli pili kwenye hukumu yake hatakiwi kushiriki uchaguzi kwa miaka mitano kitu ambacho najua ni.kinyume na Human rights,nadhani pia ni kinyume na katiba ya Tanzania so ni jambo la msingi sana kwa CDM na Lema kwenda mahakamani kutetea haki yao
 
Mtu akitaka kujua kitu Mijitu inakimbilia kumwita gamba shame on u
 
I read the topic submitted by the author, in between the lines, and therefore come up with the following opinions; as being among the citizens of Arusha urban, educated, patriotic and exceedingly in love with CHADEMA politics, i would like to inform Tanzanians, firstly, the CDM is a strongest opposition political party in Arusha region and the Northern zone in its generality, the reason of which it could not made the party being coward of not going to another by-election. Secondly, CHEDEMA, an accurate party, in its form and content, with intensive discussion and for the betterment of the marginalized Tanzanians, it could not just, think of a new by-election, but rather, think of very expensive and unnecessary costs the by-election will incur. Upholding the notion of unnecessary costs, the CDM party, has affirmative thought of referring the matter to the Court of Appeal of Tanzania, as to oversee the irregularities of the previous decisions made by the High Court Of Tanzania avoiding the what we so called "miscarriage of Justice" by seeing the provision of justice by the current final house of justice.

Huo ung'eng'ge bwana. Umejitahidi. Tuswage hivo hivo tatakinyoosha mbele ya safari!
 
Mkuu huwa nakuamini sana lakini mada yako ya leo umeteleza kidogo.CDM imekata rufaa kwa sababu hukumu inasema Lema haruhusiwi kugombea tena mpaka miaka 5 ipite...

Mimi si mtaalam wa sheria, niko tayari kukosolewa. Nadhani hukumu ya kutogombea kwa miaka mitano ni pale kuvuliwa ubunge kunatokana na suala la rushwa jambo ambalo Lema hakuhusika na rushwa.
 
kumbe unaweza kugundua itikadi na akili za mtu kutokana thread zake. Mia

kumbe unaweza kugundua itikadi na akili za mtu kutokana thread zake. Mia

hapana...kwenye chembe za ukweli ni sahihi kusema...ukweli ambao hatuusemi sisi tunaitakia mema cdm ni kuwa ushindi wa uchaguzi wa 2010 ars ulitokana na wana ars kukipenda zaidi chama cha cdm kuliko mgombea. Nasema hivo kwa kuwa tuliowengi tunakerwa na hulka ya lema ya lugha zisizofaa kwa mtu wa hadhi yake na hili naweza kulithibitsha kwa kauli alizoropoka juzi wakati wa chagizo lililorushwa na star tv kuhusu makampuni ya simu, kauli zake zilinithibitishia lema ni mtu wa aina gani na pia uwezo wake wa kufikiri na kutenda. Kiukweli kwa ars ccm hata ikisimama na jiwe la cdm itashindwa but cdm wasitumie huo mwanya kutuletea wagombea wasio na hekima na staha na wapenda shari. Sababu nyingine ambayo haiwezi kunishawishi kumtetea lema nikiwa kama mpiga kura wa ars mjini ni uwezo wa mdogo alionao lema wa kuongoza, kutatua kero na kuletea maendeleo wana ars kwa kipindi alichokuwa madarakani...ambapo kila kikao full council alishindwa kutetea haki kwa hoja badala yake tumeshuhudia vurugu pekee na kupelekea mafisadi kuendelea kujinufaisha na mali za halmashauri na ushahidi upo wazi wala hauhitaji mbunge awe phd kuubaini. Nawasilisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom