CHADEMA kutohudhuria hafla fupi ya kukabidhi taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020

Nec wapuuzi tu. Sasa wanashindwa nini kujibu barua zinahusiana na covid 19.

Tena wangeweka hadharani ili chadema waumbuke.

Vinginenvyo nec ndo janja janja
 
Tumepokea mwaliko kutoka Kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kwa ajili ya Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu, aliyekuwa mgombea urais na aliyekuwa mgombea wa umakamu wa urais kuhudhuria hafla fupi ya kukabidhi kwa Rais taarifa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Chama kupitia barua ya Katibu Mkuu kimemjulisha Mkurugenzi wa uchaguzi kuwa hatutashiriki hafla iliyopangwa kufanyika Ikulu tarehe 21 Agosti 2021 kwa sababu zifuatazo:

1. Hakukuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020; kulikuwa na "Uchafuzi Mkuu" uliohusisha uporaji wa ridhaa ya wananchi kuchagua viongozi wao na ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki. Kwa sababu ya kukosa uhuru kama taasisi, Tume ya Uchaguzi ilishiriki moja kwa moja katika kuharibu mchakato wa Uchaguzi Mkuu na kusababisha kuwa na "Uchafuzi Mkuu".

Sisi hatuwezi kushiriki kwenye tukio lolote litakalohalalisha Uchafuzi Mkuu huo mbele ya macho ya jamii ndani ya Tanzania na kimataifa.

2. Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amepewa kesi ya kubambikiza ya ugaidi kwa sababu ya chuki za kisiasa dhidi yetu. Tunaelekeza nguvu na muda tulionao kufanya jitihada za kuhakikisha Mwenyekiti wetu na viongozi na wanachama wengine waliokamatwa kwa uonevu na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wanaachiliwa huru.

3. Aliyekuwa mgombea urais wetu na Makamu Mwenyekiti wa chama Bara , Mheshimiwa Tundu Lissu, 'alilazimishwa kukimbilia nje ya nchi ' kwa sababu ya vitisho dhidi ya maisha yake vilivyofanywa na vyombo vya usalama au kwa ushiriki au baraka za vyombo hivyo.

Alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nje ya Ubalozi wa Ujerumani, na isingekuwa wanadiplomasia wa Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kuingilia kati angeweza kudhuriwa na Jeshi la Polisi.

Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi amesema hadharani kwamba Mheshimiwa Lissu hatapatiwa ulinzi wowote wa polisi licha ya ukweli kwamba aliponea chupu chupu jaribio la mauaji la tarehe 7 September 2017, jaribio ambalo halijawahi kuchunguzwa na hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Bila kuhakikishiwa usalama na uhuru wake, ikiwemo kufutiwa kesi za uongo alizofunguliwa mahakamani kati ya 2016 na 2017, Mheshimiwa Lissu hajioni kuwa atakuwa salama kuweza kurudi nyumbani kushiriki kwenye shughuli za kisiasa za nchi yetu ikiwemo kushiriki kwenye tukio hili.

4. Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijajibu mpaka sasa barua ya Katibu Mkuu ya tarehe 25 Novemba 2020 yenye kumb. Na. C/HQ/ADM/20/TU/05/14 ambapo alitaka maelezo ni nani alisaini barua na fomu za waliotangazwa kuwa wabunge wa viti maalum na kutupatia nakala ya nyaraka husika kwa ajili ya kuchukua hatua kwa kuzingatia kuwa Kamati Kuu haijawahi kufanya uteuzi wala Katibu Mkuu hajawahi kuwasilisha orodha ya majina katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

5. Kwa sasa na kwa siku zijazo, agenda kuu ya chama chetu ni kuhakikisha tunapata Katiba Mpya itakayotengeneza mfumo huru na wa kidemokrasia wa uchaguzi kwa nchi yetu. Kushiriki katika mialiko na shughuli za Tume isiyokuwa huru ni kuipa baraka za kisiasa Tume hiyo, na kupunguza nguvu na ari ya jitihada za kufanya mabadiliko yanayohitajika katika nchi yetu.

Kutokana na sababu tajwa hapo juu Chama hakitatuma mwakilishi katika hafla hiyo na badala yake tutaendeleza nguvu kutetea Uhuru,Haki,demokrasia na Maendeleo ya watu.

Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 20 Agosti,2021

John Mrema

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya NjeView attachment 1899771View attachment 1899772
Aliyetuma hizi barua akili yake Kama ya mbowe tu.first page iko wapi?

USSR
 
Mama ninaamini wewe ni mcha Mungu. Kaa mbali na huo uovu wa CCM. Unajua kutoka moyoni mwako yaliyofanyika kwamba hayampendezi Mungu anayehukumu kwa haki. Kama utakaa mbali na uovu wa CCM, Mungu atakukumbuka wewe na familia yako atakapokuja kuhukumu kwa haki maana yeye hana upendeleo katika hukumu maana yeye ni mwenye haki. Kumbuka Mungu ni mkuu kuliko hiyo CCM.
 
Back
Top Bottom