MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,211
- 22,266
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni kuhusu uchaguzi huu. Hii pia imechangiwa na wengi wenu kunitumia PM kuniomba nitoe maoni yangu kuhusu mwenendo wa uchaguzi huu. Nimekubali kufanyia kazi maombi ya wengi.
Niseme kwamba kampeni hizi za mwaka huu ni za kipekee. Ziko tofauti sana. Wapiga kura wengi kwa sasa wana akili nyingi sana na hawasikilizi blah blah. Ilishazoeleka wagombea kutamka uongo ulio wazi na ahadi nyingi hewa ila kwa mwaka huu inaonekana kabla mgombea hajatamka kitu inabidi ajifikirie mara nyingi sana. Watu wanataka maelezo ya kina. Kwahiyo hakuna Chama chenye wakati mrahisi tunapoiendea tar 28 Octoba.
CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kimeonyesha kuleta changamoto kwenye uchaguzi huu hasa baada ya kupata mgombea jasiri na ambaye inaonekana wazi hakuna anachohofia. Chama hicho kina mtaji mkubwa wa kura za huruma kutoka kwa watu wanaoamini kuwa Lisu alitendewa ubaya na CCM. Bahati nyingine ya hivi karibuni ambayo inaweza kuwaongezea kura za huruma ni hiki kitendo cha NEC kumsimamisha Lisu kufanya kampeni kwa siku 7. Tukiachana na kura za huruma ni wazi CHADEMA watapata kura chache kutoka makundi mengine ya wananchi.
Kosa la kiufundi ambalo CHADEMA wamelifanya na litawagharimu kwenye sanduku la kura tar 28 ni kutobandika picha za mgombea wao kama walivyofanya vyama vingine. Ikumbukwe Lissu amekaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa na alikuwa adimu machoni mwa wapiga kura. Au chama kimesahau kwenye karatasi ya kupigia kura kuna picha za wagombea? Mabango kwa watu wa marketing watakubaliana nami ni nyenzo kubwa sana kwenye kuitangaza bidhaa. Mtu asiyejua kusoma itamsaidia sana kwenye kupiga kura. Watu kama wahadzabe mngekuwa mmewarahisishia sana.
Mimi nionavyo ndani ya CHADEMA kuna ambao kwa makusudi waliamua kumhujumu Lisu kwa kutoweka mabango. Au pia watu hao wameona tu Rais Magufuli anatosha kwahiyo wamsaidie kinamna. Ombi langu kwa Rais JPM asimsahau Mh Tundu Lissu kwenye teuzi za serikali yake ijayo.