CHADEMA kutoa msimamo mzito leo; Ni baada ya rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya

Tanzania hii nani anakujua wewe mpaka afuatilie maneno yako unajisumbue bure!

Mkuu, acha dharau za watoto wadogo. Wewe nani anakujua?? Hapa tunaheshimiana bila kufahamiana. Au unalazimisha ujulikane kwa ku-post comment ya kitoto kama hiyo?? That was very low, low low!!
 
icon1.png
CHADEMA, NCCR, WANAHARAKATI wamekusudia haya


Juzi, nilianzisha thread yenye tittle hiyo, ilianza vizuri na watu waliichangia. Katika uzi huo, nilijaribu kuonesha kutowezekana kwa Rais/CCM kubadili msimamo wao juu ya muswaada. Nilieleza kuwa CDM walichokifanya ni kuweka kumbukumbu tu kuwa tulimshauri Rais lakini hatukusikilizwa pindi maandamano na mauaji ya watu wenye jazba ya kudai uhuru wao yatakapoanza.

Modes waliimove thread hiyo na kuiweka kwa Ng'wana swale ambaye uzi wake ulikuwa unasomeka Rais Kiketwe na mazungumzo ya wajumbe wa CDM.

Nadhani mode mmejifunza kitu hasa kwa kutokuchakachua thread za watu, kwani nilichokijadili na walivyochangia baadhi ya wadau, ndicho kinachotokea leo, iwapo kweli Rais kasaini mswaada feki.

Mkuu si peke yako, kuna thread mtu alileta hapa kuhoji CDM kupeleka shauri kwa mwenyekiti wa CCM waliyempinga dodoma, ile post wakati najibu tu, ikarushwa rushwa
 
RIP TANZINIANS thoughts subirini mja aje mtakombolewa sawa enhee...
karibuni jukwaa la MK huku hamna maandamano wala vitisho poleni wafia siasa..
 
Unajuwa angeenda Zitto mambo yangekuwa tofauti kabisa, hii ndio faida ya kupekleka walevi wakajadili jambo la muhimu kama Katiba.

zito kakufanyeje tena awe bora kuliko jk na mbowe marafiki wa siku nyingi wakati jk akiwa anaenda mziki?
halafu ni hatua tu msije mkasema kama alivyosema celina na ag kwamba lisu hakuwa anahudhuria vikao vya kamati

 



hahaha!!! ati CCM wanacheza ngoma ya CDM...

mkuu kajipange upya bana!


Tuambie lini CCM wameanza kujadili kuanzisha katiba mpya au JK wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya alitumia minitisi za kikao gani CC au NEC iliyopitisha uundwaji wa katiba mpya.
 
Ahsante Mkuu kwa kutimiza yale aliyotamka pale alipokutana na wazee wetu wa dar, nakumbuka alisema anatajwa kuwa yeye ni dictator wakati siyo na kuahidi kuwa sasa atajaribu kuwa dictator kidogo.
 
Kwa mujibu wa wanasheria kulikuwa na njia mbili tu 1) Rais asisaini muswada ili urudi bungeni upya kujadiliwa 2) Au asaini then urudishwe bungeni ukafanyiwe marekebisho then ausaini tena sheria ya gharama za uchaguzi.

Kwa maoni yangu CDM walimtega JK kumwambia asisaini muswada wakati ulipitishwa kwa mbwembwe nyingi na mawaziri wake akiwepo Wasira aka Old baboon, Lukuvi, etc hivyo kutousaini kuidharirisha serikali yake, wabunge wake na chama chake. Bila shaka hata CDM walilijua hilo........ngoja tuone.
 
Comrades,

Kwa wale ambao tumepata kushiriki katika vikao vya kuandaa na kusaini "bilateral agreements" tumepata shida kuelewa walioandaa ajenda ya majadiliano yale walikuwa makini kiasi gani. Ina maana kifungu kwamba rais asisaini muswada kabla ya mabadiliko hakikuwemo? Kama kilikuwemo lakini wakakubaliana kutokubaliana katika jambo hili, mbona makubaliano yaliyosainiwa hayasemi hivyo? Hapo ndipo tulipopigwa bao la kisigina. Vifungu vyote viwili katika makubaliano yaliyosaini ni elastic. Hivyo, mpaka sasa, Kikwete hajayavunja makubaliano yale...
Joint statements inaweza ikasummarise yale ambayo ndio matokeo ya vkikao chao kwa hiyo huitaji kutaja mpaka na hadidu za rejea
 
Huyu jamaa uwa ananichekesha sana umemuona anavyojifariji na kujiliwaza kwa msongo wa mawazo ya katiba
Tuambieni lini CCM wameanza kujadili katiba mpya tuonyesheni ilani ya CCM kama ilitaja hayo kama si kucheza mziki wa Chadema ni kitu gani.
 
Mkuu, acha dharau za watoto wadogo. Wewe nani anakujua?? Hapa tunaheshimiana bila kufahamiana. Au unalazimisha ujulikane kwa ku-post comment ya kitoto kama hiyo?? That was very low, low low!!

Hakuna dharau ni hoja nzito tu, tatizo lenu mnajisahau mnadhani JF ni mali ya Chadema..

JF ni Forum huru kwa hiyo usitake wote tuwe Chadema, tuvumiliane ndio maana ya vyama vyingi
 
Hakuna Mwenye Hatimiliki Ya hii nchi bali Watanzania wenyewe.
Katiba sio ya chama fulani cha Siasa bali na Ya Watanzania Wenyewe.

Chadema Haikukosea, na hata kama mnaona walikosea ni wao(sio wamiliki wa nchi wala katiba).

Chakufanya ni sisi wenye nchi kuamua kupewa katiba sahihi na yenye manufaa, na katika kudai hili tunahitaji kuongozwa/kuelekezwa.

Mwenye kuonesha jitihada ndio husaidika kirahisi zaidi, sasa basi tuanze kuidai kwa nguvu zote tukiwa maofisini, mashambani, vyuoni, vijiweni na mashuleni mwetu na viongozi wataonesha njia.


Amka ewe Mtanzania paza sauti yako na utasikika, sasa sio muda wa kushabikia na kulaumiana maana walotugawa wanafurahia hilo na kutimiza matakwa yao.

Wamerithi kwa mkoloni (mwingereza) ile style ya "divide n rule". Sisi ni wamoja japo wao wanajitahidi kutugawa kwa misngi ya
1. Udini
2. Ukabila
3. Mavazi
4. Elimu
5. Jinsia nk.
Wao wanakula na kufurahi pamoja japo wanazo hizo tofauti hapo juu, wakati huo huo sisi tunashindwa kuungana na kudai chetu sababu ya tofauti hizo hapo juu.


Umoja Ni Nguvu Utengano Ni Udhaifu.
 
Katiba ni muhimu sana. Inawezekana vyama vya siasa vinatusaliti kwa manufaa yao. Vyote nia yao kubwa ni kuingia ikulu. Wananchi tunahitaji katiba itakayotufanya kuwawajibisha wanasiasa, kulinda haki zetu, kutuletea maendeleo, kulinda rasilimali zetu, kuongelea mfumo wa uchumi, elimu na huduma za jamii. Tunahitaji katiba kwa ajili ya leo na vizazi vijavyo.

Hakuna mwenye uhakika ni chama gani kitakuwa ikulu baada ya miaka kumi, ila wote tunauhakika tutahitaji kuishi na kufanya kazi kwenye mazingira bora sisi na watoto wetu ndani ya katiba bora.

Ni vyema tukajua sio CCM wala CDM watakatuletea katiba bora bali sisi wenyewe. ushabiki wa vyama uwe na kikomo kwa sasa ni Utaifa zaidi kuliko unazi.
 
Mkuu si peke yako, kuna thread mtu alileta hapa kuhoji CDM kupeleka shauri kwa mwenyekiti wa CCM waliyempinga dodoma, ile post wakati najibu tu, ikarushwa rushwa
Ndio maana tunasema hii mihimili mitatu iwe na watu wasioingiliana kisiasa kama Spika asingekuwa kutoka chama chochote angeangalia maslahi ya wananchi na taifa zaidi ya UCCM.

Na kama Waziri angekuwa sio mwananchama wa CCM angetanguliza maslahi ya taifa hata Mwanasheria mkuu asingewekwa pale na mwenyekiti wa CCM leo muswaada huu ungekuwa na sura nyingine.

Kwa hiyo laumu katiba mbovu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania sio Chadema ,Raisi ni taasisi anatakiwa asiegemee,lakini wapi Raisi kiziwi ,kipofu hawezi ona anakoelekea yeye anasukumwa tuu na fimbo ongozi
 
siamini leo hata wale wapenzi wa dhati wa chadema mmewageuka chadema. Mimi nitakuwa tofauti nanyi siku zote. kwa upande wangu, chadema did well (wamejaribu mpaka pumzi yao ya mwisho) sioni sababu ya kuwabeza. Na sema hivi, hongereni chadema kwa kufanya kila lililopo kwenye uwezo wenu. keep going, kama mtakuwa wastaarabu hata mimi nitajiunga nanyi very soon. again keep on going (kistaarabu) nami na wenzangu taja kuwaunga katika juhuzi hizi za ukombozi wa taifa hili kutoka kwa ccm.
 
Huo msimamo wenyewe uko wapi? Au utatolewa usiku wa manane?
Nimeumwa sikio kutoka makao makuu Chadema, baadhi ya msimamo watakaowaambia wananchi

1. Katiba inayoandikwa ni ya CCM wananchi wasubiri katiba yao.

2. Chadema haitahusika kwa namna yeyote na mchakato wa katiba mpya.

3. Katiba itakuwa batili kwa sababu sheria ya uundwaji wake imevunja katiba iliyopo.
 
Nimeumwa sikio kutoka makao makuu Chadema, baadhi ya msimamo watawaambia wananchi

1. Katiba inayoandikwa ni ya CCM wananchi wasubiri katiba yao.

2. Chadema haitahusika kwa namna yeyote na mchakato wa katiba mpya.

3. Katiba itakuwa batili kwa sababu sheria ya uundwaji wake imevunja katiba iliyopo.

Hayo yote si walikuwa na nafasi ya kuyajadili na mkulu pale Magogoni.
 
CDM WATUPE MAELEZO YA KUTOSHA. HAIWEZEKANI ASAINI HALAFU ASEME ATAREKEBISHA SHERIA. huo ni UTOTO. KAZI IANZE ILI AJUE UTANI BASI. LOWASA ALIMTUNZIA SIRI KUWA WALIKUWA WOTE RICHMOND BILA AIBU AKAACHA ATUKANWE HII NI ZAIDI YA KUIBA. IBA LAKINI USIWASALITI WENZAKO
 
Hayo makubaliano yaliyosainiwa ikulu mojawapo ya makubaliano hayo ni kwamba Rais hakutakiwa kuusaini huo muswada?

Ama hayo makubaliano ya kutokusainiwa yalikuwa "a word of mouth"?

Naona kuna namna JK kawapiga bao la kisigino, maybe JK alipowaambia amekubali mapendekezo yao walidhani hatausaini muswada, sasa kile kipengele cha kwenye taarifa kuwa muswada utafanyiwa hayo marekebisho kwenye bunge hapo januari hawakukiona?

Tatizo ni kwamba walipotoka kwenye kikao hawakuja straight forward, sasa JK alikuwa amejipanga kunufaika na hili na wao hawakujuwa wakaingia mkenge!
 
Back
Top Bottom