CHADEMA kutoa msimamo mzito leo; Ni baada ya rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya

Chadema sasa mnataka kutoa msimamo gani tena wakati juzi mmekutana na rais ikulu mkanywa chai pamoja mkampa mapendekezo yenu!
Duuh ulipotea mpaka ukauliiziwa vipi baba kwema lakini?
 
Hata Nape mmemponza kwa njia hii hii ya kushangilia komenti zake za kipuuzi, leo mmemkimbia hatuoni mkiongelea kwisha habari yake kaiacha Chadema, hata hili la katiba siku likimgeuka aliyesaini ambaye ni hero leo mtakimbia kwa sababu mko kwa ajili ya komenti ya siku husika mfurahishane hamkomenti huku mkifikiria kuna kesho kujibu.

Na bado utaongea yote mwaka huu, rais ndio kaishafanya kazi aliotumwa na wananachi wake, kasaini baada ya kunywa juice na keki na Chadema Ikulu
 
Nasubiri kwa hamu hilo tamko maana iliniuma sana kusikia rais kasaini
 
Huo ndio ukweli Chadema walikwenda kunywa chai ikulu..

Kwa nini sasa wanataka kutoa tamko la nini?

Kumbe hizo chai za ikulu ndio zinawaponza wabunge wa ccm na kuimba tarabu bungeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. CHADEMA ni people's power sio kidumu chama cha kunguni. Baba yenu alipiga makelele chadema fanyeni mazungumzo mazunguzo yamefanyika na amepuuza na sio ya chadema tu, wapo wengi wanaharakati, jukwaa la katiba nk. Sasa asubiri mvua inyeshee hapo Ikulu.
 
Chadema cc wananchi ndo tunawapa nguvu tunapowashabikia na kuwaunga mkono hata kwa mambo yasiyona maslahi, lakini wao kama wao kwenye uongozi hawana lolote usanii tuu, kama huamini embu fikiria au jiulize kila jambo lazima washtaki kwa wananchi wao uwakilishi wao uko vp? Wanafanya kazi gani au hoja zao hazina mashiko?, Hiki ni kipindi cha masika watuache tukalime kwanza tutawasaidia baadaye . .Porojo nyiiingi na siasa zao za kitoto,, watu wasio tii hata vyombo vya sheria fumbapu zao.
 
Cha msingi chadema tunawafuasi wengi na tuwaunganishe watanzania wengine tupiganie haki za watanzania kwa njia yoyote ile itakayofaa,ila nzuri zaidi nikufanya mandamano makubwa yasiyokuwa na kikomo,mana CCM hawataki majadiliano,they have killed our past and they continue to kill our future.
 
nyingi za comments katika hii thread zinaashiria jinsi watanzania tulivyo wajinga. Maongezi ya ushabiki na mzaha usiochagua mahala pa kufanyikia ni zao la kukosa elimu japo tumekaa madarasani siku nyingi na kukabidhiwa mikaratasi tukiwa tumevaa majoho, kumbe majuha.

Ni imani yangu kuwa CHADEMA walifanya jambo la busara kwenda kufanya ule mkutano. Katika kutafuta mapatano maongezi huishia kwenye kupeana ahadi za kutimiza maafikiano ya kikao na kila mtu kutawanyika. Sasa mtu mzima mwenye akili zako unawezaje kusema kuwa
Huo ndio ukweli Chadema walikwenda kunywa chai ikulu..

Kwa nini sasa wanataka kutoa tamko la nini?
hii ni dalili ya ubongo usiofikiri kwani sijui mwenzetu alitaraji nini zaidi ya maongezi na kusubiri.

Lets be reasonable comrades: CHADEMA hawakulazimika kumpiga makofi Rais ili kuudhihirishia umma kuwa wapo serious na hawajaenda kunywa chai. Iliwalazimu kuongea, kufikia muafaka na kutoa nafasi ya maafikiano kutekelezwa. Kwa kuwa sasa hayakutekelezwa, tamko la nini kifuatie ndio linakuja. Mimi sidhani kama kulikuwa na lingine la kufanya.

Kuna mwingine tena hapa naye kasema 'ooh walitoka bung....sasa wana...'. Ndugu yangu haya aliyoyafanya rais ya kusikiliza na kuweka kapuni ndio hayo hayo yangefanyika bungeni. Wapinzani wangesikilizwa na kubezwa na wabunge wa CCM A na B kwa pamoja na baadae kile walichokiandaa CCM kama chama kingepita. Kwa ungetumia akili kidogo tu ungejua kuwa serikali, rais na CCM hawana nia ya dhati ya kufanya makubaliano na mwananchi zaidi ya kufanya kile wanachoona kina maslahi kwao.

Na la 3 ambalo ndio kubwa linanishangaza kuhusu Watanzania ni hili la 'kila mtu aende kwenye kazi yake'. Tumekuwa vigeugeu na mbayuwayu hasa. Hapo mwanzo upinzani uliitwa vyama vya msimu. "hivi si vyama vya wakati wa uchaguzi tu, uchaguzi ukipita na vyenyewe vinakufa mpk uchaguzi mwingine"=haya ndiyo yalikuwa malalamiko yetu. Sasa hivi tunao CHADEMA wanaofanya kazi ya siasa mwaka mzima, tayari tumebadili maongezi "ooh uchaguzi umepita sasa tuache malumbano tufanye kazi" Sasa swali ni hili: Ni akili kukazana kulima kupalilia na kuvuna halafu tukaweke mazao yetu kwenye ghala ambalo wote tunajua linatawaliwa na panya?

Kufanya kazi bila kutathmini wapi jasho lako linaenda ni UJUHA na ni akili za kitumwa. Kazi ndio tufanye, lkn pia tuangalie pato la kazi yetu linatumikaje. Uvivu wa kufikiri unafanya juhudi za mwili zisiwe na matunda na hapa mimi ndio huwafananisha watu na kuku. Ni kuku wa mayai ndiye hutaga yai leo, likaondolewa na kesho akataga lingine bila kujiuliza la jana limekwenda wapi. Hakuna wakati tunapaswa kuacha kufanya siasa, siasa ndio itoayo dira ya wapi tunakwenda.
 
Na bado utaongea yote mwaka huu, rais ndio kaishafanya kazi aliotumwa na wananachi wake, kasaini baada ya kunywa juice na keki na Chadema Ikulu
Your group is always the loser tuliwaambia mnaponza Nape mkabisha leo group lile lile linaendelea kumponza rais.
 
Hivi kuna mtu alitegemea kupata kitu kutoka kwa JK anayeshauriwa na Wasira, Lukuvi nk? CDM wamewatega mitego yao vizuri sana, subirini muone mambo yatakavyokuwa.
 
Chadema cc wananchi ndo tunawapa nguvu tunapowashabikia na kuwaunga mkono hata kwa mambo yasiyona maslahi, lakini wao kama wao kwenye uongozi hawana lolote usanii tuu, kama huamini embu fikiria au jiulize kila jambo lazima washtaki kwa wananchi wao uwakilishi wao uko vp? Wanafanya kazi gani au hoja zao hazina mashiko?, Hiki ni kipindi cha masika watuache tukalime kwanza tutawasaidia baadaye . .Porojo nyiiingi na siasa zao za kitoto,, watu wasio tii hata vyombo vya sheria fumbapu zao.

Wewe utaacha ushabiki wa kijinga lini,katiba ndiyo uhai wa mwanadamu katika dunia ya leo,Chadema ina nguvu ya uma,tunajua nyie ni vibaraka wa CCM mnaoiba pesa za wananchi,dawa yenu ipo jikoni,hamjifunzi kilichomtokea Gadaf.
 
Habari zenu wana JF;

Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo tarehe 30/11/2011 kinatarajia kutoa msimamo mzito baada ya Rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya.

M/kiti wa CDM Mbowe "Tulimuomba Rais Kikwete asisaini muswada huu mpaka makubaliano yetu yatekelezwe"

Kaimu Katibu mkuu wa CDM, Mnyika "Chama kitatoa msimamo mzito leo, tulimshauri Raisi Kikwete asisaini muswada huu mpaka kwanza tuliyokubaliana yatimizwe"

Wakuu mwenye taharifa zaidi atujuze.


Nawasilisha.



JK na CCM yake walipewa nafasi lakini wameipoteza -- mimi huwa si muumini mkubwa wa makubaliano bila shinikizo, anyway CDM mmefanya wajibu wenu kama chama cha wastaarabu kudai haki kwenye Meza, maadam jamaa kawazidi kete basi Wembe ni ule ule -- Nguvu ya Umma irudi barabarani aone kama ataufanyia kazi huo muswaada aliousaini. Police waagize mabomu, virungu tayari tayari kwa shughuli za mapambano na waajiri wenu yaani wananchi.

Tunaanza na wanaharakati Jmosi, Then CDM itafuata. - Katiba MPYA ni mali ya wananchi si mali ya CCM.
 
Mbele ya mashahidi 2 au 3 kila neno hudhibitika. Chadema wamedhibitishia rais kuwa msuwada uliyopitishwa na wabunge wake wa ccm+cuf..... Hauna ridhaa ya wananchi. Kwa misingi hiyo CDM haitakuwa na lawama kwa lolote litakalotokea. Ikiwa ni pamoja na umwagaji mkubwa wa damu za wenye nchi. Namwomba Mungu siku zote hilo lisitokee.
 
Hivi kuna mtu alitegemea kupata kitu kutoka kwa JK anayeshauriwa na Wasira, Lukuvi nk? CDM wamewatega mitego yao vizuri sana, subirini muone mambo yatakavyokuwa.
Chadema kuna vichwa kule CCM ilikuja na mbinu ya kuipaka CDM kuwa chama cha vurugu CDM wamewazunguka wameanza kwa mazungumzo.

Afterall CCM wanacheza mziki wa CDM it was planned even before the election 2010, Chadema wangejidai kutumia bunge kudai katiba mpya wasingefanikiwa kwa uchache wake wakaupasia mpira kwa wana CCM wenyewe sasa Chadema wamekuwa kama refa wanaangalia makosa na kukosoa wakiwa nje.
 
Hakuna ushauri ambao CDM huwa wanauchukua toka kwa wanachama wake...in other words CDM haina tofauti na Kikwete wa CCM!! kila kitu usanii.....ona sasa aibu hii!



Mkuu Waberayo me nadhani ungeweka hoja hapa ya ushauri wako kwa chadema kuliko kutoka povu kwa hasira! Je unatakaje? waungane na Cuf,tlp na ccm kupinga au waungane na jukwaa la katiba kuomboleza siku 9? Hebu tusubili hilo Tamko la cdm later then tujadili.


Mkuu ushauri ni simple and clear.....simamia maamuzi yenu! acheni kuyumbayumba

CDM isingerudi tea mjengoni, hakukuwa na haja ya kuonana na rais, mkionana na rais na kuchekeana seriousness inaungua

HAKUNA URAFIKI NA CCM MBONA HAMSIKII??? Mbowe aache unafiki

Kudos to SLAA katika hili, bifu bifu tu hakuna kucheka na wezi..

unanielewa sasa??
 
Paka ni baba yako na mama yako waliokuzaa kwa kufanya uzinzi kimakosa na ukaletwa wewe wenye akili matope wenywe kushabikia kila jambo,sijui mtaacha lini ukibaraka wa kuwa CCM.
kaka una-deep TIS - :eyebrows:
 
Mkuu ushauri ni simple and clear.....simamia maamuzi yenu! acheni kuyumbayumba

CDM isingerudi tea mjengoni, hakukuwa na haja ya kuonana na rais, mkionana na rais na kuchekeana seriousness inaungua

HAKUNA URAFIKI NA CCM MBONA HAMSIKII??? Mbowe aache unafiki

Kudos to SLAA katika hili, bifu bifu tu hakuna kucheka na wezi..

unanielewa sasa??
Kwa suala la Chadema na Mbowe msimamo wako unajulikana huna haja hata ya kukomenti mimi nikionaga ID yako tu basi najua utasema nini.
 
Mabadiliko ya kweli hayataletwa na wanasiasa na vyama vya siaa. Mfano Egypt, Tunisa, Libya, Yemen na Syria
 
Mkuu ushauri ni simple and clear.....simamia maamuzi yenu! acheni kuyumbayumba

CDM isingerudi tea mjengoni, hakukuwa na haja ya kuonana na rais, mkionana na rais na kuchekeana seriousness inaungua

HAKUNA URAFIKI NA CCM MBONA HAMSIKII??? Mbowe aache unafiki

Kudos to SLAA katika hili, bifu bifu tu hakuna kucheka na wezi..

unanielewa sasa??
nimekubali kwamba Mtanzania akikamatwa na kosa lolote Rwanda au Uganda, mapolice wakijua ni Mtanzania tu kamwe hutapewa muda wa kujitetea - Jiulize why?

Ni nyie hao hao mliotaka muafaka ufanyike badala ya maandamano kila kukicha, kama CDM wangetangaza maandamano nchi nzima mngeanza kusema chama cha waleta fujo, jazba, hawataki kukaa mezani na wenzao, ooohh wantoka toka bungeni tu bila kutoa sababu za msingi. Leo hii CDM kwa kutumia ukomavu wa kisiasa wameamua kumwoa RAIS wa Jamhuri ya muungano kwa mazungumzo ya Katiba na si kwa lolote lingine-- eti wamefanya kosa na wanajikomba. mengi mno yamesemwa kwenye move ya CDM huwezi kuamini hawa watanzania kweli au wengine.

Ku-deal na M-TZ ni shughuli pevu sana.. ndiyo maana hamna umeme na maji miaka 50 tangu mpate uhuru.
 
Back
Top Bottom