CHADEMA kutoa msimamo mzito leo; Ni baada ya rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
283
Habari zenu wana JF;

Chama cha Demokrasia na Maendeleo leo tarehe 30/11/2011 kinatarajia kutoa msimamo mzito baada ya Rais kusaini muswada wa upatikanaji wa katiba mpya.

M/kiti wa CDM Mbowe "Tulimuomba Rais Kikwete asisaini muswada huu mpaka makubaliano yetu yatekelezwe"

Kaimu Katibu mkuu wa CDM, Mnyika "Chama kitatoa msimamo mzito leo, tulimshauri Raisi Kikwete asisaini muswada huu mpaka kwanza tuliyokubaliana yatimizwe"

Wakuu mwenye taharifa zaidi atujuze.

Nawasilisha.

Msimamo gani nao hawa, walikuwa wanachekelea huku wakiweka signature sasa ndio wanataka kuleta stori. CDM kwisha kazi yake. Huyo ndio Kikwete kama mlikuwa hamumjui.
 
Chadema sasa mnataka kutoa msimamo gani tena wakati juzi mmekutana na rais ikulu mkanywa chai pamoja mkampa mapendekezo yenu!
 
Huo msimamo mlishindwa kuutoa mlipoenda ikulu mnataka muutoe leo. Hatutaki ngonjera zenu hapa za maandamano. Watu mmepewa heshima ya kuongea na Mkulu Ikulu mkaishia kukenua meno na kushangaa tausi wake tu. Mnataka mpewe nafasi gani zaidi ya hiyo?
 
CDM bana.... kwa vitisho tu hawajambo... mtu mzima hatishiwi nyauu sidhani kama wanalifahamu hili...
 
mIE NAONA KIZUNGUZUNGU TU

WATU WATOKE, WARUDI, WAKANYWE CHAI NA MTUHUMIWA, WARUDI WATOE TAMKO, TUINGIE MITAANI, TURUDI, TUFANYE MIHADHARA, TURUDI

Hii gharama ya uhuru kamili kubwa sana kwangu kisaikolojia
Umesahau kupigwa virungu
 
Hakuna ushauri ambao CDM huwa wanauchukua toka kwa wanachama wake...in other words CDM haina tofauti na Kikwete wa CCM!! kila kitu usanii.....ona sasa aibu hii!

swala la katiba lisiwe la chadema , CCM wanapata nguvu sana ya kuwadharau kwa sababu mko isolated!!!

kwa nini hamsikii paka nyie!!

hamna uamuzi wowote mgumu mtakaoweza wasaliti nyie...posho mnachukua kimya kimya.....traitors!!
 
Waende wakafanye kazi, kila mtu atawanyike ktk eneo lake la KAZI. Kwa ndg. wakulima msile mbegu na kuwasikiza Chademu, mvua za vuli zimeshaanza msije mkaja kutulilia njaa..ajizi nyumba ya dhiki..Politiki haziliwi.
 
Msimamo gani nao hawa, walikuwa wanachekelea huku wakiweka signature sasa ndio wanataka kuleta stori. CDM kwisha kazi yake. Huyo ndio Kikwete kama mlikuwa hamumjui.
Pole sana kwa kulewa ushabiki...laiti ungejua una support sheria iliyopitishwa na serikali ileile mnayoipinga mfumo wake kwenye 'vijiiwe' vyenu , usingeshabikia hiki kitu kama zuzu vile...!
 
mIE NAONA KIZUNGUZUNGU TU

WATU WATOKE, WARUDI, WAKANYWE CHAI NA MTUHUMIWA, WARUDI WATOE TAMKO, TUINGIE MITAANI, TURUDI, TUFANYE MIHADHARA, TURUDI

Hii gharama ya uhuru kamili kubwa sana kwangu kisaikolojia

Mkuu sio wewe tu...hata mie kizunguzungu

siamini kama CDM kweli waliamini JK atawasikiliza !!1 same JK we all know
 
Pole sana kwa kulewa ushabiki...laiti ungejua una support sheria iliyopitishwa na serikali ileile mnayoipinga mfumo wake kwenye 'vijiiwe' vyenu , usingeshabikia hiki kitu kama zuzu vile...!
Kikwete alisema yuko tayari kuwasikiliza wote hata nyie wa kijiweni.
 
Unajuwa angeenda Zitto mambo yangekuwa tofauti kabisa, hii ndio faida ya kupekleka walevi wakajadili jambo la muhimu kama Katiba.
 
After Chadema's apparent failure to dissuade JK from endorsing the controversial Constitution Bill, people's faith in the party's elite has eventually started to shrink. Everyone was made to believe that Chadema delegation was capable of preventing the Bill from being signed but the outcome was disappointing. That Chadema has failed to take an advantage of a rare Presidential meeting to convince him not approve the Bill means that its leaders do not have postulated abilities necessary for a political leader.
 
Hakuna ushauri ambao CDM huwa wanauchukua toka kwa wanachama wake...in other words CDM haina tofauti na Kikwete wa CCM!! kila kitu usanii.....ona sasa aibu hii!

swala la katiba lisiwe la chadema , CCM wanapata nguvu sana ya kuwadharau kwa sababu mko isolated!!!

kwa nini hamsikii paka nyie!!

hamna uamuzi wowote mgumu mtakaoweza wasaliti nyie...posho mnachukua kimya kimya.....traitors!!
You can say better than this hata ukitumia lugha ya ki staarabu utaeleweka.
 
quote_icon.png
By MTM

mIE NAONA KIZUNGUZUNGU TU

WATU WATOKE, WARUDI, WAKANYWE CHAI NA MTUHUMIWA, WARUDI WATOE TAMKO, TUINGIE MITAANI, TURUDI, TUFANYE MIHADHARA, TURUDI

Hii gharama ya uhuru kamili kubwa sana kwangu kisaikolojia
Mkuu shughuli yenyewe ndiyo kwanza inaanza, mbona kizunguzungu mapema?
 
Mimi nawapongeza CDM. Wamejaribu kufuata njia ya mazungumzo. Si ndio tunasisitiza kila siku? Watu wamalize njia zote za mazungumzo, ikishindikana kisago ndio njia pekee inayobaki. Kwa hiyo CDM hongereni sana. Mmedhihirisha hakuna Afrika katiba ya wananchi mpaka tuchinjane kwanza kama ilivyokuwa Rwanda na Kenya. Na hii itakuja tu, hata kama sote tulio hai leo tutakuwa tumekufa. Vizazi vyetu vijavyo watachapana tu ndio waheshimiane.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom