CHADEMA kutinga na kutikisa Mtwara; shughuli kuanzia Mjini Mtwara leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kutinga na kutikisa Mtwara; shughuli kuanzia Mjini Mtwara leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, May 28, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  Wakuu;

  Leo tunatinga Mjini Mtwara. Tumelala Mjini Lindi. Advance team katika operesheni hii ya Kusini inasema mipango yote inakwenda vyema kabisa. Hamasa ni kubwa. Wenyeji wanatusubiri wageni. Mgeni njoo, mwneyeji apone. Katika hili wenyeji watapona kwa kupata elimu ya siasa, hasa juu ya mchakato wa katiba mpya.

  Wenyeji watapona kwa oganaizesheni ya chama kujengwa kuanzia ngazi ya vijijini mpaka mijini. Wenyeji watapona kwa kuendelea kupata hoja na namna ya kudai uwajibikaji wa serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Watapata hoja za namna ambavyo serikali inapaswa kuwajibika kwa kushughulikia vyanzo/viini vya matatizo yanayoikabili jamii kwa sasa, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Badala ya kushughulikia matokeo ya matatizo kama ambavyo serikali ya CCM inafanya sasa.

  Baada ya Mjini Mtwara leo, kesho timu itagawanyika katika makundi kadhaa kwa ajili ya 'kuvamia' kata zote za Mtwara Vijijini. Keshokutwa itakuwa zamu ya Tandahimba. Kazi ni moja tu. Kusambaza chama kwa kasi mithili ya moto wa petroli. Amesema Kamanda Mbowe juzi pale Chadema Square. Nitawapatia ratiba ya maeneo mengine kadri muda unavyokwenda.

  Unaweza kuona kuna watu wameanza kuweweseka hapa. Tumesikia wengine tangu shughuli pevu ya juzi pale Chadema Square hawajapata usingizi sawasawa. Mambo kichwani hayawaendei sawasawa. Wengine wameanza kuelewa kuwa inaweza isifike na si lazima mwaka 2015. Wengi wao wameanza kuiona 2015 inakaribia kwa kasi sana. The exit is very obvious!

  Kiwewe cha M4C, Vua Gamba na Vaa Gwanda, Watanzania wanyonge kuchangia vuguvugu bila uoga (kama ilivyokuwa wakati wa kupigania uhuru), safari yetu ya Kusini na mengine mengi yanawafanya waanze kuandika uongo hapa. Wanahangaika kweli! Jogoo, awike asiwike, kucha kutakucha. Wanajua hilo! Wajiandae.

  Kama ilivyo ada, Operesheni hii ya Kusini pia itafanywa na timu ya watu makini. Imekuwa hivyo katika operesheni zote za Chadema. Kamanda wa Anga, Freeman Mbowe anaongoza jahazi, Kamanda wa Ardhi, Dkt. Willibrod Slaa yuko tayari. Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Said Issa Mohamed yuko kamili.

  Wabunge kadhaa wametangulia field, John John Mnyika, Tundu Lissu, Ezekiah Wenje. Wengine wako njiani muda si mrefu kuuungana na makamanda waliotangulia. Timu ina mchanganyiko wa vijana na wazee, wazoefu na wapya. Wenyeji watapewa nafasi ya kufanya kazi zaidi ili wapate uwezo wa kusonga mbele wageni wakiondoka.

  Operation Commander kwa shughuli hii ya Kusini ni John Heche, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA). Kiuhalisia, kama ilivyo jeshini timu nzima iko chini ya Heche. Viongozi wakuu watalazimika kuingilia pale panapohitajika sana na katika masuala mengine machache ambayo ni wazi yanahitaji uongozi wa juu kusimamia, kuelekeza, kuagiza na kuamuru. Kuongoza!

  Walioko Mtwara Mjini karibuni sana. Wengine walioko mbali tutawajuza kila kinachotokea. Punde tunaondoka Lindi, kwenda Mtwara. Baada ya Mkoa wa Mtwara, shughuli itahamia Mkoa wa Lindi. Ratiba mtaipata hapa hapa. Asanteni.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  safi sana wakuu, kazi njema
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Mkuu Makene hatuna wasiwasi na nyie, wenye wasiwasi ni hawa wanao hama kutoka kuwa chama cha kisiasa kwenda kuwa chama cha kibiashara. Wakumbatieni wakulima wenzetu wa korosho wamedhulumiwa na kupuuzwa vya kutosha sasa ni wakati wa kujiunga na chama makini kinacho tetea wanyonge.

  Mkumbuke kutuwekea updates za matukio tufuatilie kwa ukaribu yale yanayojiri.
  Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke.
   
 4. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Safari njema wa kuu.
   
 5. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kila la heri Makamanda, Mungu yu pamoja nanyi kwani mlifanyalo ni jema kwa wana wa nchi aliyowapa Mungu.
   
 6. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kazi nzuri makamanda all the best.mi nipo hapa saut mtwara.kwa upande wa wanachuo hamasa ni kubwa sana na karibu kila kona ya mitaa tunayoishi habari za chadema zimeenea bila shaka ujio wenu unafahamika vyema kwa watu wa mtwara.karibuni sana tutakutana kwenye mkutano bdae ngoja nipige lecture mbili tatu hvi.peopleeez...!
   
 7. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja nanyi tunawaombea uzima na afya tele
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Duh, mkuu bandiko umeliweka mithili ya ngojera halichoshi kusoma! lugha laini na nyepesi kusoma. Ahsanteni makamanda, Kila la kheri wakuu!!
   
 9. m

  mob JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  nawatakia safari njema.WAO WANA FEDHA CHADEMA INA MUNGU
   
 10. Q

  Qixima mQiqa Senior Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi njema ya ukombozi kusini
   
 11. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona makamanda 99.99% ni wa dini moja? hao Waislamu wa huko watawaelewa kweli?
   
 12. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,995
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  :israel:M4C iwafikie wote hasa wale wa vijijini.
   
 13. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Karibuni Saaaaaana ILULU
   
 14. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hii hoja ya dini za makamanda imekutokezea tu ama huwa unaiwaza na kuiota na kuifanyia kazi?kwa mwelekeo huu wewe ni aina ya gamba
   
 15. m

  muislamsafi Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila la heri
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu, unajuaje kuwa wote ni wa dini moja? Au umeangalia majina. Jina sio dini, bali dini ni imani. Natumaini makamanda hao wana imani inayowaunganisha, ya kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania, bila kujali, zaidi ya yote, dini.
   
 17. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mbona viti maalum mnagawana kaskazini, yaani ubunge mgawane nyie sisi tule vumbi. Haiwezekani njooni tuwashangae tu.
   
 18. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  2po pamoko.
   
 19. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana makamanda na sisi hatutawaangusha Watanzania wa leo siyo wale wa wazamani ambao ulikuwa ukiingia sebuleni kwao unakuta vitambaa vya makochi ni vya kijani akiwemo baba yangu hahahahaaaa.
   
 20. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Hapo mkisambaa nchi nzima, nadhani ndipo itakuwa muda mwafaka wa mimi kuanza kuwakubali. Safi sana makamanda.
   
Loading...