CHADEMA kuteketezwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA kuteketezwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kigugumizi, Nov 4, 2009.

 1. k

  kigugumizi Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ipo mikakati mingi sana inayofanywa na Serikali ya CCM, Usalama wa Taifa, pamoja na jeshi la ulinzi, ili kuweza kudhoofisha nguvu ya chadema Tanzania.

  Huku CCM ikitumia mfumo wa Usalama wa Taifa kuweza kuwasaidia katika mambo mengi ya kiusalama; Sasa mipango hiyo imeweza kusukwa kwa kutumia mfumo wa kiutendaji wa Usalama wa Taifa:
  1. Ajenda ya kukichafua chadema.
  Kwanza, Baada ya Ikulu, na Usalama wa Taifa kuanza mikakati ya kuwachafua wapiganaji wa vita vya ufisadi Tanzania, ili kupoteza mwonekano na imani ya wananchi kuhusu vita vya ufisadi, na wapiganaji wenyewe, kwa kuonekana kuwa wao ni mafisadi kwa kuwalenga akina Mwakyembe na wenzao, mkakati huo uliokabidhiwa kwa Takukuru umeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana. Ndiyo maana Hosea anajeuri ya kuwagombeza wabunge kuwa hawawezi kumfanya lolote. Lengo pia, ni kumtoa Lowassa kwenye truck ya Richmond.

  Pili, Baada ya hao anayefatia ni kuondoa imani ya wananchi kwa chadema hasa kwa Dr. Wilbrod Slaa. Ajenda ya Ufisadi wa fedha za Yatima, Sadaka za kanisa la RC wakati akiwa ni mtumishi umeshakamilishwa pamoja na vielelezo vipo, wakati si mrefu Maaskofu kadhaa au watu senior watajitokeza kutoa kashfa hizo kwa Dr. Slaa pamoja na mfululizo wa Front page kwenye magazeti makubwa hapa Tanzania ili kuifanya kuwa leading story na debate kwenye vyombo vya habari Tanzania. Tayari wahariri kadhaa wameshataarifiwa.

  Tatu, Wakati Zitto akiwa anahusishwa na uswahiba na JK, Rostam na watu senior Serikalini + CCM, itaoneshwa kuwa chadema ni CCM B kama vile ambavyo madai ya CUF yanavyosema. Vyama vingine vya upinzani kama TLP, NCCR-Mageuzi watajitokeza mstari wa mbele kutoa comments kuwa chadema ni CCM B. Lengo ni kuondoa imani kwa wananchi dhidi ya CHADEMA.

  Nne, Usalama wa Taifa wakishirkiana na Mtanzania, Hoja na Majira walishindwa kuilabble chadema kama Chama cha Kikabila kwa matarijio yao makubwa sana.

  Tano, Mpango wa kukihusisha na fedha za SMS Fundraising kama ufisadi wa Mbowe, umelenga zaidi kuondoa imani ya wananchi kukichangia fedha Chama hicho.
  2. Zitto Kuhamia CCM.
  Mosi, usalama wa Taifa, CCM wanaamini kuwa Zito atahamia CCM kabla ya Uchaguzi. Zito akiwa ahamini utendaji wa mbowe na Dr. Slaa anajua kuwa Chama kinaweza kufa wakati wowote.

  Pili, uswahiba wa JK na Zito ulianzia kwenye kamati ya madini. Katika marekebisho ya Wizara, Zito alipewa Uwaziri na JK, kabla ya JK kufanya marekebisho ya ghafla akiwa Dodoma baada ya kupata upinzani ndani ya CCM.

  Tatu, Zito ameahidiwa Uwaziri wa Nishati na Madini kwenye awamu ijayo. Conditon ni kuingia CCM. Ili kuwa mzuri katika hiyo field, ameanza masomo yake nchini Ujerumani akichukua masuala ya sheria za mikataba ya madini kwa mwaka mmoja.

  Nne, ameanza kuwa kunolewa katika siasa za kimataifa ili kuandaliwa vyema. Kukaa kwake Bungeni ni nadra sana, au kwenye shughuli za Chama chake. Lengo ni kupunguza uwajibikaji wake katika Bunge na Chama.

  Tano, Sina hakika kama Zito yupo tayari kuhamia CCM kama Usalama unavyoamini, ila akicheza mpira vizuri atapewa Uwaziri wa Nishati na Madini akiwa bado chadema mwaka 2011 na JK.

  Taarifa za ndani za chadema zinasema kuwa Mbowe amehitisha kikao kisicho rasmi Dodoma, wiki hii huku Zito ameondoka mapema kwenda nje ya nchi pasipo taarifa kwa viongozi waandamizi wa Chama hicho. Hali bado haijawa shwari ndani ya Chama hicho, athari za Uchaguzi bado zipo.

  sasa tusubiri hali itakuwaje.

  • Nasubiri nyaraka feki dhidi ya Dr. Slaa ambazo ameandaliwa na Usalama wa Taifa, kisha zitakuwa kwenye JF hivi karibuni.
   
 2. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,243
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huo mkakati kwa kweli unaonyesha kuna dalili za ukweli hasa huo wa zitto,

  kale kajamaa sometimes sikaelewi kabisa yani kanarukaruka kama ndama,

  ndo mana nahisi hii makala itakua na ukweli.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Chadema mbona kimeshakufa...
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Lini hiyo Kibs?

  Jamani mbOna huku naniliu tuko strong sana na kila siku yanafunguliwa matawi?

  Au naongea na mamluki?

  Mmetumwa?

  Nanani?

  Mnalipwa nini nyie?
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hata mimi ningehamia CCM ikiwa nitapewa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu ktk uongozi kuliko kuganda na chama kisichokuwa na mwelekeo...Upuuzi mtupu!
   
 6. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mhhhhhh! mbona hivi karibuni thread zinamjadili Mh.Zito kwa kasi, kunani?

  Wanasema penye moshi kuna moto ingawa wakati fulani baridi ikiwa kali basi unaona kitu kama moshi kinafuka yawezekana nao huwa ni moto wa aina fulani.
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 673
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Zitto akiamia CCM atakuwa ameyarudia matapishi yake mwenyewe kwani amekuwa msitari wa mbele kuikosoa serikali ya CCM. Ila sishangai sana kwani watuwengi wanauwezo wa kupiga kelele na kuwa na msimao mkali,lakina akipewa chochote,basi kasi inaisha. Na hii ndo mbinu CCm inayoitumia kuwafifisha wanasiasa machachari.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,441
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hata Mandela alikuja ungana na Kaburu.... Ujinga ulipo sasa hivihauna nafasi kwa wananchi...LOLOTE na LIWE kwangunpoa tu, siasa za Bongo nimechoka nazo.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Tokea walipomaliza Mkutano Mkuu wao..
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 680
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  Huu niuzushi mtupu wa kutia hofu watu. Tuambie source of your information. Manake thread yako imejaa mambo kufikirika na kihisia zaidi. hata chedema kikifa kuna siku chama kimojawapo kitaiondoa ccm madarakani kwani tanzania itadumu daima na ccm haiwezi kudumu daima. is a matter of time and level of literacy. ninaimani shule za kata kwa miaka kama 15 ijayo zitaleta mapinduzi ya kufikiria watu. na hivyo hawatakubali kuchakua pilau na kutoa kura for five years.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Uzushi mtupu hao CUF walidai lini kuwa Chadema ni CCM B...?
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  ^^ Nyie CUF kaburi lenu linaandaliwa vema kule PBA
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  wauwaji wakubwa nyie, mara hii tutakufa sote, kujiliputa tu kwenda mbele...watahadharishe jamaa zako, Mpemba mmoja akiuliwa hakikisheni tutahesabu askari miamoja...
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Habari hii ni nzito . Mimi sitaki kusema sana . Kuna hili la Slaa najua watapiga chini hawataweza na watadhirika , Kanisa katoliki hawawezi kuingia ujinga wa kusema mambo ya Slaa . Zitto kuingia CCM hili ni gumu sana sana na siamini lakini ..............................

  Mengine nafungua macho wazi zaidi nijionee na masikio yamesha tegwa
   
 15. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 355
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Habari nzito hii, ebwana weee, yani kupinga unashindwa kukubari unashindwa,kila kitu kinawezekana.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Kwenye siasa lolote linaweza kutokea, hasa wakati huu ambao kauli za Zitto Kabwe zimekuwa hazieleweki hasa pale baada ya kumaliza ufuatiliaji wa mikataba ya madini! Amebadilika sana baada ya hapo! Anyway, whatever the case, kwenye siasa kuna kupanda na kushuka, remember Augustine Lyatonga Mrema? What happened to this man politically? Sio kafulia tu bali kaanika!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kheeee heeeh! Na bado...
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,674
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
 19. M

  Masatu JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,286
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Chadema ni debe tupu kama matokeo ya chaguzi za serikali za mitaa na vitongoji yanavyo onyesha. Dar wameambulia kito kimoja tu katika zaidi ya viti 130
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 133
  Kimtazamo tu Zitto ana aim high katika siasa lakini si dhani ni kwa namna hiyo hawa "usalama wa taifa" walivyoimwaga hapa, na kwa Dr. Slaa it will take more than politically rumour mongering atmosphere to finish this strong and committed guy.
  Na bado mtalipana posho mara kumi kumi kwa kazi moja ikibidi watanzania wakae gizani na hata wafe njaa, Kidumu chama cha Mafisadi...Kibs, unapotea nshakuona!
   
Loading...