Chadema kutamu;msafiri mtlemwa anyanganywa gari alilopewa na zito.halima mdee amgeuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kutamu;msafiri mtlemwa anyanganywa gari alilopewa na zito.halima mdee amgeuka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 13, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Famili ya zito imekuwa na kikao cha dhararua na kuazimia mambo yafuatayo

  Kikao hicho kilijadili misaada ya magari ambayo Zitto ametoa kwa baadhi ya vijana wanasiasa ndani ya CHADEMA kwa ajili ya kuwasaidia washinde katika majimbo yao ya uchaguzi. Mmoja kati ya watu hao anatajwa kuwa ni Msafiri Mtemelwa ambaye wakati wa uchaguzi wa ndani ya CHADEMA alikuwa Kampeni Meneja wa Zitto Kabwe kwenye kugombea nafasi ya uenyekiti na hata katika kupanga safu za viongozi wa ngazi zingine ndani ya CHADEMA. Familia ilielezwa kwamba hivi karibuni Msafiri alionekana akiongea na Katibu Mkuu Dr Slaa ofisini. Familia ikaelezwa kuwa alipigiwa simu hivi karibuni na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. Kutokana na mambo hayo, kikao hicho kilianza kumtilia mashaka kuwa amemgeuka Zitto Kabwe.

  Mtoa habari wetu anafafanua kuwa David Kafulila alikieleza kikao kuwa Msafiri Mtemelwa alichangia uteuzi wake kama Afisa utenguliwe kwa kuwa alikuwa mjumbe wa Kikao cha Sekretariati kilichokaa chini ya uenyekiti wa Dr Slaa lakini hakumtetea. Kafulila aliendelea zaidi kukieleza kikao kuwa badala ya kupingana na wajumbe wengine wa sekretariati ili kumnusuru, Msafiri alitoa hoja kwamba atolewe nje ya kikao baada ya kujieleza kwa masaa manne ili maamuzi yaweze kufikiwa. Hivyo, wanafamilia walichukua uamuzi wa kumnyang'anya gari aliyopewa na Zitto Kabwe aina ya Prado. Uamuzi huu umeshatekelezwa kwa Msafiri Mtemelwa kunyang'anywa gari hiyo.

  Mwanafamilia huyo anaendelea kudodosa kuwa maadui wa Zitto wanatajwa kuwa ni Freeman Mbowe, Dr Slaa na wakurugenzi wote wa makao makuu ya CHADEMA isipokuwa Msafiri Mtemelwa. Katika orodha hiyo anatajwa pia mfanyabiashara mmoja na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari. Pia wabunge wote wa CHADEMA isipokuwa wawili. Gazeti la jana la Rai limeeleza pia katika kundi la wabunge anayeongoza kwa uadui na Zitto ni Halima Mdee ambaye anatajwa kuwa amewasilisha nyaraka ya tuhumu 22 dhidi ya Zitto Kabwe kwa chama hicho ikiwemo tuhuma zinazohusiana na masuala ya kampuni ya Dowans. Kutajwa kwa jina la Halima Mdee kumethibitisha maelezo ambayo Msaidizi wa Karibu wa Zitto Kabwe, Omar Ilyas aliwahi kuyatoa katika Mtandao wa Jamii Forums, akieleza kwamba yupo mbunge mmoja kijana ambaye alikuwa karibu na Zitto ambaye amemgeuka na kumtuhumu kwa mambo mbalimbali. Omar amekuwa akihusisha mbunge huyo, na jina la Mwafrika katika mtandao huo.
   
 2. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Duh! kweli wenzio wakinyolewa wewe tia maji.

   
 3. tunalazimika

  tunalazimika JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2013
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  habar ya mwaka 2009 hiyo mzee
   
 4. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2013
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Omfgwtf?.
   
 5. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2013
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Wafanye yote ila Zito ni gunia la misumali
   
 6. M

  Manyerere Jackton Verified User

  #6
  Nov 27, 2013
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 2,357
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Tangu mvurugano ndani ya Chadema ulipoanza, sipati hata raha ya kula. Nchi hii bila mageuzi haitafika popote. Chadema ilijipambanua kama chama ambacho kingeweza kuiweka kando CCM, lakini kwa vurugu hizi sidhani kama hii ndoto itawezekana tena. Ikumbukwe kuwa kazi hii iliwashinda NCCR-Mageuzi, na sasa Chadema. Pengine tusubiri kweli CCM yenyewe ipasuke ili tupate upinzani wa kweli. Inauma sana kuona hali hii. Wote mnaohusika na vita hii iacheni mara moja ili tufaidi matunda ya mageuzi katika Taifa letu.
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Isome vizuri halafu tafakari inahusika mwaka huu 2013 hii.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Huu ndio UKWELI MCHUNGU, zaidi ya hapo walio kuwepo WAENDELE KUHAMASISHA MAGEUZI MPAKA HAPO LIKITOKEA HILO.
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wategemea unachokiita wapinzani wa kweli watoke ccm hii? Mie najilia kwa raha zangu maana najua makapi yanakitoa kubaki nafaka halisi!
   
 10. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2013
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm........... J k Nyerere.
   
 11. T

  Torch JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 11, 2013
  Messages: 536
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kaka Manyerere Jackton maneno yako mazito sana. Nami nikifikiria kwa kina naumia sana,
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,445
  Likes Received: 19,811
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo sasa hivi jamaa anachapa lapa?
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2013
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Tambueni huu ni uasi ndani ya chama kuna vijitu vinatumiwa kutaka madaraka ndani ya chama ni sawa na kuanzisha mkakati wa kumpindua mwenyekiti wa maccm yupo madarakani watu waanze mpango wa kumwondoa.
   
 14. M

  MahinaVeterani JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2013
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 714
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nikosolewe kama nitakosea, kwenye red, bold na underline hapo, sio kuwa Mwl. Nyerere alisema hayo? Ukweli ndiyo maana mimi sishobokei sana masuala ya Vyama vya Upinzani vilivyopo - wote ni Makanjanja, ni kama NGOs za watu binafsi tu! Chama cha Kisiasa cha kuitoa CCM Madarakani bado kupatikana!
   
 15. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,804
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  kumbe wanaume walifadhiliwa tu.....!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...