Chadema kutaka maelezo toka wabunge 10 ambao hawakuja Bungeni wakati wa "walkout'

Status
Not open for further replies.
Nadhani hakuna mjadala hapa kuhusu Zitto, kilichopo afukuzwe tu kwenye chama maana yeye ndie chanzo cha migogoro mingi ndani ya chama...

Tunajua plani yake yote hivyo hamna sababu ya kumkawiza huyu mlasiti.
 
kosa la mwaka, chadema kumuondoa naibu kambi ya upinzani ZItto. sisi watz tutahoji kulikoni?tutapapasa kunanini. na mwishowe tutao kauli sio bure, na mwishowe ni pigo kwa Chadema

Sidhani kama zito anazo sifa ambazo wengi mnampa. Kwa kipindi chake cha abunge alibahatika kuongelea suala la Buzwagi akawa kama kalamba dume. Ni sawa na Ana Kilango alivyobahatisha kusoma na kuiongelea ripoti ya richmond na baada ya hapo akabakia anajisifia tu. Ukiacha suala la Buzwagi ni kipi Zito amekifanya cha maana?

Zito alikuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu ya mashirika ya umma na kwa kipindi hicho ndo tulishuhudia mashirika ya umma (TTCL, NIC, TANESCO, ATC, TRC (Usafiri pekee wa kwao), nk) yakizikwa kama sio kuwa mahututi bila ya kamati yake kuongea lolote. Alizidiwa hata na mwana CCM (Shelukindo).

Hana lolote ila anapenda misifa tu. Kwenye chama tofauti za mawazo lazima ziwepo lakini kunapokuwa na uamuzi wa pamoja, ni lazima mtekeleze au la ujiuzulu.

Pia uamuzi ukishatoka, msemaji ni mmoja. Kwa nini zito akatangaze maamuzi wakati msemaji ni mmoja? Kitendo cha zito kutangaza kuwa haungi mkono ni cha kukihujumu chama na kimedhoofisha jitihada za CHADEMA kudai tume huru kwani tayari CCM wameona kuwa msimamo wa CHADEMA si wa pamoja. Afadhali asingehudhuria na akakaa kimya.

Aondoke CHADEMA kwani kuna watu maarufu kuliko yeye waliondoka upinzani na bado upinzani unaendelea.
 
Duh, na amakweli Zitto ametupa ujiko tuliomuita Arrogant na tukasema hafai kuwa KUB
Zitto ananifanya nitembee kifua mbele maana nilimpinga kwa nguvu zote alipotangaza nia ya kugombea ukuu wa kambi ya Upinzani
Kweli Zitto ni kirusi cha kuogopwa
 
Imeandikwa; Ukiona mkono wako unakufanya usifike peponi, Ukate. Chadema inataka kwenda peponi, kwa nini walee hii kansa????? njua wakimtema sisiem itaokota makombo, lakini hatakuwa na platform!!!! HE FELT SHAME TO WALK AWAY FROM JUA KALI (JK), NOW IS TIME FOR CDM TO WALK AWAY FROM HIM.
 
siku za nyuma nili hofu Zito anaweza kusambaratidha kambi ila mda unavyo zidi wa Tz wanazidi kugundua usanii na ukibaraka wake ,Chadema wasipo mkaripia hadharani kama yeye alivyo msifu bwana yake hadharani ,Chadema wajiandae kukaripiwa na wananchi , Zito ni nani abomolewe kabla haja bomoa chama chetu, hana shukurani yeye ni kama mbwa
 
Reyes,
Siasa unaianza kwa style mbaya.
Kwanini unadhani Zitto ni kirusi?
Hawa wengine usiwaige, they have nothing to loose.
Zitto ni mtu peculiar, ndio maana mawazo mepesi yanapata shida kumuelewa.
 
Nadhani hakuna mjadala hapa kuhusu Zitto, kilichopo afukuzwe tu kwenye chama maana yeye ndie chanzo cha migogoro mingi ndani ya chama...

Tunajua plani yake yote hivyo hamna sababu ya kumkawiza huyu mlasiti.

Chama hakiendeshwi kwa utashi wa watu binafsi, bali huondeshwa na katiba.
Kama Zitto mkosefu, basi katiba na kanuni zitumike kumpa adhabu. Hizi danadana za maneno hazijengi.
Hivi mnadhani CCM hawaadhibiani? wenzenu wanajua nani aseme nini na wapi.
 
siku za nyuma nili hofu Zito anaweza kusambaratidha kambi ila mda unavyo zidi wa Tz wanazidi kugundua usanii na ukibaraka wake ,Chadema wasipo mkaripia hadharani kama yeye alivyo msifu bwana yake hadharani ,Chadema wajiandae kukaripiwa na wananchi , Zito ni nani abomolewe kabla haja bomoa chama chetu, hana shukurani yeye ni kama mbwa

Gaza, tumia vifungu husika. Taja kifungu cha sheria au kanuni halafu eleza Zitto jinsi alivyokivunja.
 
Reyes,
Siasa unaianza kwa style mbaya.
Kwanini unadhani Zitto ni kirusi?
Hawa wengine usiwaige, they have nothing to loose.
Zitto ni mtu peculiar, ndio maana mawazo mepesi yanapata shida kumuelewa.

Tuna kutambua hivyo utupi taabu hata kidogo, hivi umekwenda kujibu maswali uliyoulizwa na Dr.Slaa?
 
Imeandikwa; Ukiona mkono wako unakufanya usifike peponi, Ukate. Chadema inataka kwenda peponi, kwa nini walee hii kansa????? njua wakimtema sisiem itaokota makombo, lakini hatakuwa na platform!!!! HE FELT SHAME TO WALK AWAY FROM JUA KALI (JK), NOW IS TIME FOR CDM TO WALK AWAY FROM HIM.

Wewe unadhani Ikulu ni peponi! Ndio maana umekubali kujidhalilisha kwa ajili ya Chadema. Kwanza Ikulu siyo peponi, pili Chadema kwa chuki mnazozidhihirisha hamuwezi kuingia Ikulu. Ni lazima mjifanyie marekebisho makubwa kama alivyoshauri Rev. Kishoka: Chadema MUST refom and restructure.
 
Excellent, Zitto sasa Kabweka, halafu huyu ana sifa gani zaidi ile ya Buzwagi ndio kapata kasifa kapata kichwa hilo, ana akili ndogo bado huyu, atoke haraka CHADEMA mm nisimkute
anajua nini? Dr Slaa kamfundisha even how to answer & asking questions bungeni,

Nyinyi na huyo Dr Slaa wenu tena! Ni sawa na yule kipofu aliyepewa nuru kwa dakika chache na mbele yake alikuwepo punda, basi tena kila kitu kikawa ni 'kizuri kama punda?'

Huyo Zitto afundishwe na Dr. Slaa kwani yeye mwenyewe hakusoma?

Na kwa nini munamhukumu yeye wakati wako wengine kama akina Ndesamburo na Shibuda hawakuhudhuria bungeni lakini haijawa issue, issue ni Zitto tu!
 
Zito ni kansa ikiachwa bila kushughulikiwa itasambaa mguu mzima na hatima yake ni kuukata wote. Aondoke aende akajumuike na mafisadi. Inawezekana alichokuwa anatafuta amekipata tayari.
 
kosa la mwaka, chadema kumuondoa naibu kambi ya upinzani ZItto. sisi watz tutahoji kulikoni?tutapapasa kunanini. na mwishowe tutao kauli sio bure, na mwishowe ni pigo kwa Chadema

Ni kosa la mwaka kumuingiza MS Chadema....... bora aendelee kuwa mafunzoni westbank kwa niaba ya tawi la HAMAS
 
Maswali ya Dr. Slaa majibu yake anayajua, so sioni sababu ya kuhangaika nayo.

Kama umeshindwa kujibu yale maswali ya Dr.Slaa, sasa ndio najua wewe ni nani unayejifanya kujua mambo ya ndani ya CDM. Nakupa pole sana maana umekuja wakati mbaya sana na huwezi kufanikiwa bali utaishia kupata aibu ya mwaka.
 
Asante kwa ushauri.
 
Hapa wanazungumziw wabunge 10. Vipi iwe Zito peke yake? Je hao wengine wafukuzwe pia au hatua gani nyingine ichukuliwe?Je ni nini madahara ya kufanya hivyo? Busara ni nini?

Je Zito ameleta madhara na mazuri mangapi kwa CDM mpaka sasa? Ukimpima anastahili nini?

Mimi binafsi ningependa Zito awajibishwe kwa sababu yeye ndiye aliyewachochea wenzake kutokuhudhuria. Hii yeye mwenyewe alisema. Yeye kama kiongozi mwandamizi hakustahili kuwashawishi wenzake, tena baada ya hapo akaelezea umma, akijua kuwa alifanya kosa ambalo adhabu yake aliijua nikufukuzwa na akawaomba wapambe wake wajitayarishe kumpokea. Zito hastahili kupewa nafasi nyingine kwani nionavyo keshapewa kabla na ameonywa mara nyingi sana. Ni mwiko kukaa na mamluki, ni hatari, na hasa wa calibre ya Zito, ana madhara makubwa mno nafuu kukosa nafasi ya kuunda serikali kivuli.

Ningetoa maelezo mengi lakini naona mengi yamesemwa na nitatumia nafasi kubwa bure
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom