Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,712
- 1,906
Kwa hiyo tunasherehekea kudidimia kwa uchumi nini??????????Hii inakupa picha ya wapi tunaenda
Kwa hiyo tunasherehekea kudidimia kwa uchumi nini??????????Hii inakupa picha ya wapi tunaenda
Nchi haiendeshwi kwa kusubiri chenji kwa hiyo mnasubiri kosa lingine ili mpate chenji ya kujenga zahanati? hizo sherehe sherehekeni nyie na watoto wenu sisi ni job kama kawa.
Nawapongeza sana makamanda kwa kususia hawataki kuwa sehemu ya unafiki kwa sababu hata maana ya sherehe yenyewe inapotoshwa imekuwa ya kisiasa si ya kitaifa tena, kama leo tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ikifika mwaka 2014 itafikisha miaka mingapi 53?
Waungana katika pitapita zangu nimegundua wana CDM hawafurahi TZ kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dalili zimejoinyesha;-
1. Viongozi wao katika ngazi zote kutoshiriki vikao vya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru
2. Viongozi wao kushindwa kushiriki kuukimbiza mwenge ulipofika katika maeneo yao; mfano Ubungo (mhe.Mnyika) na Kawe (mhe. Mdee ).
3. Wabunge wao wameshindwa kushiriki katika vikao vya maandalizi ya miak 50 ya uhuru pasipo kutoa udhuru.
Watanzania inabidi tutumia akili ya mbaimbawi tuwahukumu CDM katika masanduku ya kura kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2012 na tuwape kichapo kikubwa uchaguzi mkuu 2015. Hawa wamekosa uzalendo, wamebaki kushabikia sera za Mfadhili wao David Cameroon.
Hii ni fursa pekee kwa watz kujiuliza, kutafakari pale tulipojikwa na kupata mkakati wa kitaifa, TUZIDI kusonga mbele.
Mwaka 1961, graduate walikuwa 12, leo wapo mitaani hawana idadi wengine wanatumika pasipo kujitambua kushiriki maandamano ya CDM; tuwe waungwana tujitambue maendeleo yamepatikana.
Leo watoka Mwanza hadi DSM siku moja.
UDOM ni ishara ya maendeleo katika elimu
Powertillers kwa wakulima walioingia katika KILIMO KWANZA
Unahoja nzito lakini mjumbe jaribu kufupisha unakumbuka enzi zile za kuandikiana barua na kutuma kwa postaKatika hili swala la Mwenge na Maadhimisho ya miaka 50 ya UHuru wa Tanganyika kusema kweli mimi sintakubaliana na Chadema na kwa sababu zangu maana mimi ni Mhafidhina na Utaifa wangu unatangulia kwanza hata kama kesho Afrika itaungana na kuwa nchi moja.
Tafisri ya neno UHURU itabakl palepale kama siku wananchi wa nchi fulani wamepoata UHURU wao, ikiwa na maana hoja ni WATU waliokuwa huru ktk mipaka ya NCHI hiyo. Na UHURU huu unaweza weka mipaka ama kupunguza mipaka lakini kitu muhimu ni raia wananchi wake kuondokana na kutawaliwa..Na kama nilivyosema, kila nchi ina WATU na MZINGIRA tofauti hivyo hatuwezi kuiga nchi kama Mareakani ambayo inasherehekkea Uhuru wake July 4, kwa sababu ndiyo siku nchi hiyo ime declare Uhuru kutoka kwa koloni la Muingereza na zikiwemo nchi 13 tu, leo hii zimefikia 50 na zaidi na bado wanaweza kuongeza nchi nyingine wakiendelea kutumia jina la USA..
Tofauti na wao, sisi tumebadilisha jina baada ya kuunganisha nchi zetu mbili bila kufikiria mbele maana ni asili yetu kufikiria kwa marefu ya mkono. Kesho tukiungana na Kenya au Uganda lazima tutabadilsiha jina na vivyo hivyo maana Muungano wetu bado una tabaka za kijamii ambazo tumeshindwa kuzivunja. Zanzibar wana/taendelea kusherehekea siku ya Mapinduzi na halali kwao lakini haramu kwa Bara kusherehekea Uhuru wao. Kwa nini tunajaribu sana kujidanganya? ukweli unabakia kwamba Bara ipo ni nchi ambayo kisiasa tu tunaindoa ktk ramani lakini hatuwezi kufuta historia kwa siasa vile vile, Mungu apitishie mbali kesho Muungano ukifa tutarudi kwa nani?
Na kwa nini watu waseme tusherehekee miaka 50 ya Tanzania ifikapo April 2014 ikiwa hizo zitakuwa sherehe za Muungano wa nchi ambazo tayari zilikwisha kuwa HURU.. Je kweli tunakubali kupoteza historia ya UHURU wetu kwa siasa na majivuno ambayo ndiyo yalipelekea tukasahau hata kuweka kumbukumbu za vita ya Maji Maji, ukweli kamili wa biashara za Utumwa, tukawasahau wazee walioshiriki kuupata Uhuru wetu ambao kesho ktk sherehe hizi tunatakiwa kuwatunukia tunu za Ushujaa..
Jamani Watanzania wenzangu, kwa mara ya kwanza tuwe na roho ya kitajiri maana umaskini huja na mengi. Leo hii hata Mwenge umepoteza maana yake kabisa kwa sababu wananchi wameshindwa kuikubali hali halisi na hivyo mwenge unawakumbusha machungu tu. Wanafikiria gharama ya kuutembeza Mwenge lakini hawataki kupunguza posho zao wala kuacha mashangingi yao. Wanafikiria gharama za Mwenge lakini watazame ktk maharusi wakinunua pete za mamillioni zenye vito vinavyopatikana ndani ya ardhi yao. Wasifikirie haya na jinsi leo tunavyotawaliwa ktk mazingira ya ajabu ajabu lakini haramu kujikumbusha tulikotoka na tunataka kwenda wapi.
Mimi kusema kweli siku hiyo nitasimama na kufanya kitu kama Yoga, yaani nita meditate na kukumbuka nili/tulikotota, kumshukuru Mungu tumefika hapa tulipo japokuwa maskini na tuna matatizo yetu ya ndani... kumbukumbu hii ya Uhuru itanipa ari zaidi kuendelea kudai Haki na UHURU walopigania wazee wangu hata kama umeporwa na jamaa zetu.
Mjumbe kwa taarifa hakuna nchi ya Tanzania Bara inayotambuliwa na FIFA na CAF na kuruhusiwa kushiriki michuano ya kimataifa. Tafadhali acha upotoshajiIsitoshe kwa upande wao nchi yao ya Tanzania Bara haipo nchini lakini inashirikiki mashindano ya mpira kwa timu za taifa,pia vilabu vyao kila mwaka vinashiriki mashindano ya vilabu vya soka kwa nchi za Africa mashariki na kati ambapo kwahivi sasa yanga ya Tanzania Bara ndio mabingwa wao.
Coach Salum
Waungana katika pitapita zangu nimegundua wana CDM hawafurahi TZ kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Dalili zimejoinyesha;-
1. Viongozi wao katika ngazi zote kutoshiriki vikao vya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru
2. Viongozi wao kushindwa kushiriki kuukimbiza mwenge ulipofika katika maeneo yao; mfano Ubungo (mhe.Mnyika) na Kawe (mhe. Mdee ).
3. Wabunge wao wameshindwa kushiriki katika vikao vya maandalizi ya miak 50 ya uhuru pasipo kutoa udhuru.
Watanzania inabidi tutumia akili ya mbaimbawi tuwahukumu CDM katika masanduku ya kura kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2012 na tuwape kichapo kikubwa uchaguzi mkuu 2015. Hawa wamekosa uzalendo, wamebaki kushabikia sera za Mfadhili wao David Cameroon.
Maneno yako unaonyesha aidha ni mrundi ama una hasira za kukosa kuingia jumba la magogoni mwaka jana. Wewe kama ni mtz, utatembea kifua mbele kutokana na mafanikio ya miaka 50, sikulaumu sana kwa vile umri wako ni mdogo yaliyotokea baada uhuru huoni ni ya kujivunia.
Jaribu kukaa kitako na mama yako muulize kabla ya uhuru wao walizalishwa maeneo gani. Wewe hauna shukrani, UMEZALIWA zahanati, umeshoma shule ya msingi na sekondari bora.
Tujipongeze watz, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA
Ni Uvivu huu wa kusoma ndio maana sisi bado maskini na unaskini huo unatokana na uzembe wa kutosoma maelezo marefu. Hivi kweli mnasoma vitabu vyenye kurasa 200 au, sema kweli?.. Nani kati yenu mwenye mazoea ya kusoma kitabu kila siku... sidhani!..hata hivyo, turudi kwenye mada.Unahoja nzito lakini mjumbe jaribu kufupisha unakumbuka enzi zile za kuandikiana barua na kutuma kwa posta
alama za taifa la tanzania ni;
1.mwenge wa uhuru
2.wimbo wa taifa
3............
4............
5...............
kwa hiyo kuwa mpinzani siiiiiii kupinga kila kitu.tuheshimu misingi ya utaifa iliyoasisiwa na baba wa taifa hili.