CHADEMA Kususa Mwenge na sherehe za miaka 50 ya UHURU ni KUKOSA UZALENDO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Kususa Mwenge na sherehe za miaka 50 ya UHURU ni KUKOSA UZALENDO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Dec 6, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Waungana katika pitapita zangu nimegundua wana CDM hawafurahi TZ kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
  Dalili zimejoinyesha;-

  1. Viongozi wao katika ngazi zote kutoshiriki vikao vya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru
  2. Viongozi wao kushindwa kushiriki kuukimbiza mwenge ulipofika katika maeneo yao; mfano Ubungo (mhe.Mnyika) na Kawe (mhe. Mdee ).
  3. Wabunge wao wameshindwa kushiriki katika vikao vya maandalizi ya miak 50 ya uhuru pasipo kutoa udhuru.


  Watanzania inabidi tutumia akili ya mbaimbawi tuwahukumu CDM katika masanduku ya kura kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa 2012 na tuwape kichapo kikubwa uchaguzi mkuu 2015. Hawa wamekosa uzalendo, wamebaki kushabikia sera za Mfadhili wao David Cameroon.
   
 2. P

  Paul J Senior Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Miaka hamsini ni kwako mkuu unayefaidi keki ya uhuru, sisi wengine bado tunatafuta uhuru wa kweli na si uhuru wa bendera! Haingilii akilini mnasherekea miaka hamsini ya uhuru huku umasikini, ujinga na maradhi vinazidi kutuundama na waandaaji wa sherehe hizo wanaficha uozo kwa kuupaka perfume!

  Unakaa sehemu gani ya Tanzania wewe? CDM kutoenda ni haki kabisa, huwezi kupoteza billions of money wakati akina mama wanajifungulia chini, watoto wanakalia mawe, 12km kutoka magogoni hamna maji ya bomba, miundombinu duni na rasirimali za nchi zikiporwa eti mnasherekea miaka hamsini ya uhuru! Inabidi tuomboleze maana miaka hamsini ya uhuru taifa linazidi kujichimbia kaburi chini ya wakoloni weusi ccm! Heri yako usiyoyaona haya!
   
 3. M

  MUGOLOZI Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kweli kama si mnafiki, mjinga au fisadi atakuwa mwendawazimu. Haiwezekani avipe kipaumbele vitu visivyokuwa na tija. Haina maana kukimbiza mwenge nchi nzima na huku nchi iko gizani, si vizuri kufanya sherhe za miaka 50 ya uhuru huku hali ni ngumu mitaani. Utashi wa kisiasa umehamia kwenye starehe ndo maana hali ngumu. Ni sawa na kufanya birthday ya mtoto huku akiugua unakosa hela ya kwenda hospitali.
   
 4. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Wewe mwenyewe unayeunga mkono sherehe hizi za miaka hamsini ya uhuru hujui ni nchi gani inayosherekea miaka 50 ya uhuru wenzio waniita Tanzania bara, wewe sijui umetoa wapi Tanganyika, ingekuwa inaitwa TANGANYIKA basi tungekuunga mkono!!!!!!!!!!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Eti kushiriki mbio za mwenge my foot hizo gharama zinazotumika wangenunua madawati mangapi wangenunua drip ngapi za quinine, niliushika mwenge mwaka 75 nikiwa mtoto sikujua leo nikibahatika kuushika naumwagia ndoo ya maji.
   
 6. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Maneno yako unaonyesha aidha ni mrundi ama una hasira za kukosa kuingia jumba la magogoni mwaka jana. Wewe kama ni mtz, utatembea kifua mbele kutokana na mafanikio ya miaka 50, sikulaumu sana kwa vile umri wako ni mdogo yaliyotokea baada uhuru huoni ni ya kujivunia.

  Jaribu kukaa kitako na mama yako muulize kabla ya uhuru wao walizalishwa maeneo gani. Wewe hauna shukrani, UMEZALIWA zahanati, umeshoma shule ya msingi na sekondari bora.

  Tujipongeze watz, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!!
   
 7. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  unalaana miaka hamsini ya nini? ya dhiki kuu au:spy:
   
 8. m

  mwananchit Senior Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mafilili,

  Hivi wewe unaishi nchi gani?

  Kuhusu sherehe ya miaka hamsini, ni ya nchi ipi? hiyo Tanganyika, Rais wake ni nani? Bendera yake ina rangi gani? Vipi kuhusu wimbo wake wa taifa? au kwa sababu tumeshazoea kusherehekea (siyo kuomboleza) kuhusu marememu wetu Nyerere basi uzi ni huo huo tuendelee kusherehekea nchi yetu na kipenzi chetu Tanganyika iliyokufa mwaka 1964 ikiwa na umri wa miaka 3 (mitatu) tu? Kama kuna cha kusherehekea, basi ni kumbukumbu ya miaka 47 tangia kifo cha nchi yetu na kipenzi chetu TANGANYIKA!

  Kuhusu huo mwenge ambao umekuwa ukizunguka nchi nzima kwa miaka 50 iliyopita ikiwamulika mafisadi na wezi wote wa mali ya umma. Sasa hivi mwenge unachofanya siyo tena kuwamulika, bali KUWAMULIKIA ili wapore kiulaini tena kweupe!

  WATOTO YATIMA WA MAREHEMU MAMA YENU TANGANYIKA TAFAKARI VINGINEVYO MTAJIKUTA MNASHEREHEKEA MSICHOKIJUA.
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mdau kwa serikali hii na CCM hii kama ilivyo wao kuukimbiza mwenge wa uhuru ni matusi kwa walalahoi kwani dhana ya mwenge wa uhuru na vitendo vya viongozi wa CCM na sera zake zinaoana katika majukwaa na si kimatendo.Umoja ,vita dhidi ya rushwa ,ufisadi,elimu bora,umasikini,huduma bora za afya yatafute haya katika CCM.

  CCM katika kanuni zao wanasema ni Chama cha wakulima na wanafanyakazi sasa CCM ni chama cha MAFISADI na WAFANYABIASHARA.Siasa ya ujamaa na kujitegemea sasa ubepari na tegemezi. MWENGE WA UHURU KAMA ULIVYO KWA VIONGOZI WA MAFISADI NI MRADI WA KUJIPATIA FEDHA KIFISADI KUTOKANA NA MAKUSANYO YA PESA EBU WATUELEZE BAJETI YA MWENGE HUO NA PESA ZINAZOKUSANYWA NA WALALAHOI NA WAFANYABIASHARA KWA KULAZIMISHWA NI KIASI GANI NA ZINATUMIKA KWA SHUGHULI ZIPI?

  CCM NA SERIKALI YAKE INAFANYA KAZI KAMA FORMALITY AMBAPO WAKATI MATENDO YAO NA YALIYOMO KATIKA DHANA YA KUWASHA MWENGE HAVIOANI MAFISADI TELE NDANI YA CHAMA NA SERIKALI HAWAHITAJI MWANGA WA MWENGE KUWAMULIKA.

  UMASIKINI NA N.K.KUSHIRIKI KATI MWENGE HUU KAMA ULIVYO NI KUFATA MKUMBO NA SI VINGINEVYO NA KUANAOPATA FAIDA KUBWA KIFEDHA(UFISADI)KWA MBIO HIZI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 10. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Majibu ya kuboresha miundombinu ya elimu yameshapatikana. Chenji za rada zinaenda kutatua matatizo ya elimu ikiwepo kununua madawati na ujenzi wa nyumba za walimu. Shime tujiunge pamoja watz tuondoe tofauti za vyama TWENDE KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU KUENZI kazi iliyofanywa na waasisi wa nchi!!!
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mafilili,mafilili,mafilili.

  acha unafiki mtoto wa kiume utavalishwa kanga,hao watanzania utakaoongea nao ujinga huo ni wepi?
  wale wanaouziwa sukari 3000, wale wanaokula msosi 1 kwa siku?

  Au wale wanaopigwa virungu na kuuwawa na polisi wakishirikiana na wawekezaji?au wale wanaofukuzwa kwenye maeneo yao kisa wawekezaji wa hoteli za kitalii mbugani?

  Au unaongelea wale wa igunga walioibiwa utu wao kwa kibaba cha mahindii? au wale waliopigwa vurungu mbeya?

  wewe filili kweli.
   
 12. P

  PARAGEcTOBORWA Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama kuna chama ambacho hakitambui ht historia ya taifa le2 bc hakifa1
   
 13. d

  davidie JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio bure wewe mgonjwa,ebu niambie faida ya huo mwenge kwa sasa, pia hiyo miaka 50 unasheherekea nini? Ni kipi cha kujivunia mbele za watu, umri mkubwa kisha majukumu zero si heri tungekua kama rwanda wewe bichwa kubwa hakili hamna
   
 14. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wewe mwenge waq uhuru ndio nini.,mnashindwa kufanya maendeleo mnatueleza habari za kuwakiwa jua,nanui anataka ujinga huo?kutufisadi mtufisada bado mwataka mtushindishe juani,shame opone you,magamba ndi mwende mkakimbize huo upuuzi wenu.
   
 15. P

  Paul J Senior Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tujipongeze watz, TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!![/QUOTE]


  Hizi ni kaulimbiu za yule mtu ambaye baba wa taifa alimuita mjinga! Anapewa kichupa, na kuachia dhahabu! Tafakari mkuu kila jambo unalolishabikia? Maendeleo unayoyaona wewe kwa wanamahesabu huwa wanasema is negligible ukilinganisha na rasilimali ambazo tumepoteza hasa kuanzia kwenye miaka ya tisini mpaka sasa! Ole wako wewe upotezaye dhahabu na kushangilia kichupa!
   
 16. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  we MAFILILI mbona unapenda sana kuwafatilia makamanda, we dili na magamba wenzako bwana... Makamanda sikuzote huwa wanawaza mbele zaidi!
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Nchi haiendeshwi kwa kusubiri chenji kwa hiyo mnasubiri kosa lingine ili mpate chenji ya kujenga zahanati? hizo sherehe sherehekeni nyie na watoto wenu sisi ni job kama kawa.

  Nawapongeza sana makamanda kwa kususia hawataki kuwa sehemu ya unafiki kwa sababu hata maana ya sherehe yenyewe inapotoshwa imekuwa ya kisiasa si ya kitaifa tena, kama leo tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ikifika mwaka 2014 itafikisha miaka mingapi 53?
   
 18. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hii ni fursa pekee kwa watz kujiuliza, kutafakari pale tulipojikwa na kupata mkakati wa kitaifa, TUZIDI kusonga mbele.

  Mwaka 1961, graduate walikuwa 12, leo wapo mitaani hawana idadi wengine wanatumika pasipo kujitambua kushiriki maandamano ya CDM; tuwe waungwana tujitambue maendeleo yamepatikana.

  Leo watoka Mwanza hadi DSM siku moja.

  UDOM ni ishara ya maendeleo katika elimu

  Powertillers kwa wakulima walioingia katika KILIMO KWANZA
   
 19. libent

  libent JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mi naona tumethubutu kuwa nchi ya kifisadi, tumeweza kuzidisha umaskini kwenye jamii na pia tunasonga mbele kwa kuwatetea mafisadi ili waendelee kuinyonya tz yetu ili tuweze kuanza safari nyingine ya miaka 100
   
 20. eddo

  eddo JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wewe mwenge umelusaidia nini mpaka sasa?cdm haishiriki kwenye mambo ya upuuzi kama mwenge
   
Loading...