CHADEMA kusambaratika ndani ya mwaka mmoja ujao - Wassira

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano Stephen Wassira amesema chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kitakumbwa na mgogoro mkubwa ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Wassira amesema mgogoro huo ndio utakaopelekea kusambaratika vibaya chama hicho na kubaki historia hapa nchini.

Amesema mgogoro huo utahusiana na Uongozi na kuwaomba wananchi wavumilie kidogo ili washuhudie anachokisema.

Wassira amesema CDM ni chama cha hovyo na cha ajabu kilichojaa ubinafsi wa hali ya juu.

Amesema CDM kimekuwa kikipinga kila kinachofanywa na serikali ya CCM na kwao CDM hakuna zuri la CCM tangu uhuru wa Taifa hili.

Source: Majira Jumapili.
------------------------------------------------------------------------
UPDATES:
---------------
Wassira pia alimshambulia vikali Muasisi wa CDM Edwin Mtei kwamba aliianzisha CDM kama kampuni ya kifamilia na kwamba hata sasa CDM ni NGO ya Edwin Mtei.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mahusiano Stephen Wassira amesema chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kitakumbwa na mgogoro mkubwa ndani ya kipindi kifupi kijacho.Wassira amesema mgogoro huo ndio utakaopelekea kusambaratika vibaya chama hicho na kubaki historia hapa nchini.Amesema mgogoro huo utahusiana na Uongozi na kuwaomba wananchi wavumilie kidogo ili washuhudie anachokisema.
Wassira amesema CDM ni chama cha hovyo na cha ajabu kilichojaa ubinafsi wa hali ya juu.Amesema CDM kimekuwa kikipinga kila kinachofanywa na serikali ya CCM na kwao CDM hakuna zuri la CCM tangu uhuru wa Taifa hili.

Source:Majira Jumapili.

Hawa ndio mawaziri wetu wa serikali wanaolipwa kwa kodi za watanzania wote
 
Kama Shibuda atakuwa Mwenyekiti inawezekana,,, labda ZZk na Shibuda wamempa jinsi ya kuisambaratisha,,, huenda ni kweli, kwetu Bad news its good News.
 
Zee la Gombe halina jipya likisinzia likishtuka linabwabwaja bila kujua kabla ya kulala nini alikuwa akifanya, hahahahaahhhahaah Zama za kushika hatamu ndo hizo zinamong'onyoka watawala wanaona tonge linadondoka so wanaweweseka na kila aiuna ya kauli
 
kama mungu akipanga iwe ivo naamini itajukuwa,lakini kama ni Wasira wala sina wasiwasi,mana ataweza asife mpaka aone raisi wa chama pinzani kutoka cdm.

Pili kama angekuwa mzazi wangu ningemkataa kwa sababu baba muongo na mpika fitina si baba,vitabu vinatueleza mtu kama wasira ni sawasawa na mtu anayekula nyama ya mtu.
 
Huenda alishatega timing bomb huko CDM na anaona linakaribia kulipuka! Haya mambo ya siasa magumu kweli. Watu hatukuamini kama NCCR ingesamabaratika na kubaki historia. Nikikumbuka NCCR ya 1993 ikaja ile ya Mrema ya 1995 na kisha ukaja ule msambaratiko wa Tanga naogopa. Nikikumbuka akina Marando, Selasini na Komu kuwa walikuwepo Tanga siwezi kusema kitu hadi tufike 2015 na kuipita CDM ikiwa salama.
 
Naona CCM wanapata nguvu mpya ya kuongea baada ya counseling waliyopewa na Shibuda!
 
Huenda alishatega timing bomb huko CDM na anaona linakaribia kulipuka! Haya mambo ya siasa magumu kweli. Watu hatukuamini kama NCCR ingesamabaratika na kubaki historia. Nikikumbuka NCCR ya 1993 ikaja ile ya Mrema ya 1995 na kisha ukaja ule msambaratiko wa Tanga naogopa. Nikikumbuka akina Marando, Selasini na Komu kuwa walikuwepo Tanga siwezi kusema kitu hadi tufike 2015 na kuipita CDM ikiwa salama.

Mkuu Kimbunga sasa ujinga wake anaropoka kabla.Ni kweli ndiyo wanamtumia Shibuda lakini nakuhakikishia watachemsha.Shibuda anawafuasi gani CDM? Huyu Wasira na Shibuda hawana tofauti na mizimu.
 
Naona CCM wanapata nguvu mpya ya kuongea baada ya counseling waliyopewa na Shibuda!

Nadhani wamekosea sana kumtumia Shibuda kwa wakati huu.Wangekuwa wajanja wangemwambia Shibuda azushe vurugu kipindi cha kukaribia uchaguzi mkuu.
 
Back
Top Bottom