Chadema kupitia Wenje imewadhalilisha wanawake wote Tanzania kuwa wao si cho chote bali ni 'ma sweety tu'!

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,326
Katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni, Chadema kupitia kada wao Wenje, imewadhalilisha sana mama zetu na dada zetu hasa wale wabunge wa kike kwamba wao si cho chote bali ni ma 'sweety tu'.

Kama chadema haitatoa tamko la kukanusha kile alichosema Wenje kwamba si msimamo wa chama bali ni msimao wake binafsi: basi wategemee adhabu kali kutoka kwa akina mama wa Tanzania kwa udhalilishaji huu mkubwa na ubaguzi wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na kunyimwa kura za wanawake wote katika uchaguzi huu na chaguzi zijazo.
 
Unaweza kuweka total au partial content ya hayo maneno ya Wenje ili tuweze kuyachambua mkuu?
 
Unaweza kuweka total au partial content ya hayo maneno ya Wenje ili tuweze kuyachambua mkuu?
Iko Yu tube
ww umejidhalilisha mwenyewe. kwani tangu lini ma sweet wanakuwa wanaume?
Sweet wa mwanamke ni mwanamume na sweet wa mwanaume ni mwanamke. Maneno haya yanatumiwa na wawili wa jinsia tofauti walio kwenye mahaba ya kimapenzi na yanatumika kwenye mazingira stahiki ya faragha. Yakitumika kama alivyoyatumia Wenje hadharani akiwaita wabunge wote wa kike si lo lote wala cho chote bali ni ma 'sweety ' tu, maneno hayo yanakuwa ni matusi na udhalilishaji wa kijinsia kwa wabunge hao wa kike. Na hii si mara ya kwanza maneno kama hayo kutamkwa na makada wa kiume wa chadema na wakati mwingine yanaonyeshwa kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom