CHADEMA kupata ofisi mpya ya Makao Makuu-Mwenge

Huwa sikubaliani sana na misaada. Haya ndio yanaifanya CCM wasiweze kufurukuta leo mbele ya akina Rostam. CHADEMA inabidi wawe makini sana

Pesa bana kibaya huwa kizuri. Leo hii Mustapha Sabodo yanasemwa mazuri tu, nakumbuka lugha ilikuwa tofauti sana kipindi kada huyu alivyokuwa amejikita CCM. Wengi walisema ooooh anatumia jina la Mwalimu Nyerere kujiimalisha mara si mzawa,mwizi na blaaa blaaa kibao.

Sabodo leo pesa imemsafisha upinzani, kweli Marijani Rajab alisema mwenye pesa si mwenzio kwa maana ya "pesa sabuni ya roho". Sabodo mpaka sasa bado anajitambulisha kama Mwana CCM, kwanini anaendelea kumiliki kadi chafu ya CCM?. Nadhani mbali na ufadhili kuna aja ya CDM kujaribu kumshawishi ajiunge CDM na pengine kupewa kadi ya heshima.

Wahindi kwa uzoefu wangu are always opportunists na huwa hawatumbukizi miguu yao yote mpaka wawe na uhakika na future zao. Sabodo si Sabodo kama Sabodo ila utambue ana ndugu zake,rafiki zake na jamaa zake. Tambua inawezekana akawa na uhusiano na Jeeetu Patel,Chavda na wale wahindi ambao wameng'ang'ania na kutaka wauziwe nyumba za Msajili pale Kariakoo na kwinginepo town.

Ninachomaanisha ni kwamba kuna haja ya kuwa na tahadhari na pesa za Wahindi na Waarabu, wao huwa ni "Quid pro Quo" slogan.Wahindi hawa Waarab hawa ndio chimbuko la kufa/kudhoofu kwa CCM kutokana na misaada yao na baadae kutaka madaraka. Kesho mtoto wa Sabodo/ndugu yake wa karibu atataka jimbo ama upendeleo maalum wa kiuongozi CDM, huku uwezo wa uongozi hana ama biashara (tenda ndani ya Serikali ya CDM bila kuwa na vigezo).Ni vigumu kumweka pembeni huku jengo lao mmekalia na Mzee wake alichangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa chama.

There is no way CDM itaweza kuepuka misaada hii kwani inahiitaji tena sana hasa katika kipindi hiki. Sio tu Mustapha, watakuja ata wale Wahindi/wafanyabiashara aliosema Mbowe kuwa hawataki kuonekana kwa sababu ya TRA na TISS. Muhimu hapa ni CDM kutambua prons and cons za misaada hii na kujipanga.Michango ya matajiri wa enzi za TANU si ya kizazi hiki cha cameleon style.
Ni mtazamo wangu tu "hutaki unaaacha"
 
Ben,
Nashukuru kwa kutoa alert ingawa unaibatiza mijadala yetu kuwa ni ya kipuuzi. Lakini nina swali kidogo. Baada ya Uchaguzi wa BAVICHA kumalizika nakumbuka Dk Slaa alitoa kauli nzito kwamba wameweza kutokomeza mapandikizi kutoka CCM. Ni wazi kauli hii ililenga kutoa taarifa juu wasiwasi wa baadhi ya wagombea ambao waliota kama uyoga na kuwa maarufu kwenye harakati za kampeni. Emu tufafanulie maana na wewe ulikuwa ni miongoni mwa wagombea mlioenguliwa. Ni nani Dk Slaa alikuwa anamlenga kwamba ni mbegu ya CCM iliyoletwa kupandikizwa ndani ya BAVICHA?

Teeeh.....teeeeh. Kweli TUMBIRI kula kwa akili dunia haina siri. Unataka kusema BEN ni TISS, ama ndiye pandikizi la CCM ndani ya CDM?. Nimjuavyo mimi Ben ni kijana machachali ndani ya CDM na ni hazina iliyowekwa kama akiba kwa baadaye. Ben anauwezo wa juu sana mbali na lugha yake ya kigeni (mimi sio mpenzi wa lugha hii) ila ni mjuzi wa kujenga hoja na kuitetea. Sasa mbona mnafanya kama Nabii asiyekubalika kwao? Tafadhali Quinene na Tumbiri "reload" your network and come again.
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?
wewe kwa akili yako watakabidhiana jengo bila doccumention au mikataba yoyote??
 
Pamoja na kujaribu kueleza kuwa umeinukuu habari hii,hakuna sehemu ambapo Mzee Sabodo amesema amewapa CHADEMA jengo wala ofisi,amesema "nitaongea na washauri wangu kuona uwezekano".
Huyu mzee huwa hababaisha ukishasikia hivyo jua kila kitu kiko kwenye pipeline.
 
Sabodo kama Mzalendo wa kweli anajua anachokifanya nasisi wengine tuchangie hata senti tano ili Chadema waweze kutoa elimu hasa kwa watu wa vijijini ikiwa ni pamoja na kufungua mashina nakumbuka kuna program ya washa taa hii iliishia wapi? ilianzia nyanda za kusini!
 
Teeeh.....teeeeh. Kweli TUMBIRI kula kwa akili dunia haina siri. Unataka kusema BEN ni TISS, ama ndiye pandikizi la CCM ndani ya CDM?. Nimjuavyo mimi Ben ni kijana machachali ndani ya CDM na ni hazina iliyowekwa kama akiba kwa baadaye. Ben anauwezo wa juu sana mbali na lugha yake ya kigeni (mimi sio mpenzi wa lugha hii) ila ni mjuzi wa kujenga hoja na kuitetea. Sasa mbona mnafanya kama Nabii asiyekubalika kwao? Tafadhali Quinene na Tumbiri "reload" your network and come again.
Ni upuuzi kusifia mtu kwa lugha yake unaonyesha ulivyo low kwenye thinking ability.
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?
Kweli wewe ni makalio hasa, kwani umeambiwa taratibu za kisheria hazitafuatwa? taabu ya elimu ya shule za kata!
 
pesa za LOWASA zinafanya kazi indirectly! hongera sana mwana ccm Sabodo kuwasaidia hawa jamaa pesa maana hawana kitu kabisa
 
kama manati haiwezi kuua tembo, Alama ya jembe na nyundo inawezaje kuua tembo ilihali umasikini imeshindwa kuua?
 
hizo anazowapa CDM mbona ni chache tu mbona, kuna taasisi zingine anawapa Bilions of Money. Hivi majuzi tu kachangia jamatini zaidi ya Dola milioni mia
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?

inawezekana ukawa umeongea point hapa...ila mmh hapana nahisi harufu ya mashudu 2 hakuna point hapa
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo kama Mzee Sabodo,Mungu amtunze na aulinde uzee wake.Amen

Binafsi napenda kuonna chama kinapata msaada kwa watu binafsi lakini lazima sasa chama kianzishe miradi ya kukifanya kisiwe tegemezi hasa kwa watu binafsi utakyuwa ni utumwa hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom