CHADEMA kupata ofisi mpya ya Makao Makuu-Mwenge

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo, amesema anafanya mazungumzo na wataalamu wake kuangalia uwezekano wa kuipatia CHADEMA jengo lake la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, liliko eneo la Mwenge (ITV), Dar es Salaam ili wafanye ofisi ya kisasa.

Akimshukuru mfanyabiashara huyo kwa msaada wa jengo hilo na kiwanja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, alisema pamoja na msaada wa sh milioni 100 waliopewa watatumia sehemu yake katika matengenezo ya ofisi hizo, na sehemu nyingine kuingizwa katika mfuko wa ‘CHADEMA Movement for Change' (M4C) uliozinduliwa hivi karibuni.

Source: Tanzania Daima.

MY TAKE: Asante Sabodo na Hongera Chadema kwa kupata ofisi mpya, matarajio yangu mtaitumia hiyo ofisi kama chachu ya maendeleo ya chama na wananchi kwa ujumla.
 
yes..the place is very strategical...halafu pako wazi...kule kinondoni palikua hakuna space ya kutosha halafu pamejificha sana..i like this!!!
 
Ila one thing sijapenda, Dr Slaa anasema 'watatumia sehemu ya 100m kwa matengenezo ya hiyo ofisi'! Kwani walijua watapewa mshiko na ofisi? Nini mipango ya CDM kuwa ofisi kabla ya mchango wa Sabodo?
 
Ila one thing sijapenda, Dr Slaa anasema 'watatumia sehemu ya 100m kwa matengenezo ya hiyo ofisi'! Kwani walojua watapewa mshiko na ofisi? Nini mipango ya CDM kuwa ofisi kabla ya mchango wa Sabodo?
Mipango ndiyo ilikuwa hiyo.
 
Ofcourse, naona mzee Sabodo ameamua kufa kifo chema, sadaka zako Mungu anaziona.
Wenzie wazee kuliko yeye wanaendelea kuiba eti za wajukuu.
 
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo, amesema anafanya mazungumzo na wataalamu wake kuangalia uwezekano wa kuipatia CHADEMA jengo lake la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, liliko eneo la Mwenge (ITV), Dar es Salaam ili wafanye ofisi ya kisasa.

Akimshukuru mfanyabiashara huyo kwa msaada wa jengo hilo na kiwanja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa, alisema pamoja na msaada wa sh milioni 100 waliopewa watatumia sehemu yake katika matengenezo ya ofisi hizo, na sehemu nyingine kuingizwa katika mfuko wa CHADEMA Movement for Change (M4C) uliozinduliwa hivi karibuni.

Source: Tanzania Daima.

MY TAKE: Asante Sabodo na Hongera Chadema kwa kupata ofisi mpya, matarajio yangu mtaitumia hiyo ofisi kama chachu ya maendeleo ya chama na wananchi kwa ujumla.

Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?
 
Kweli Mustafa Sabodo Jembe dah! Nimemkubali sana kwa mapenzi aliyo nayo kwa chadema!
 
Hapa usiwe na shaka, anatoa kisheria na hamna wa kulinyemelea. Watoto wake pia hawana njaa na dhiki ka za mcc. Pia usisahau tuko kwenye harakati za ukombozi kwa hiyo kila upatacho unashukuru ili tuufikie ukombozi wa dhati. Aksante Sabodo
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?

Najua unakizunguzungu cha viwanja vya mpira na vingine vya ccm. lazima tuvirudishe serikalini.
 
Huyu Mzee ni Msafi na hakuna wa kumgusa, na anachukizwa na Ufisadi uliojaa serikalini. Sabodo ni Mzalendo kuliko Fisadi wa Magogoni anayeongoza Kundi la Majambazi lenye sare ya Yanga
 
Nadhani pale sio Mwenge ni Mikocheni...angalizo Chadema kuweni makini kuna baadhi ya vitu chama kinatakiwa kufanya kwa nguvu zake, siku Sabado hakiwa hayupo familia yake wakalitaka jengo lao itakuwaje?

Pamoja kwamba wewe ni wa chama cha upinzani (to be) kwenye hili upo sawa!

Nishashuhudia kesi za miskiti au kanisa, kisa kiwanja alitoa mzee kwa kauli tu
 
Back
Top Bottom