Chadema kuongoza mchakato wa kura ya kutokuwa na imani na Rais

MwanzoMugumu

Member
Jan 27, 2012
24
22
Dr, Slaa amesema kama mchakato wa kumg'ona Waziri Mkuu uatachakachuliwa bungeni CDM itawaongoza watanzania kupiga kura kwa kusaini sahihi milioni 8 za kumuondoa Rais madarakani. Ameyasema hayo Jijini Mwz katika mkutano wa hadhara maeneo ya Sahara. Amesena Rais alichaguliwa kwa kura milioni 5 tu hivyo milioni 8 zinatosha kumuondoa madarakani
 
Sidhani kama ndio utaratibu. Ngoja kina Mzee Mwanakijiji waje watueleze. Kuna thread alianzisha, nadhani lazima bunge livunjwe kwanza na kuwe uchaguzi mpya...
 
Last edited by a moderator:
kama hii ya kumng'oa rais inawezekana mi nadhani ndo njia rahisi kuliko kumng'oa waziri mkuu
 
kama hii ya kumng'oa rais inawezekana mi nadhani ndo njia rahisi kuliko kumng'oa waziri mkuu
Inawezekana ila sio kwa njia hiyo. Wapi EMT aje atueleze katiba inavo sema?
 
Last edited by a moderator:
Tunatakiwa kulilia rais avunje bunge wote warudi kwa wananchi

itatumika modality ipi maana problem kubwa ccm ndio majority bungeni halafu wanaogopa mno kurudi kwenye uchaguzi kutokana na hali ya chama chao!Je hii ya kukusanya shahihi milioni 8 anayosema Dr.Slaa kisheria au kikatiba does it hold water??
 
Dr, Slaa amesema kama mchakato wa kumg'ona Waziri Mkuu uatachakachuliwa bungeni CDM itawaongoza watanzania kupiga kura kwa kusaini sahihi milioni 8 za kumuondoa Rais madarakani. Ameyasema hayo Jijini Mwz katika mkutano wa hadhara maeneo ya Sahara. Amesena Rais alichaguliwa kwa kura milioni 5 tu hivyo milioni 8 zinatosha kumuondoa madarakani
Safi sana Dr Slaa, it is a good move japo sijui kama ina legitimacy kisheria.
 
Jk kuachia kiti kabla ya muda? labda kwa maandamano ya nchi zima yasiyokoma! chukulia leo pamoja na bunge na wananchi kuwa na sinto fahamu lakini rais ameshaandaliwa mamilioni ya kutafunwa kwaajili ya mazishi huko malawi, wabunge wanalalamika matumizi mabaya kwenye wizara lakini mbona matumizi ya rais hayachunguzwi?
 
Inaonesha kyna watu wamechanganyikiwa.

Labda sio Rais wa Tanzania anaongelea Rais wa Karatu.
 
Hii inawezekana kweli??

Hiyo haiwezekani;

Katiba ya nchi ina njia moja tu wa kumwondoa rais madarakani kwa nguvu bila ridhaa yake; nayo ni kupitia bungeni. Zinaweza kuwapo sababu nyingi za Bunge kumwondoa rais madarakani lakini raia hawawezi kumwondoa rais madarakani kwa kura za kutokuwa na imani naye. Ndiyo maana tume ya uchaguzi inatakiwa iwe ni tume yenye kuthamini sana masalahi ya nchi kwani wakishamwapisha rais hata kama hakuchaguliwa na wananchi basi wanakuwa wamelitwisha taifa mzigo mkubwa sana wa kubebwa kwa miaka mitano, na hata baada ya hapo. Nitategemea katiba mpya iwe na njia nyingi za kumwadhibu rais ili awe anawajibika kwa wananchi badala ya kuwa anazurura nchi za nje tu.
 
Tunatakiwa kulilia rais avunje bunge wote warudi kwa wananchi

Mkuu hiyo ya Dr. Slaa si sahihi hata kama Rais alichaguliwa kwa kura laki 2 huwezi kumtoa kwa sahihi za watu milioni 8. Hilo ni tatizo la kikatiba. Lakini pia ni vigumu kwa Rais kujivunja na kuitisha uchaguzi mpya katika hali kama hii ya kisiasa ambayo inaonekana CCM inapigwa pembeni kati kulia na kushoto. Labda Rais na chama chake wawe hawajitaki!
 
Dr, Slaa amesema kama mchakato wa kumg'ona Waziri Mkuu uatachakachuliwa bungeni CDM itawaongoza watanzania kupiga kura kwa kusaini sahihi milioni 8 za kumuondoa Rais madarakani. Ameyasema hayo Jijini Mwz katika mkutano wa hadhara maeneo ya Sahara. Amesena Rais alichaguliwa kwa kura milioni 5 tu hivyo milioni 8 zinatosha kumuondoa madarakani

Slaa yeye mwenyewe alipata kura milioni 2 sasa nani kampa mamlaka ya kuwasemea wa Tanzania milioni 45.

Slaa kama unataka urais huwezi kuupata kwa saini nchi hii ni ya demokrasia kuna taratibu zake za kiutawala.

Hata upate saini milioni 40 Slaa utabiki kuwa rais kivuli tu.
 
Sidhani kama ndio utaratibu. Ngoja kina Mzee Mwanakijiji waje watueleze. Kuna thread alianzisha, nadhani lazima bunge livunjwe kwanza na kuwe uchaguzi mpya...

slaa siku zote sio mtu wa kuaminika,ni mkurupukaji na mwepesi kudanganywa kwa kuwa hapendi kujuisomea,yeye anataka kuwa rais tu basi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom