CHADEMA kuongea na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Chama

Ha ha ha chawa wa Mbowe na tajiri wa JF ha ha ha

RBC mnyaki una GRANDIOSITY

RBC una GRANDIER DELUSION

Ukiguswa tu "nerves" unakimbilia kujitapa kuwa wewe TAJIRI ha ha ha TAJIRI GANI unakesha JF kumtetea Mbowe ha ha acha pang'ang'a ndugu Chawa wa femili ya Mbowe.....

Japo kuwa mimi si TAJIRI ila pia si maskini.....

Nisalimie mumeo aliyeshindwa UBUNGE.....relaaax
Very Poor !
 
Taarifa yao iliyosambazwa hii hapa



=============================================

"Ili [CHADEMA] tuweze kushiriki kikao chochote cha Msajili [wa Vyama vya Siasa] lazima zuio la vyama kufanya mikutano ya hadhara liondolewe, ili tukienda kwenye vikao, twende kama vyama huru, tusiende kama vyama vinavyotoka mahabusu." - Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, Benson Kigaila.

"Kikao cha Msajili cha Oct 21-22, 2021 kinaitwa kikao cha Wadau cha kujadili changamoto za utekelezaji wa sheria ya Vyama vya Siasa, hakuna Chama kilichompelekea Msajili changamoto ya utekelezaji wa sheria hiyo licha ya sheria hiyo kuvunjwa kwa miaka 6 iliyopita"

"Hatuwezi kukutana na wadau chini ya msajili kujadili changamoto ya kutekeleza hiyo sheria. Hatutaki kualikwa kwenda kujadili namna ya kuvunja sheria. Sisi kama chama cha siasa [CHADEMA] tumesajiliwa na tumejifunza kufuata sheria na tunaamini utawala wa sheria."- Benson Kigaila

"Sisi kama Chadema hatuwezi kwenda kwenye vikao vya Msajili mpaka mwenyekiti wetu freeman mbowe aachiwe bila masharti yoyote kwa sababu Watanzania wanajua, Serikali inajua na Dunia inajua kwamba Mbowe Sio Gaidi. Mbowe amebambikizwa kesi ili kumtesa."

"Moja ya kazi kubwa ya chama cha siasa ni kuwasemea watu ambao hawana majukwaa ya kusemea mfano ni machinga na wengine, unapozuia mikutano ya vyama vya siasa maana yake umezua majukwaa ya Watu hao wasiseme na wasiwe na sauti za kusema"

"Baada ya kusikia kilio cha Wananchi kuhusu katiba mpya, tulimwandikia Rais Mstaafu Kikwete barua ya hitaji hilo akakubali kukutana nasi, tukashauriana na mchakato uliishia ulipoishia, alipoingia Rais Magufuli tuliandika barua nne na zote hazikujibiwa"

"Mwezi April Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Samia ya kuhitaji kukutana naye, Rais Samia amekutana na makundi mbalimbali ila kundi la Wanasiasa bado, tuna imani ya kukutana naye tumweleze mambo yanayosababisha ufa kwenye Taifa hili"

"Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili"
Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili"

Mungu ibariki CHADEMA! na watu wake wote!
 
Nia na lengo letu la kuonana na Rais Samia sio kwenda kumueleza mambo yetu binafsi, bali mambo mbalimbali ya kuendesha Nchi yetu vizuri, na tuko tayari kwa mazungumzo na Rais, lakini hatuko tayari kukutana na Msajili"

Mungu ibariki CHADEMA! na watu wake wote!
Hiyo ndio habari kubwa , bahati mbaya kuna vijana duni sana wanaochangia uzi huu wanajaribu kuvuruga bila mafanikio
 
Back
Top Bottom