Chadema Kunani?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,967
22,476
Hii thread ni mjadala wenye swali moja kubwa....
IS CHADEMA STILL THE SAME?
If Yes Why...And if not then Why not?
Are these people together as they used to be?
Je kama watajiunga na vyama vingine vya upinzani na kumsimamisha mgombea mmoja..Ni sera zipi watakazozinadi?
Wameshajitayarisha?
Ama wanataka wapewe nchi based on politics na si kile watakachowafanyia wananchi?
Mjadala uanze...
 
kuna watu waling'aka walipoambiwa kwamba CHADEMA makao makuu kuna matatizo,tatizo la pale ni kwamba kuna watu wanafikiri kwamba siasa ni nadharia peke yake! Danda kama ndiyo mtafiti mwenyewe basi hana tofauti na kina Tambe hizza au kina Francis wa UVCCM!
 
Tatizo kubwa la CHADEMA ni makao makuu ambako kumejaa watu ambao matarajio yao makubwa ni kugombea madaraka kwanye maeneo wanayotoka,kwa hiyo rasirimali chache za chama adala ya kuzitumia kujenga chama wao mawazo yao yoooote ni kwenye chaguzi!

Kwa mfano ndivyo alivyofanya Akwilombe alipokuwa pale,muulize Kigaila,Erasto Tumbo,Danda,Mnyika,Komu,wote hao ndoto zao ni vipi watafaidika kwa kuwapo pale na siyo vipi chama kitafaidika kwa wao kuwa pale makao
 
Hata wakati wa kufanya mabadiliko ya Katiba ya CHADEMA ambayo iliua nguvu ya mikoa na kuleta mfumo wa wilaya zenye nguvu na mfumo buniwa wa majimbo,wanachama na wajumbe wa mkutano mkuu walipiga kelele lakini hawakusikilizwa

nakumbuka kulikuwa na mabadiliko 13 ya katiba ambayo mwenyekiti aliwashawishi wajumbe wajadili badala ya kujadili mabadiliko ya katiba nzima. Matokeo yake mfumo wa kizipa nguvu wilaya nakubakisha kazi ya uratibu kwa ngazi ya mkoa haujaonyesha matunda

Hoja hapa ni kwamba makao makuu wanaishi kwenye njozi za kufanikiwa huku kwa bidii kubwa wakikwepa njia halisi ya kuwapeleka kwenye mafanikio,ni kama vile wanataka kwenda mbinguni lakini hapo hapo wanaogopa kufa!
 
Na kibaya zaidi wakati mwingine nadharia na falsafa za chama zinakuwa kama vile zimerudufiwa kutoka kwenye vyama vingine vya ulaya,sera nyingi hadi unajiuliza hawa watungaji wamesadifu hali halisi ya nchi yetu au wanaleta ukasuku kwenye mambo yanayohitaji mbongo zinazochemka
 
Hata wakati wa kufanya mabadiliko ya Katiba ya CHADEMA ambayo iliua nguvu ya mikoa na kuleta mfumo wa wilaya zenye nguvu na mfumo buniwa wa majimbo,wanachama na wajumbe wa mkutano mkuu walipiga kelele lakini hawakusikilizwa

nakumbuka kulikuwa na mabadiliko 13 ya katiba ambayo mwenyekiti aliwashawishi wajumbe wajadili badala ya kujadili mabadiliko ya katiba nzima. Matokeo yake mfumo wa kizipa nguvu wilaya nakubakisha kazi ya uratibu kwa ngazi ya mkoa haujaonyesha matunda

Hoja hapa ni kwamba makao makuu wanaishi kwenye njozi za kufanikiwa huku kwa bidii kubwa wakikwepa njia halisi ya kuwapeleka kwenye mafanikio,ni kama vile wanataka kwenda mbinguni lakini hapo hapo wanaogopa kufa!

Lakini Mkuu si ni vizuri kama Mkoa ukiwa unakazi ya uratibu si ndio vizuri maana sasa wanakuwa wanazisimamia wilaya kwa maslahi ya wananchi?
Ama kama nimeelewa kivingine naomba unieleweshe haswa ni kwa kivipi utaratibu huo wa mabadiliko 13 yameathiri utendaji wenye nia nzuri na wananchi.
 
jamani! chadema, chadema,chadema... hivi JF ni ya chadema? mara mwajadili sera zao,mara viongozi wao, mara sijui Dr Slaa for President 2010... hapa hamvitendei haki vyama vingine.
Tanzania tuna vyama 18, ni ufinyu wa majadiliano, kila siku chadema chadema chadema... jadilini na vyama vingine
TLP
Demokrasia makini
CHAUSTA
PPT Maendeleo
UPD
DP
NCCR Mageuzi
CUF
Jahazi asilia
CCM
nk

Jiulizeni huko kwenye vyama vingine kunaendelea kitu gani ndipo mtaweza kuwa na mtizamo au chaguo bora.
 
Hoja hapa ni kwamba, uratibishaji unahitajika kwenye watu waliokomaa kisiasa,huwezi kuamini lakini ndiyo ukweli kwamba kwenye mikoa mingi watu wa wilaya wanataka maelekezo toka mkoani

lakini kwa sababu unataka kuchukua uongozi wa serikali wenye mfumo wa Kimkoa kwa nini uondoe ngazi yako ya chama ya mkoa kabla ya kuchukua madaraka ya kidola nakubadilisha hali ya mambo?

kinachotokea eti makao makuu ina haki ya kuendelea na kusimamia mambo ya chama lakini wanasema ngazi ya mkoa haina kazi. hebu tuwe wakweli wakati CCM wana nguvu mbili kwa wakati mmoja kwenye mkoa,yaani dola na chama chao,CHADEMA wao wana nguvu kwenye wilaya tuu.

inawezekanaje makao makuu kufanya kazi Nyamagana kwa ratiba waliyopanga wao bila ya mkoa kuwa na Input yake?
 
hebu tuwe wakweli wakati CCM wana nguvu mbili kwa wakati mmoja kwenye mkoa,yaani dola na chama chao,CHADEMA wao wana nguvu kwenye wilaya tuu.

QUOTE]
These are not the only political parties in TZ, broaden your discussion scope
 
jamani! chadema, chadema,chadema... hivi JF ni ya chadema? mara mwajadili sera zao,mara viongozi wao, mara sijui Dr Slaa for President 2010... hapa hamvitendei haki vyama vingine.
Tanzania tuna vyama 18, ni ufinyu wa majadiliano, kila siku chadema chadema chadema... jadilini na vyama vingine
TLP
Demokrasia makini
CHAUSTA
PPT Maendeleo
UPD
DP
NCCR Mageuzi
CUF
Jahazi asilia
CCM
nk

Jiulizeni huko kwenye vyama vingine kunaendelea kitu gani ndipo mtaweza kuwa na mtizamo au chaguo bora.

Waridi hapo juu nilisema kuwa wapinzani wanataka kumsimamisha mgombea mmoja!
Hivyo hiyo listi yako ungefupisha ili iwe tu
1)Upinzani
2)CCM

Hakuna mwenye kutaka kuijadili CCM no more!
Nilishawahi kuanzisha thread ya namna hiyo na no body is interested!
Watu wameshaanza kuipa CCM mgongo na sasa wanaangalia upande mbadala!
Na ndio maana halisi ya thread hii!
Hii thread si ya wanachadema peke yaoBali ni kwasababu CHADEMA licha ya kwamba ndicho chama cha upinzani chenye nguvuzaidi upande wa bara..Bado wana consider tiketi moja...
Na hapo ndipo mjadala unaanza kuwa ni kipi hicho watakachoifanyia nchi yetu provided wanapewa madaraka wakiwa wameungana kwa tiketi moja na vyama vingine vya upinzani?
 
Jiulizeni huko kwenye vyama vingine kunaendelea kitu gani ndipo mtaweza kuwa na mtizamo au chaguo bora.

hata kama wewe una thread kuhusu vyama hivyo unavyovionea huruma .wewe iweke humu watu waisasambue.Hata hivyo siyo kwamba CHADEMA wanatukuzwa humu ndani bali wanajitahidi kuwa wavumilivu hawako kama mzee kingunge
 
kwasababu CHADEMA licha ya kwamba ndicho chama cha upinzani chenye nguvuzaidi upande wa bara..Bado wana consider tiketi moja...
Dhana ya chadema kuwa ni chama chenye nguvu bara haitazami historia ya vyama vingi nchini, ndugu Mushi, kila baada ya miaka mitano mambo yanabadilika, hiyo nguvu unayodhani chadema inayo usingeweza kuiongea 1995, wala 2000, na hujuma walizofanyiwa wengine ktk chaguzi za 2005 zisikufanye ukadhani chadema ina nguvu kuliko vyama vingine vya upinzani.

Aidha kama kuna chama kinapinga mambo ya tiketi moja ya upinzani chama hicho ni chadema, bisha nikupe ushahidi
 
hata kama wewe una thread kuhusu vyama hivyo unavyovionea huruma .wewe iweke humu watu waisasambue.Hata hivyo siyo kwamba CHADEMA wanatukuzwa humu ndani bali wanajitahidi kuwa wavumilivu hawako kama mzee kingunge
neno la huruma limekujaje hapa? au unamaanisha determination yenu ni kuionea huruma chadema?
 
Dhana ya chadema kuwa ni chama chenye nguvu bara haitazami historia ya vyama vingi nchini, ndugu Mushi, kila baada ya miaka mitano mambo yanabadilika, hiyo nguvu unayodhani chadema inayo usingeweza kuiongea 1995, wala 2000, na hujuma walizofanyiwa wengine ktk chaguzi za 2005 zisikufanye ukadhani chadema ina nguvu kuliko vyama vingine vya upinzani.

Aidha kama kuna chama kinapinga mambo ya tiketi moja ya upinzani chama hicho ni chadema, bisha nikupe ushahidi

Nabisha..toa ushahidi!
Kumbuka mimi ni mtu ambaye nataka nione uwajibikaji kama ilivyo kwa vilio vya wananchi walio wengi!
 
Na kama huamini CHADEMA ina nguvu flani then unaota da Waridi...Na kama hauamini kuwa CCM ni taabani then sina comment!
 
Umaarufu wa CCM umeyumba!
Na kwasababu kuna nafasi ya upinzani kuchukua nchi then ni lazima tuwajadili!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom