CHADEMA kunani kanda ya Nyasa?

NgugiAchebe

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,025
688
KWENU VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA

UCHAGUZI KANDA YA NYASA UTAZAMWE UPYA,HALI NI TETE, UBAGUZI,FEDHA,NGUVU YA NAFASI,UCHU NA TAMAA YA MADARAKA ZINATAWALA NA SIO MAPENZI KWA CHADEMA.

Tunajua kwa sasa uchaguzi unaendelea wa kutafuta viongozi wa kanda,,ambazo katika nchi hii nzima kuna kanda 8 tu. Na kiongozi wa kwanza wa kanda kuchaguliwa atakua ni wa kanda ya kati.

Nataka haswa nizungumzie hali jinsi ilivyo kwa kanda ya Nyasa, ambayo ni kanda kubwa kuliko zote, yenye mikoa ya Iringa, Mbeya,Songwe,Njombe. Katika kanda hii kuna wagombea ambao wametangaza nia na wamepata ridhaa ya kushindania nafasi hiyo. Ila kuna mgombea mmoja sinto mtaja jina hapa, lakini nitamuelezea kwa undani kwa jinsi ambavyo amekua mwiba kwa chama katika mkoa wake na hii inatosha kumfanya asiwe kiongozi tunaemuhitaji kukiongoza chama kwa kanda nzima.

Uchaguzi wa kanda ya Nyasa unatarajiwa kufanyika mwezi December kama sio January baada ya chaguzi zingine. Lakini je! Chama kiko tayari kuona Kanda ya Nyasa inagawanyika na hata kupoteza makada wake kisa muheshimiwa fulani? La hasha haipaswi hata kidogo. Lazima muheshimiwa huyo azuiliwe na wenye dhamana ya kuchagua waambiwe ukweli wale wanaotoka maeneo ya mikoa jirani na anapoishi muheshimiwa huyo. Ambao hawaujui ukweli huu, wasipumbazwe na umaarufu wake.

Muheshimiwa huyo amekua uharibufu wa ndani kwa chama kwa sasa na uongozi taifa unalijua hilo.

KWANINI NI MUHARIBIFU:

1) Kwanza alianza kukataa makubaliano ya chama pale kiliposema hakitashirikiana na CCM nje na ndani ya Bunge lakini yeye alikiuka makubaliano hayo, na kushirikiana na CCM, na tabia hii ya kukiuka makubaliano na wenzake katika chama yalipelekea KUENGULIWA KWAKE kutoka KAMATI KUU YA CHAMA. Kwasasa muheshimiwa huyo hayupo kamati kuu tena. (Tafuteni mje ni nani huyo alienguliwa kamati kuu mwa huu na ni mbunge)

2) Mh. Huyo alipofuatwa na viongozi wenzake kama wakina Lissu na wakina Halima Mdee kwenye Group lao la wabunge wa CHADEMA na baadhi ya viongozi huko, aliwajibu wenzake kwa kiburi mpaka kufikia kusema "nyie wakina nani bhana" kisha aka left group

3) Amekua mchonganishi wa viongozi kwa viongozi ndani ya chama mkoani kwake(sinto utaja mkoa huo) ambako ndiko kikao cha uchaguzi kitafanyika kwa kanda ya Nyasa. Mh huyu hana mahusiano mazuri na viongozi wa chama mkoa, amefikia level ya hata kutoongea nao kwa sasa. Na bado anataka kua kiongozi wa kanda ya Nyasa, hii itazamwe upya.

4) Amekua akiwatukana CHASO mkoa kwamba wao ni Omba Omba, ile hali nilipoongea na uongozi uliopita wa CHASO mkoani humo. Walikanusha tuhuma hizo kwamba Mh. Hujawahi wapa support waliyo hiitaji kwako, na ulipotoa shilingi laki mbili walipo kwama mchago wa mahafali basi ikawa shida na walihitaji laki tano iliyopelea. CHASO inakulaumu kwa tabia zako za kujiweka juu kuliko chama na kukidharau chama. Amekua mtumia lugha ya matusi sana kwa viongozi wenzake, hujibu kwa dhihaka anapokosolewa..na mnukuu alipowahi mjibu mwenyekiti wa CHASO pale mwenyekiti huyo alipoomba mchango, muheshimiwa alijibu "huwezi fuga mbwa kwa mavi ya mlevi" akimaanisha mbwa ni CHASO mfugaji ni CHADEMA na fedha ni MAVI alafu yeye ndio MLEVI. Kama kafikia hapo kuwajibu viongozi wanaokijenga chama vyuoni kwa wasomi hivyo inakuaje kwa wasiopo katika elimu za juu?

5) Umekua ukiudharau uongozi wa BAVICHA kuanzi mkoa mpaka wawakilishi wa kitaifa waliopo mkoani kwako.

6) Kwa muda wote wa kua mbunge haujawahi kukitetea chama katika nia ya kukijenga nje ya jimbo lako, umekua ukibishana sana na uongozi wa mkoa kwenda maeneo kadha wa kadha kukijenga CHAMA na umewekeza nguvu nyingi jimboni kwako kwa maslahi yako tu ya ubunge.

7) Haujawa dira ya umoja katika chama, unakumbuka ulipoombwa na CHASO uwe mgeni rasmi ukakataa, na ulipoombwa umuombe Godbless Lema aje, ulikataa na ukasema hakuna mbunge anaeweza kuja mkoani mwako bila idhini yako? Mpaka mahafali yalihairishwa na wana CHASO na BAVICHA wakaumia sana dhidi yako?
Ulikataa kufanya maandalizi ya lile KONGAMANO lililohusu "HALI YA MKWAMO WA KISIASA ZANZIBAR" lililo andaliwa na BAVICHA kupitia CHASO mpaka BAVICHA kupitia CHASO wakaamua kumuomba Tindu Lissu mbunge wa jimbo la mkoa mwingine aje, na Lissu bila hiana alikuja. Na wewe kwa aibu ukaja kwenye mdahalo huo tena ukajiweka high table. Mh. Umepotoka na hautufai kutuongoza kanda ya Nyasa.

MH NA DHANA YA UBAGUZI

1) UBAGUZI WA KUIHUBIRI FEDHA NDANI YA CHAMA. Umekaririwa ukitamka matamshi ya kibaguzi dhidi ya mgombea mwenzako katika kinyang'anyiro hicho(video clip tunayo) umesema, hutuwezi kua na kiongozi wa kanda asiye na PESA? Je! CHADEMA kwa sasa imeamua kuihubiri pesa na kumuona mtu huyu afanyalo ni sahihi? CHAMA TAIFA FUATILIENI UKWELI HUU WAITENI WATU WA CHAMA WATASEMA UKWELI, MH huyo amewa bagua watu kwa tuhuma za kuwapa pesa baadhi ya watakaopiga kura ili wampigie kura (Mh achunguzwe)

2) UZAWA, Mh. Huyo amenadi ubaguzi wa kiuzawa kwamba mpinzani wake katika nafasi hiyo si mwenye asili ya Nyasa, kwakua tu ana asili ya Kimasai. Amejaribu kumuundia ubaguzi huo ili yeye achaguliwe.

DHUMUNI KUU LA MH. HUYO

Mpaka tunaadika makala hii, dhumuni haswa la Mh. Huyo ni kuitaka nafasi ya yeye kua mjumbe wa kamati kuu na sio kukijenga chama (Trust me). Kwakua amepoteza sifa za kua kwenye kamati kuj kupitia sifa ya ubunge wake. Sasa kwakua anatambua ukiwa Mwenyekiti wa kanda inakupa sifa za kua mjumbe wa kamati kuu moja kwa moja ndio maana mh. Huyo amepagawa na kusaka nafasi hiyo adhimj kwa kila njia na hila.

WANA NYASA MUWE MAKINI MTAKIUA CHAMA NA KUWAGAWA WATU,KWA KUMUOGOPA MTU AMA KUMPIGIA KURA KISA UMAARUFU WAKE.

USHAURI WANGU KWA CHADEMA.

Najua mnamjua mlengwa kusudiwa wa andiko hili, sasa ili asikivuruge chama huku NYASA ni heri mumpe huo UJUMBE WA KAMATI KUU TAIFA anakolenga. Mpeni tu kwa kupitia sifa ya ubunge wake. Asikivuruge chama, tumemuheshimu lakini inatosha, ataharibu mkimpa nafasi hiyo nyeti. Mh. Kwasasa hana mapenzi na chama tena, bali ni pesa na vyeo.
 
Kampeni za mtandaoni!Uchaguzi wa kanda hii unafanywa kuwa mgumu kwenye mtandao,ila kiuhalisia sidhani kama ni mgumu wala hauna tishio lolote kwa chama.
Naona vijana wengi wenye kujua kutumia mtandao wanampinga Kamanda Msigwa.
 
Kampeni za mtandaoni!Uchaguzi wa kanda hii unafanywa kuwa mgumu kwenye mtandao,ila kiuhalisia sidhani kama ni mgumu wala hauna tishio lolote kwa chama.
Naona vijana wengi wenye kujua kutumia mtandao wanampinga Kamanda Msigwa.
Mkuu, nimepitia kule facebook na kwenye magroup yao ya facebook wanampinga sana Kamanda Msigwa na wanataka Patrick Ole Sosopi apite bila kupingwa. Hizi ni kampeni za BAVICHA kuhakikisha mtu wao anapita
 
Msigwa anasema sosopi no mtu was kasakazini inakuaje agombee Nyasa mbona watu was kanda zingine hawaendi kaskazini?
 
Mimi sio BAVICHA ila sioni haja kwanini mtu mmoja awe na madaraka meeengi!!!
Mh.MSIGWA ni mbunge na waziri kivuli.
Awe radhi kuona na wengine wanapata nafasi ya kuonesha talanta zao.Mbona kanda ya Pwani walimwachia retired PM Sumaye kirahisi?
Nashauri kanda zote zisiongozwe na wabunge.Nafikiri ndio msimamo wa Katibu Mkuu Mashinji kuanzia kwenye sekretarieti ya chama.
 
Mimi sio BAVICHA ila sioni haja kwanini mtu mmoja awe na madaraka meeengi!!!
Mh.MSIGWA ni mbunge na waziri kivuli.
Awe radhi kuona na wengine wanapata nafasi ya kuonesha talanta zao.Mbona kanda ya Pwani walimwachia retired PM Sumaye kirahisi?
Nashauri kanda zote zisiongozwe na wabunge.Nafikiri ndio msimamo wa Katibu Mkuu Mashinji kuanzia kwenye sekretarieti ya chama.
Huyo Sosopi naye ni Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA. Awapishe wengine
 
Back
Top Bottom