Chadema Kuna Intelijensia Gani? CCM na Ikulu Hakuna Intelijensia Yeyote?

niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
116
Tunaona Jinsi Gani Vyombo vya Usalama na Ulinzi Tanzania Vinatumia Nguvu Zote Kutafuta Any Kind of Intelijensia Chadema Wakati Hizo Skills za Intelijensia Zingetumika Kujua Nani Alifanikisha Dowans Kuingia Tanesco. Chadema Kuna Intelijensia Gani Zaidi ya Upinzani wa CCM? Kweli Taifa Letu Linahitaji "Katiba" ya Kutenganisha Siasa na Utendaji Serikalini na Manufaa ya Taifa Letu. Kitendo cha Jeshi la Polisi Arusha Kupiga Risasi Wananchi Wake Linaonyesha Kabisa "Priorities" za Jeshi Hilo na Vipaji Walivyokuwa Navyo Kufanya Maamuzi Potovu. Tuki Summaries Yaliotoke Arusha Tunaona Jk Anapriorities Potofu Tanzania

Tanzania Police Force Website - Dira na Lengo
 
Wenyewe ni miguvu tu hakuna jingine zaidi ya miguvu busara hakuna kabisaa
 
Wenyewe ni miguvu tu hakuna jingine zaidi ya miguvu busara hakuna kabisaa

upo sawa kabisa wenyewe ni miguvu tu, yaani hata risasi za mipira hatuna kweli? MAKABURU ambao miaka yote tumekuwa tukiwaona kama MASHETANI ilifika kipindi huruma iliwaingia wakawa wanatumia risasi za mipira. Leo hii mwaka 2011 Tanzania nchi ya AMANI na UTULIVU wenyewe mnavyohiita hamna risasi za mipira ambazo makaburu walikuwa wanazitumia miaka 1980? MWEMA MUST GO, MWEMA MUST GO ...........
 
Niongeze kwa kuuliza ni intellijensia gani alionayo IGM na polisi wake kama bado kuna uhalifu wa kila aina ukiendelea hapa TZ ikiwa ni pamoja na watu kuuawa na majambazi,
kuchunwa ngozi,
albino kuuawa au kukatwa viungo.
Intellijensia gani hiyo kama sio unafiki tu?
 
Hakuna intelijensia yoyote bali ni uhuni wa CCM kupitia IGP. Intelijensia ambayo haiwezi kutambua wezi wa nchi hii, hawajui wamiliki wa Dowans, hawajui wageni wanaoingia Tanzania bila vibali. Wanajuaje kuwa watu wanaoandamana na vitamba vyeupe mikononi ndiyo wanaovunja amani wakati wanashindwa kutumia intelijensia kuwatambu majambazi wanaofanya ujambazi kila kukicha. Intelijensia gani inashindwa kubaini njama za wizi wa fedha za BOT(bilioni10) uwanja wa ndege.

IGP anatumia hoja za kiintelijensia kama kichaka cha cha kujificha tu wakati anatka kuhalalisha uhuni wa polisi kufanya uovu usio na kifani.
 
Back
Top Bottom