CHADEMA kumwomba Rais Samia aingilie kati kesi ya Mbowe ni kutaka Katiba ya JMT ivunjwe. Nchi hii ina mihimili mitatu iliyo na mamlaka kamili

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,531
2,000
Huku sasa kwa wanaCHADEMA ni kupaniki na hii ni baada ya Caution statement za mmoja wa watuhumiwa wenzake na Mbowe kupokelewa kama ushahidi mahakamani.

Kwa nini Mnyika J, anasahau na kutoa kauli za ajabu ambazo hazina mashiko? Kesi ipo mahakamani na rais hana mamlaka ya kuingilia muhimili wa mahakama. Lakini Mnyika anaomba rais atoe neno ili kesi ifutwe. Hii ni sawa?

Kama chama makini nilitegemea kipambane Mahakamani ili kuwashinda Jamhuri, lakini sio kuomba msaada kwenye tuta wakati wanajua mhimili wa mahakama upo huru. Hii inaanza kutia shaka huenda watuhumiwa wanakosa.

My take: Mambo ya Mahakama tuwaachie mahakama.
 
Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,428
2,000
Chadema wanataka katiba mpya imupungizie nguvu rais, lkn kwenye kesi ya mbowe wanataka rais apewe nguvu zidi ya mahakama kwa kwel Mimi ngachanganyikiwa kabisa, nikisimama nchale nikitembea nchale nyie CDM tuacheni CCM tupumue basi.
 
Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,645
2,000
Unaongea kama mtu aliyeamua ajivike ujinga kwa muda.

1) Anayemshtaki Mbowe ni Samia

2) Aliyempa Mustapha rushwa ya cheo ili kutoa hukumu ya upendeleo ni Samia.

3) Aliyembambikia kesi Mbowe na wenzake ni Samia (ndiye kiongpzi mkuu wa Polisi na majeshi yote)

Kama aliyewabambikia kesi ni Samia, aliyewashtaki ni Samia, aliyetoa rushwa kwa jaji aliyekuwa anaendesha kesi ni Samia. Unadhani ni nani mwenye uwezo wa kuifuta kesi hiyo kama si yule aliyeitengeneza?
 
Separation of powers bro.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom