Chadema kumshitaki Mkurugenzi Mwanza.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kumshitaki Mkurugenzi Mwanza..........

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 26, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Sakata la umeya Mwanza limechukua sura mpya baada ya uongozi wa Chadema kumshtaki Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa yale yanayodhaniwa ni kuvuruga uchaguzi wa Umeya na kukipendelea CCM.........................

  Barua hiyo ameandikiwa Waziri wa Serikali za Mitaa.........Bw. John Nguchika...............

  Wasiwasi wangu ni kuwa hivi Nguchika ni wa chama kipi? Je, anaweza kutenda haki hapo............na sheria zikoje................................nini nafasi ya NEC kwenye chaguzi hizo na mahakama zetu..................................

  CHADEMA wamshtaki mkurugenzi wa Mwanza


  na Sitta Tumma, Mwanza


  [​IMG] CHAMA Demokrasia na Maendeleo mkoani Mwanza kimemshtaki mkurugenzi wa jiji la hilo, Willison Kabwe, kwa madai ya kuingilia na kuharibu utaratibu wa uchaguzi wa nafasi ya Meya na Naibu wake.
  Kabwe ameshtakiwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, kupitia barua yenye kumbukumbu CDM/M/MZ/04/77/10 iliyoandikwa na CHADEMA ya Desemba 24 mwaka huu.
  CHADEMA inamlalamikia mkurugenzi huyo kuingilia na kuvuruga uchaguzi huo uliofanyika Desemba 17 mwaka huu katika ukumbi wa jiji hilo la Mwanza.
  Katika barua hiyo, iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbushi, imelaani Mkurugenzi huyo wa jiji la Mwanza, kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uongo katika ofisi ya Waziri wa TAMISEMI, kwamba madiwani wote wa jiji hilo wameshindwa kumchagua Meya na Naibu wake.
  Kwa mujibu wa barua hiyo iliyotumwa kwa Waziri wa TAMISEMI, na kutolewa nakala kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini pamoja na nyingine kwa Mkurugenzi huyo wa jiji la Mwanza, CHADEMA kinasema madiwani wa jiji hilo hawajawahi kushindwa kumchagua Meya na Naibu wake, bali Mkurugenzi ndiye aliyeshindwa kutimiza majukumu yake.
  "Ni vema tukumbushane kuwa, Mkurugenzi kama Katibu wa mkutano wa madiwani kushindwa kufuata kanuni za kudumu kamwe hakuwezi kutoa baraka kwa hatua ambazo anawaza, ofisi yako (TAMISEMI), ichukue hatua, " inasema sehemu ya barua hiyo ya CHADEMA.
  "Mkurugenzi wa jiji ni Katibu wa mkutano kwa mujibu wa tafsiri ya kanuni namba 2 ya halmashauri ya jiji la Mwanza ya mwaka 2003. Pia kifungu cha 24 (7), cha sheria ya Serikali za Mitaa na mamlaka ya miji na sheria namba 8 ya mwaka 1983 nayo inasema vivyo hivyo."
  Aidha, katika barua hiyo, inamweleza Waziri Mkuchika kwamba CHADEMA kimesikitishwa na mkurugenzi wa jiji la Mwanza (Kabwe), baada ya kuitisha mkutano aliendelea kuwa mwenyekiti, Katibu na Msimamizi wa uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya.
  Kutokana na hali hiyo, CHADEMA kimeiomba ofisi ya wa TAMISEMI kulichukulia hatua jambo hilo kwa umakini mkubwa, kwa kuzingatia sheria na kanuni za kudumu za halmashauri.
  CHADEMA, imehoji juu ya Mkurugenzi huyo wa jiji la Mwanza kujihusisha na kile kilichoitwa udanganyifu na ubabaishaji kama huo, na kwamba taarifa hiyo iligusia pia matukio mbali mbali yanayosadikiwa kufanywa na Kabwe, likiwemo la kumtangaza aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Nyamagana na mbunge wa sasa, Ezekiel Dibogo Wenje (CHADEMA), kuwa siyo raia wa Tanzania.
  Mkurugenzi wa Jiji hilo la Mwanza, Kabwe, alipoulizwa na Tanzania Daima Jumapili, kuhusiana na tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake dhidi ya CHADEMA, alisema kwa kifupi: "Hizo tuhuma mimi sizifahamu, hata nakala ya barua yao sijaipata kwa hiyo siwezi kuzungumzia lolote kwa sababu nipo kikaoni muda huu."
   
 2. n

  niweze JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi Hawa CCM Ni Akina Nani Nchini Kwetu? Mbona Wananchi Tunawaachia Sana? Uchaguzi wa Raisi Wamevuruga na Kuiba, Ubunge Wameiba na Sasa Udiwani Wanavuruga na Kuwapa CCM. Wananchi Kweli Tuamke La Sivyo Wataendelea Kutuumiza na Vidonda Vikawa Vikubwa Zaidi. Utulivu na Amani ya Kimaskini Ndio Chanzo cha Kuonewa Sioni Jingene Hapa. Sasa Hivi JK Anatarajiwa Kutangaza Wakuu wa Mikoa Kama Katiba Inavyomruhusu. Wananchi "Katiba Katiba Jambo Muhimu" Tulete Revelution in Tanzania.

  "Revolution ya Inchi Lazima Ianzie Ndani ya Nchi Katika Kila Kona: Kuelimishana, Kuhamasishana na Kusukamana Kujenga Nchi Yetu"
   
 3. zoeca

  zoeca Senior Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  fafanua kumshtaki kwa nan maana hao pia ni ccm
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ipo siku! Siku ikifika watan'goka tu! Natural force combined with people's power is irressistible.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Tatizo nilionalo ni kuwa CCM yaweza kujifunga kengele yenyewe?
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Chadema wanafanya kosa kumuandikia barua George Mkuchika maana hawezi kuwasaidia kitu chochote ni bora wakatafuta njia nyingine. Labda kama wataniridhisha kwa kuniambia kuwa wamefanya hivyo kama formalities wakati wanaendelea na mikakati mingine hapo nitaelewa la sivyo wanapotezamuda tu.
   
 7. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  jamani ifikie kipndi tuwe na adabu, sijawahi kuona nchi inaendeshwa kizembe kama Tanzania , kabwe kuna barua ngapi zimo humu jf ambazo tangia mwanzo wa uchaguzi alionekana kuipendelea CCM, sasa tutafute jinsi ya kumfanya , uwezo tunao, tutafute vijana wakamle kiboga, au tumpoteze duniani
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nadhani hatua hiyo ni formality zaidi ili kama wakichukua hatua zaidi iwe kielelezo.
  Hata hivyo kama wengi wetu tujuavyo Kabwe anatetea masilahi ya CCM na hakuna litakalomfika kwa madudu ananyoyafanya tokea kabla na baada ya Uchaguzi mkuu.
  Inahitajika mbinu mpya ya kuwashughulikia watu aina ya Kabwe. Wasomali wamegundua namna ya kuwafanya matajiri warudishe walichojilimbikizia, Wapalestina wao wameendelea mbinu yao kujiondoa kwenye makucha ya Israel, Niger Delta walipiga kelele wakachoka wanachofanya kwa sasa tunakijua n.k
  Mbinu ipi jamani inafaa kwa mazingira yetu??
   
Loading...