CHADEMA kumjadili Kikwete

pefla

Senior Member
Jan 31, 2012
105
74

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), inakutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, leo na kesho, katika kikao chake cha kawaida, ambapo mbali na mambo mengine itamjadili Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, ilisema kuwa Kamati Kuu itapokea taarifa ya utekelezaji kutokana na maazimio ya kikao cha dharura kilichokutana Septemba 9, mwaka huu.

Kikao hicho mbali ya kuagiza chama kimwandikie barua rasmi Rais Kikwete ili asimamie utekelezaji wa baadhi ya masuala yaliyoko kwenye mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Kamati Kuu pia iliazimia masuala kadhaa.

Miongoni mwa masuala hayo ambayo yaliazimiwa ni kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema, na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.

CHADEMA iliazimia hivyo kwa kuzingatia kwamba mauaji kadhaa yametokea mikononi mwa Jeshi la Polisi ambalo liko chini ya usimamizi wao; na vilevile waliazimia kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Morogoro na askari waliosababisha mauaji ya raia wasio na hatia Morogoro na Iringa wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kukionya chama chake kuacha kutegemea nguvu ya jeshi la polisi katika kukabiliana na wapinzani, mpaka sasa bado hajajibu barua aliyoandikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kuhusu mauaji yanayofanywa na jeshi hilo kwenye shughuli za chama hicho.

Hata hivyo, watuhumiwa wanaolalamikiwa na CHADEMA wakitakiwa kujiuzulu, kufukuzwa au kuchukuliwa hatua za kisheria, bado Rais Kikwete ameshindwa kuwachukulia hatua yoyote mpaka sasa. Kwa mujibu wa Makeni, kikao hicho cha siku mbili, mbali na kupokea taarifa hiyo kuhusu Rais Kikwete, pia kitakuwa na ajenda tatu ambazo ni taarifa ya hali ya siasa nchini; mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya nchi; na Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).

Mara kadhaa viongozi wakuu wa chama hicho, wamekuwa wakimkumbusha Rais Kikwete kujibu barua yao na kuwachukulia hatua wahusika ili kuondoa hofu ambayo imetawala kwa umma kuhusu mauaji ya raia yanayozidi kujitokeza.

CHADEMA katika barua hiyo kwa Rais Kikwete walitoa wito wakimtaka aunde tume ya huru ya kiuchunguzi ya kimahakama (Judiciary Commission of Inquiry) kuchunguza vifo vilivyotokea katika mazingira tata katika mikoa ya Arusha, Tabora, Singida, Morogoro na Iringa.

Pia kutokana na utendaji wasiokuwa na imani nao wa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, Kamati Kuu ilimtangaza kuwa ni adui wa demokrasia asiyefaa kuwa katika nafasi aliyo nayo.
Kamati Kuu iliazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, CHADEMA haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine.

Likini pia azimio hili hadi leo halijatekelezwa pamoja na lile la kutaka vyombo vya habari vya umma kuripoti taarifa zao bila upendeleo wowote kwa weledi, maadili na utaalamu wa hali ya juu kutokana na kuendeshwa kwa kodi za wananchi.

 
Chadema wanamjadili JK kwani wameishamkubali kama rais wao.
 
Chadema wanamjadili JK kwani wameishamkubali kama rais wao........

Mkuu Ritz,JK aliwaambia hawana rais mwengine zaidi yake wakajifanya kichwa ngumu na walijaribu kumtia ujinga babu na kutaka kuingia ikulu kimabavu wameshindwa.

Sasa wanaona aibu kutamka hadharani kwani hata picha ya rais usikute zipo ofisini kwao wamezitundika kwa kumbukumbu.
 
CCM mbona mnamngangania slaa hivyo hata kama mamluki tuachieni tunamkubali mamluki kwa miaka 17 mbunge kwa miaka 15 kagombea uraisi mpaka sasa tume haijui matokeo halisi.

Sisi tunamkubali katibu wetu mkuu anajenga chama yupo kila kona.
 
-Sasa kama ni mamluki si ndiyo mngefurahi zaidi? Tangu lini CCM wakawa na uchungu na mamluki wetu?Kama Dr.Slaa ni mamluki basi mamluki wa aina hii ndiyo wanaotufaa kuliko wanasiasa na wanaharakati wengine
 
Elimu fake hasa degree uliyonayo ya kubebwa na Prof. Ibrahim Juma ndio tatizo. Pia unasumbuliwa na aphasia. Wahi Milembe!........

Mkuu mie nimehoji Chadema wamemkubali rais Kikwete mpaka wamjadili? Wanamjadili ili iweje? Sasa wewe badala ya kujibu hoja unaleta viroja.
 
-Sasa kama ni mamluki si ndiyo mngefurahi zaidi? Tangu lini CCM wakawa na uchungu na mamluki wetu?Kama Dr.Slaa ni mamluki basi mamluki wa aina hii ndiyo wanaotufaa kuliko wanasiasa na wanaharakati wengine
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Mkuu Ritz,JK aliwaambia hawana rais mwengine zaidi yake wakajifanya kichwa ngumu na walijaribu kumtia ujinga babu na kutaka kuingia ikulu kimabavu wameshindwa.

Sasa wanaona aibu kutamka hadharani kwani hata picha ya rais usikute zipo ofisini kwao wamezitundika kwa kumbukumbu........

Mkuu Mingoi,
Hawa viongozi wa Chadema wanaangaika bure na kupoteza muda wao!

Wakiwa kwenye majukwaa wanasema hawamkubali rais, wengine wanamuita rais dhaifu halafu hao hao leo tena wanamjadili baada ya kikaoo wanagawana posho ambazo ni kodi zetu (Ruzuku)

Sasa hapo dhaifu sijui ni nani.
 
-Sasa kama ni mamluki si ndiyo mngefurahi zaidi? Tangu lini CCM wakawa na uchungu na mamluki wetu?Kama Dr.Slaa ni mamluki basi mamluki wa aina hii ndiyo wanaotufaa kuliko wanasiasa na wanaharakati wengine
 
Back
Top Bottom