makundi4619
JF-Expert Member
- Jul 12, 2012
- 486
- 141
uongo upi wameongea mkuu' au wewe na Nape mnafanana?
Umempa jibu lenye mashiko! Mafisadi yamezoea kila kukicha ni uongo na uzushi Napa ataipata fresh safari hii
uongo upi wameongea mkuu' au wewe na Nape mnafanana?
Mahakama ipi atakayokwenda? Nina wasiwasi wa kesi ya nyani kuhukumiwa na ngedere.
Mkuu, Katika siasa, ukweli na uongo vyote hutumika, ili mradi kuvuta hisia za jamii ambao ndio mtaji wa chama kisiasa. Hata chama chenu, si yote wasemayo ambayo ni kweli. wamekuwa wakitumia madhaifu machache ya kiutendaji ili kuvuna wanachama wengi, ambayo hata kama leo wangeingia madarakani, si rahisi kutimiza matazamio wanayowatazamisha jamii. Hii ndiyo maana tunaita kuwa siasa ni gamba gumu, kwa kuwa ni lazima uvumilie kusikia maneno mazito. Hii ndiyo inayo weza kutofautisha mwanasiasa aliyekomaa na mwanasiasa anayejifunza. Kisiasa, mahakamani huwa hatuendi ila tunaenda kwa wananchi. anayekimbilia mahakamani ni mwanasiasa uchwara. hivyo usikimbilie kuona kama mwenzenu karopoka, ila hiyo ndiyo siasa
Tusife moyo. Kuna watendaji wazuri tu katika mahakama zetu. Mifano ipo kama wabunge wa CDM kushida kesi za uchaguzi kupitia vyombo vyetu vya mahakama. Mungu yupo atawainua wenye kutetea haki katika nchi yetu inayoelekea kubaya.
Nafikiri CHADEMA kupitia mheshiwa mnyika wako sawa kwenye hili. Nape alikataa kutoa ushahidi akisema anakumbuka muda muafaka ufike ndo amwage data nakumbuka aliyasema haya wakati akihojiwa na Fina Mango. Nafikiri wakienda mahakamni ukweli ndo utajulikana,,,, so usiwatishe CHADEMA kutumia haki yao ya kikatiba mkuuNingeshauri muachane na nape, mtaaibika bure. Mnyika my brother huenda hii issue ndani ya chama chako huijui ndo maana unakurupuka. Nakuhakikishia kwa hili nepi atawaaibisha. Dili nzimz anaifahamu mbowe na lema nyie wengine bendera tu. Kama unabisha, komaa na nape mwiho wake zigo utabaki nalo peke yako.
na nyie chadema bwana, mnahangaika na domo kaya lile? hebu asiwapotezee muda wa kufanya mambo ya msingi achaneni naye aendelee kugombana na EL wake
mbona mnyika alibanwa na mwigulu akashindwa kuongea
maelezo aliyotoa mnyika na vielelezo spika alilimaliza kimya kimya style alivomaliza lile la kamanda lema na pinda!!
Kumbe mkuki ni kwa nguruwe tu ee?mbona mnyika na chadema wote kila siku wanazusha,wanaongea uongo,wanawapotosha wananchi au ndio ile nyani haoni kundule?