Chadema kulikoni? Utitiri wa Vyeo (Mpango madhubuti wa kulindana huku mkibomoa chama)

Status
Not open for further replies.
Ndugu yangu, Tuntemeke, ukileta ukosoaji wowote wa Chadema humu jukwaani, najua kitakachokupata.

Japo mimi sio Chadema na huwa huru to speak my mind, nimekusoma na kugundua mwenzangu una matatizo!. Kwa wewe ni Chadema, si busara kuleta sebuleni kuanika nguo zenu za ndani mbele ya wageni!. Acha kwanza huyu mgeni kwa jina la 'Arumeru' apite ndipo uendelee kutuanikia mauchafu yenu ya ndani mbele ya kadamnasi ya watu kwa kudhani yatasaidia!.

Kisaikolojia unaonekana kuna vitu umeumizwa, na inawezekana wewe nyota yako ni nnge, hivyo umedhamiria ku hit back with a sting, ili kujeruhi Chadema, ili kikiangukia pua huko Arumeru, wewe ndio upate gratification!.

Just do the right thing at the right time!, this is not the right time kwa hayo. Sasa Chadema needs to come together mote than anyother time, ili kikishindwa, kisitafute mchawi bali kikae chini na kujitathmini upya, sio kuangalia wapi kilipoangukia, bali pale walipo jikwaa!.

Leo Pasco umetoa point...

Huyu Tuntemeke anashida binafsi na viongozi wa juu wa chadema...akidhani kwa kufanya hivo itakuwa ni faida. Ngoja nifananishe cdm (chama kinachokua/kipya) na biashara mpya...Ukiwa wewe ni mfanyabiashara ukitaka faida kwa haraka na kuepuka gharama ya uendeshaji karibu kazi nyingi utafanya mwenyewe au utawapa wachache kazi nyingi iwezekanavyo ili kuepuka gharama za kuajiri wengi na kuwalipa... Tuntemeke haelewi misingi hii. Wakati bado chadema kinahitaji kukua na kujiendesha kwa kujitolea sana na kwa gharama kidogo sana maana nahisi hawana pesa nyingi za kuwa na team kubwa ya watu kugawana hizo titles anazotaka zisambazwe kwa wengi, basi hapo wachache watafanya kazi nyingi sana kwa gharama kidogo na huenda hata sehemu kubwa wanajitolea....suala hapo nadhani nani atapewa ... yeyote yule...Hata Tuntemeke ungeweza kuwa miongoni wao ila bahati mbaya umekuwa sio miongoni mwao au kama ni miongoni mwao basi wewe ni mnafiki na unashida kubwa sana kichwani mwako....

Nimefuatilia threads za Tuntemeke karibu zote yeye ni kwamba anakisilani na chadema...na nilishawahi sema kuwa ni wale walio tumwa au kununuliwa kwa mission maalum ya kubomoa chadema isifanikiwe. But hata kama cdm viongozi wake anawaona wanamapungufu mengi....ambapo siwezi kushangaa maana nao ni wanadamu....basi Tuntemeke unamapungufu mengi zaidi na unaonekana wazi sana katika threads zako. Pasco amekuambia unashida ya kisaikolojia na kuna kitu umeumizwa nacho....kuna ukweli mkubwa sana katika hilo. Sasa dawa si hivo unavo fanya bali ni heri kutulia au kuachana kabisa na huo mpango mbaya ulio nao haukuasidii wewe wala taifa letu

Furaha ya wanachadema ni kuona haya yanasemwa kule>>>>ccm,cuf,tlp...yaani hapo hamuwezi kumuita mtu mental impired au katumwa kuja kuichafua ccm,cuf na tlp.
Hivi mnajibu hoja au mnaegemea kuangalia huyu ninani na kapost nini?au kumchambua mtu ilihali hata maandishi hamjasoma?.
Tujadiliane juu ya hili la mrundikano wa vyeo na sio jina la TUNTEMEKE, yaani limekuwa mwiba kwenu?
 
Mkuu Pasco,

Ni kweli kuan hulka hiyo hasa katika challenges zizazo iface CDM.Ila mleta mada anaonekana kama yuko kwenye vita na CDM,Sio mkosoaji kama anavyojiita yeye.Ni mtu ambaye anahuzunika kutokana na kukosa nafasi fulani.So anaamua kukichafua chama kwa nguvu zote.Nina wasiwasi atakuwa sio MwanaCDM kwa maana ya kuwa na Mapenzi na CDM.Amekuwa Pandikizi na CDM wamemgundua na kumweka pembeni,so is fighting the war

Hivi kweli kusema ukweli ni kukichafua chama?,,,,ulitaka tuwetusema kuwa chadema yatikisa arumeru,Dr.slaa amwamini Mnyika na kumkabidhimikoba kibao ya uongozi,Chadema si mafisadi...n.k.

Kuwekwa pembeni kivip? bado sana na ni baadae sana
 
Nadhani nihoja nzuri lakini haijakaa vizuri na badala yake inaonekana ni hoja ya kulazimisha.

a. Ni vyeo vingapi kiongozi mmoja anaweza kuwa navyo? Well, achana na Mnyika for a second tuzungumzia katika maisha ya kawaida ya watumishi mbalimbali. Kuna watu ambao ni Wakurugenzi katika nyadhifa mbalimbali za utumishi. Kwa mfano, Dr. Dau wa NSSF unaweza ukafikiria ni cheo pekee alichonacho. Lakini ukiulizwa vyeo vingine alivyonavyo mara moja utaweza kuona mlolongo wa vyeo/nafasi mbalimbali. Siyo yeye tu hata ukimtafuta Msechu au mzee Mengi utashangaa nafasi mbalimbali walizonazo. Swali la 'how many are too many" ni swali ambalo siyo la CDM tu bali karibu la watendaji wetu wote. CCM kuna watu wana vyeo hadi unaweza ukashangaa! Kuna watu wanavyeo kwenye bodi, chuo, taasisi, kanisani/msikitini, na kimataifa!

b. Vyeo vya utendaji na vyeo vya kujitolea. Wapo watu - acha viongozi wakubwa - ambao nao wana nafasi mbalimbali za kujitokea. kwa mfano kuna watu wana vyeo vya ofisini na wana vyeo kwenye vyama vyao vya kazi, wanavyeo kwenye misikiti au parokia zao, na wanaweza kuwa na nafasi katika taasisi fulaniya pembeni. Hivyo, kuna uwezekano mkubwa tu hakuna mtu hata mmoja ambaye ni kiongozi maarufu ambaye ana cheo kimoja tu au nafasimoja. As a matter of fact inaweza kusemwa kwamba mtu ambaye ana nafasi moja tu inawezekana hana mvuto na si kiongozi mzuri! Mtu mwenye mvuto, na kiongozi mzuri anatafutwa na utakuta anakataa nafasi nyingine.

c. Kutokana na hayo mawili ya juu ni vizuri basi kutofautisha nafasi/kazi/vyeo vya utendaji na vile vya kujitolea ambavyo havihitaji mtu kufanya kazi 24/7. Kwa mfano, kuwa Katibu wa wabunge wa Dar siyo kazi ngumu hivyo na ni wazi mmojawapo wa wabunge atakuwa hivyo!

Kwa ufupi ni kuwa japo hoja inapendeza lakini ilivyokaa imekaa bila mahali pa kusimamia. Ukitaka kuiona ilivyo jiulize - ni kiongozi gani maarufu ndani ya CCM ambaye ana nafasi moja tu? halafu jiulize Ni kiongozi gani maarufu nchini ambaye ana nafasi moja tu ya kiuongozi? Ukimpata na kuonesha kuwa yupo basi hoja itakuwa na nguvu!
 
Na hapa je?
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM

Mwanakaijiji;
Hii ni habari ya Chadema, mimi ni mwanaccm napita tu lakini kwa ufupi hicho ulichoandika ni mfumo ambao upo Tanzania lakini swali la msingi la kujiuliza je huko kupeana mlolongo wa vyeo ni kwenye kuboresha ufanisi au kulinda maslahi ya wachache? Turudi kwenye Chadema niliwahi kusema CDM walichofanya ni copy and paste utaratibu wa CCM lengo hasa la mfumo wa CCM ni kukifanya kikundi cha viongozi wachache kuwa na monopoly power dhidi ya wanachama wa kawaida, na ndio sababu maamuzi mengi makubwa yanayofanywa na CC na NEC ya CCM hayawakilishi maoni ya wanachama wa kawaida, siwezi kuilaumu sana CCM kwa sababu ni chama ambacho kilianza tukiwa na mfumo wa chama kimoja itachukua muda kujiendesha kidemokrasia; alichosema Tuntemeke hicho kipo ndani ya Chadema wala huitaji rocket science kulielewa, siongelei unazi wa kisiasa ila labda niwaulize wanachadema ile tenda aliyopewa mwenyekiti ya mamilioni ya fedha vilitumika vikao na vigezo gani? Kama chama kingekuwa na utaratibu wa kweli ni wazi mh. Mbowe asingeweza kufanya biashara ile, ilkuwa ni rahisi sana kwake kwasababu tayari alishautengeneza mfumo wa kulinda maslahi yake binafsi, ikiwa kama vyeo vyenyewe watu wanafanya kwa kujitolea kunasababu gani kumpa mtu majukumu mengi? Ukweli ni rahisi sana kurubuni watu 10 lakini ni kazi kubwa sana kurubuni watu 100.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Wewe ni Mzushi na Mzandiki mwenye kutaka kupandikiza migogoro CDM.Huna nia njema na chama zaidi ya Uchafuzi tu.Okay kwa mnyika;

JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.-INA UHUSIANO GANI NA CHADEMA?
4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA-KATIBU NI SILINDE LABDA UKO LESS INFORMED
6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA-KWA UWEZO WAKE ANASTAHILI
8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA-zitto ni nani?
10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam-Hii si nafasi ya CDM

Mkuu,hata kama unavitaka vyeo hivi wewe huwezi pewa kwa sababu huna sifa yoyote zaidi ya uzandiki

thanks!!! labda ungetumwagia na za akina lukuvi ili aone tofauti, na msekwa
 
Mkuu, hakyanani chadema wakiingia mkenge wakakupa wewe cheo utawaulia chama. Yawezkana wanakujua tabia zako ndo maana wanakupotezea, matokeo yake umebaki kulalama tu.
 
Ivi Tuntemeke ruzuku ipo chadema tu,kama umepigwa chini tafuta kazi nyingine acha majungu.yaani hapo umeshindwa kunishawishi fisadi wewe..acha vijana wapige kazi
 
Hakuna kiongozi yeyote mzuri duniani ambaye ana nafasi moja tu kama yupo natoa changamoto mumtaje
Kuwa na vyeo vingi au majukumu mengi hatukatai. Lakini kinachopingwa hapa ni ulimbukeni wa CDM wa kuwalimbikizia watu wachache madaraka.
 
Just imagine jamaa anasema tukae kimya eti kwa sababu mgeni amewasiri?yaani hakuna kuisema CHADEMA kwa sababu ya uchaguzi wa arumeru?upo adicted na mapenzi ya chadema kiasi hiki?...pole.
Kunautofauti gani na CCM waosema no kuandamana au kudai haki yako yoyote hadi BUSH aoondoke?akisha ondoka ndipo tufungue midomo yetu.Pole sana pasco
Asante, kama unadhani mimi ni Chadema, katafute thread yangu ya "CCM Imechokwa na Chadema Haijajipanga" uisome!.

Wewe unaonekana ni Chadema, hivyo vyeo hawajapeana leo, chama chako kina kazi kubwa mbele yake kuongeza mwali mpya!, why now?!. Hii timing sio fair kwa mwana Chadema kukikosoa chama chake!. Kuna ukosoaji wenye malengo mema ya kujenga/kurekebisha mapungufu, "constructive criticisim", ambao huishia kukijenga na kukiimarisha chama, na kuna ukosoaji wa kukibomoa chama , "destructive criticisim" ambao huishia kukisambaratisha chama!.

Juzi umetoa siri ya mikakati ya Chadema Arumeru kwa kuhoji matumizi ya fungu la feasibility study ili iweje?.

Thread hiyo ilisababisha wapambanaji na baadhi ya mashujaa wa chama chenu kuvuana nguo kwenye kadamnasi ya watu!. Huko sasa ni kujenga, au kubomoa?.

Mzazi mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae atamuadhibu kwa wakati muafaka ili kumfunza ila yule asiye na mapenzi ya dhati, atamuadhibu kumkomoa!. Onyesha mapenzi yako ya dhadi kwa chama chako haswa kwa wakati huu kuliko wakati mwingine wowote, lakini kama lengo lako ni kukikomoa Chadema, nimekushauri just go!.

Nyie ndio type ya wale wanaume/wanawake unatoa mapungufu ya mwezi wake hadharani ili kupata justification ya kuvunja ndoa, kuwa mstaarabu tuu kama ndoa imekushinda, achaneni kwa amani, sio kutoleana kashfa ndipo muachane!.
 
Na hapa je?
1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM

Tunataka CDM i cut na ku paste yale ya CCM? Mimi nadhani Tuntemeke ana hoja ambayo inahitaji majawabu mujarabu badala la kebehi. Nadhani pia Tuntemeke anaitakia mema CDM badala ya fikira kwamba anaiponda. CDm isiwe kama vyama vya kikomunist ambavyo vilikiwa vinataka visifiwe tu na ukikikosoa tu basi panga ama shaba ndio halali yako.
CDM ina vijana wengi ambao nadhani wanatakiwa wawe exposed kwenye utawala na naamini pi wapo vijana ambao wako tayari kujitolea kufany kazi hizo bila kulipwa ujira. Hili suala la kuwalimbikizia watu hasa wabunge vyeo litakuja kui cost CDM. Hivi hatujasikia tetesi za malalamiko dhidi ya Mnyika na Wenje? Tutasema zililetwa na Tuntemeke? Mimi tatizo langu ni hawa wabunge kulundikiwa vyeo vingi nadhani kuna hatari ya kushindwa kubalance na kujigawa katika kuvitumiki. Hivi kama kaa sasa CDM wanaonekana kuwa na watu wachache na kujilimbikizia vyeo itakuwaje hamad mwaka 2015 wamekamata dola ambapo kutakuwa na nafasi lukuki za kujaza? Wana raslimali watu za kukamata dola? Watuonyeshe hiuo raslimali watu isiwe ni Mnyika, Zitto, Wenje, Mnyika Zitto, Wenje! Kama alivyosema Dr. Slaa ushauri siyo deni lakini wangeketi chini walione hili suala kwa macho matatu.
 
Kitu ambacho Tuntemeke hajakizingatia ni kwamba nafasi za uongozi katika vyama vya siasa, na hasa vyama vya upinzani, ni za kujitolea na haviambatani na maslahi yeyote yale. Ingependeza sana kama vyeo ulivyovitaja vingegawiwa kwa vijana wetu wanaomaliza vyuo vikuu na ambao wana mapenzi na CHADEMA na wana uwezo, lakini ukweli ni kwamba ni vigumu kuwaweka hawa vijana wajitolee tu hivihivi, nao pia wanahitaji maisha. Ndio maana ni rahisi zaidi kuwatumia wabunge kwa sababu wao tayari ni full time politicians na wanaweza kubeba majukumu yote hayo ya kisiasa bila kutetereka.

Kwa upande mwingine, wale wanaofanya kazi wanaelewa kwamba hata maofisini kuna watu ambao wana majukumu mengi zaidi kuliko wengine. Watu wote wanaonyesha uwezo na ufanisi katika kazi hujikuta wakirundikiwa majukumu lukuki wakati kuna watu wengine hukohuko maofisini wanatafuta kazi za kufanya. Uwezo wetu binadamu ni mkubwa sana-tunachotofautiana na bidii. Mwenye bidii atapewa majukumu zaidi na ndiyo inavyotokea kwa Mnyika na vijana wengine ndani ya CHADEMA. Hoja hapa ingekuwa je Mnyika amemudu majukumu aliyopewa? Kwa maoni yangu ningesema sana tena kwa sana. Sasa watu wenye bidii kama Mnyika wanapaswa kutiwa moyo, na sio kukatishwa tamaa.
 
Wewe ni Mzushi na Mzandiki mwenye kutaka kupandikiza migogoro CDM.Huna nia njema na chama zaidi ya Uchafuzi tu.Okay kwa mnyika;

JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.-INA UHUSIANO GANI NA CHADEMA?
4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA-KATIBU NI SILINDE LABDA UKO LESS INFORMED
6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA-KWA UWEZO WAKE ANASTAHILI
8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA-zitto ni nani?
10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam-Hii si nafasi ya CDM

Mkuu,hata kama unavitaka vyeo hivi wewe huwezi pewa kwa sababu huna sifa yoyote zaidi ya uzandiki

Mkuu jinsi ulivomjibu mtoa mada,nimecheka sana, haahhahaahahahaa
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na umakini wa viongozi wake katika kuhakikisha kwamba vijana ni nguvu mabadiliko na wanauwezo wakuongoza na kulinda rasilimali za chama na mgawanyo wa madaraka.Sasa the top wa chama hicho wameamua kimyakimya kugawa madaraka/vyeo kwa watu wanaoona watatumika kulinda siri na mambo mbalimbali ya viongozi wa juu(zidumu fikra za Mwenyekiti)

Naweza kusema CHADEMA sasa imekomaa na kukua kuliko vile jamaa walivyokuwa wanategemea,kiasi kwamba imewawea vigumu kuukumbatia mbuyu huu wenye matawi yake karibia tanzania nzima.Hii imewapa wakati mgumu wamiliki wa chama namna gani wanaweza kulinda rasilimali zao na vyeo vyao....

Hao watu makini (tunaowaita sisi watanzania)wamekuja na mpango kabambe wa kuwagawia madaraka wale watu wanaoona watahakisha wanadumisha fikra za mwenyekiti

Naomba kutumia baadhi ya watu kama mifano tu...ilikuleta maana ya kile ninachokisema.

A.JOHN MNYIKA(Mbunge wa Ubungo)
Huyu ni mbunge wa jimbo la ubungo,amepewa majukumu ya fuatayo kuhakikisha nguvu ya vijana inaonekana.
1.Huyu ni mwenyekiti wa taasisi ya kiraia iitwayo ubungo foundation development.
2.Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa kinondoni
3.Mkurugenzi wa vijana makao makuu ya CHADEMA
4.Katibu wa wabunge wa CHADEMA
5.Waziri kivuli wa nishati na madini
6.Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA
7.Mjumbe wa sekretarait wa CHADEMA makao makuu
8.Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA
9.Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CHADEMA TAIFA
10.Katibu wa wabunge mkoa wa Dar es salaam
Hivi huyu mtu anajigawaje katika majukumu yote haya,bila shaka ni kpenzi cha the top kwa sababu anadumisha fikra za mwenyekiti.

B.HEZEKIEL WENJE
1.Mbunge wa Nyamagana Mwanza
2.Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema
3.Mjumbe wa sekretarait wa Chadema
4.Na sasa Katibu mkuu wa chadema amemteua kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje wa chadema ambapo automatic anahudhuria vikao vya utendaji wa chama makao makuu...ambavyo karibia kila baada ya siku 2 mbili vinafanyika nainatakiwa ahudhurie,,,Jimbo lipo wazi pale mwanza kwa sababu muda wake mwingi yupo pale makao makuu kwenye vikao vya chama.

C.MWIGAMBA
1.Ni mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima(freeman mbowe)
2.Ni mwenyekiti wa mkoa wa arusha
3.NI muhasibu wa chadema makao makuu
Huyu ameacha mkoa ukiwa hauna mwenyekiti(Dr.slaa analiona hilo) nakuitwa kuja kusimamia fedha za chama(uhasibu wa chadema makao makuu)Hadi dakika hii Arusha hapana mwenyekiti wa mkoa wa chama.

D.BENSON MLAMBA
1.Katibu wa CHADEMA mkoa wa tanga
2.Afisa wa habari wa chadema makao makuu
Huyu ameondolewa tanga kuja pale makao makuu kwa sababu za kusaidia kukumbatia mbuyu usiguswe na watu wengine.Ameacha mkoa wa tanga bila kuwa na katibu...huku Dr. akijua kwamba mkoa wa tanga hatuna diwani wala mbunge na chama kina suasua,Kwa mantiki hiyo huyu mtu alikuwa nakazi ya kujenga chama pale tanga.

MY TAKE:
Kumbuka hakuna chama chenye vijana wasomi na wenye utashi/uthubutu mkubwa wa kufanya mambo katika tanzania hii kama CHADEMA.....Lakini hili si rahisi kuliona Dr.slaa kwa sababu vijana waliowengi wameshatumika kwenye mbio za uchaguzi mkuu na sasa hawana thamani tena ndani ya chama hiki.
Kuna vijana wengi sana wamejitolea kujenga chama na wengine wameshapoteza degree zao kwa sababu wanakipenda chama.Wengine wamethubutu kuingia katika vinyang'anyiro mbalimbali vya udiwani,ubunge na wengine wamekuwa wakijitolea kuratibu kampeni mbalimbali za CHADEMA lakini kwa sasa nikama makarai mabovu ya kujengea nyumba.

Je?Kama chadema bado hawachukua dola wamesahau vijana wao,itakuwaje wakishika dola?
Au huu ndio ule mkakati madhubuti wa kulinda na kula keki ya chama watu wa chache huku mkiweka MORANI(tajwa) pembezoni msiguswe?.

Najua kunawatakao tukana na kukejeli kwa sabubu wamepofoka na mapenzi yao juu ya chama,huku wakijisahau kuwa chadema kinamapungufu yake hasa katika matumizi ya rasilimali watu(vijana) na kuwa dampu kama taka.
Kxeli naona swala la mamluki haulijui, na pia hauwajui ccm, ww ujui kinachoendea, hebu tusiulaumu uongozi, security matter
H
 
Mkuu Mkumbo basi watjmieni vijana hata kwenye hizo feaaibility studies ambazo naona si za kijitolea bali huambatana na mafingu. Wapeni uwezo badala ya kuwatumia akina Aweda na Mrema ambao tayari wana vyeo.
 
mushaija muraru at work ujawahi kuwa cdm
 
Nadhani hii tabia ya wanachama wetu kugombana au kutofautiana na kuleta tofauti zao humu JF ni dharau kwa jukwaa hili. Hili jukwaa sio la CHADEMA, hili ni jukwaa huru kwa Watanzania. Jukwaa hili likifanywa la chama litapoteza maana ya uwazi na mijadala na hata Uhuru.

Imekuwa kawaida sasa watu wa chama changu kuleta tofauti zao humu na hivyo kuwapa maadui zetu kisiasa silaha za kutushambilia.

Hivi Mnyika hizo nafasi zilizotajwa anazo zimepatikanaje? Amegombea? Nyingi ya nafasi ulizotaja ni za kuombwa na wenzake ili kusukuma mbele harakati zetu za kufanya mabadiliko nchini. Sisi sote tuna nafasi zaidi ya moja. Hebu angalia mimi binafsi
Naibu Katibu Mkuu
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma
Waziri kivuli wa Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Wabunge wanaotoka maeneo ya wavuvi
Kaimu Mwenyekiti wa Wabunge wa Kigoma
Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Mabunge duniani kuhusu utatuzi wa migogoro
Mjumbe Kamati tendaji ya Wabunge wa Jumuiya ya Madola Africa Region
Mbunge Kigoma Kaskazini
Mwenyekiti wa Vuguvugu la Demokrasia ya Rasilimali (movement for Resources Democracy)

On and on and on

Wakati mwingine mambo tunayokuja kuyaanika hapa wenzetu wanatucheka. Mwanachadema yeyote anayekipenda chama chake ataleta kero zake kwenye chama, kwenye vikao vya chama. Acheni upuuzi huu wa kupika majungu na fitna. Tutaonekana hopeless kabisa. Majungu na fitna yaacheni CCM.

Mnyika na Wenje ni vijana wanaokua kisiasa na waacheni wakomazwe kwa kupewa majukumu. Wana uwezo nayo. Wakielemewa tutapunguza. Mbona juzi hapa Mnyika kaachia mwenyewe Ukatibu wa Wabunge na tumempa kijana mwingine Silinde?

Mwisho hakuna cheo cha Kaimu Katibu Mkuu. Pale Katibh Mkuu hayupo, Naibu huchukua nafasi. Pale wote hawapo Mkurugenzi yeyote wa chama anaweza kukaimu. Maana naona Mnyika anasakamwa sana na nafasi hii ya Ukaimu.

Zebu tuacheni tufanye kazi. Msituchonganishe
 
Kitila mkumbo safi sana,huyu nadhani ni wale wanaosafiria meli ya kafulila na zitto.wa2 wenye asili ya kigoma ni tabu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom