CHADEMA Kukutana Kesho Dar es Salaam

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI

KUHUSU

KIKAO CHA KAMATI KUU

Taarifa inatolewa kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA itakutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Siku ya Jumanne, Machi 1, 2016 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe(MB), ambapo pamoja na masuala mengine, itajadili agenda zifuatazo;

1. Hali ya kisiasa nchini.

2. Kupokea taarifa ya vikao vya mabaraza ya mashauriano ya mikoa.

3. Kupokea na kujadili Mpango Mkakati wa Chama.

4. Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya chama katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015

Imetolewa leo Jumatatu, Februari 29, 2016 na

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Katibu mkuu sumaye mnamtangaza lini

Tunamkubali sana pia kikao kitangaze uchaguz wa Mkiti tunamhitaji Rais wa mioyo yetu lowasa awe Mkiti maana mchango wake umeonekana uchaguz wa 2015
 
Nashangaa sana kuona wanachama wa chama chetu wakikaa kimya bila kuhoji ubakwaji wa katiba. Ni zaidi ya miezi saba sasa tunakaa bila ya kuwa na Katibu Mkuu ilhali katiba inasema muda usiozidi miezi mitatu
 
Mkuu hapo ulipo huko kanisa gani!
 
Katibu mkuu sumaye mnamtangaza lini

Tunamkubali sana pia kikao kitangaze uchaguz wa Mkiti tunamhitaji Rais wa mioyo yetu lowasa awe Mkiti maana mchango wake umeonekana uchaguz wa 2015
Chadema hatuendeshwi kwa Mihemko
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI

KUHUSU

KIKAO CHA KAMATI KUU

Taarifa inatolewa kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA itakutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Siku ya Jumanne, Machi 1, 2016 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe(MB), ambapo pamoja na masuala mengine, itajadili agenda zifuatazo;

1. Hali ya kisiasa nchini.

2. Kupokea taarifa ya vikao vya mabaraza ya mashauriano ya mikoa.

3. Kupokea na kujadili Mpango Mkakati wa Chama.

4. Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya chama katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015

Imetolewa leo Jumatatu, Februari 29, 2016 na

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Tafadhali CHADEMA MSIJE JADILI WANAOTIMULIWA NA magufuli,jadiliananeni jinsi ya kupata wanachama wengi vijijini.
Nchi ilikua imeoza sana tumuache magufuli awanyooshe kidogo hao watumishi wa umma
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI

KUHUSU

KIKAO CHA KAMATI KUU

Taarifa inatolewa kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA itakutana katika kikao chake cha kawaida kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Siku ya Jumanne, Machi 1, 2016 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe(MB), ambapo pamoja na masuala mengine, itajadili agenda zifuatazo;

1. Hali ya kisiasa nchini.

2. Kupokea taarifa ya vikao vya mabaraza ya mashauriano ya mikoa.

3. Kupokea na kujadili Mpango Mkakati wa Chama.

4. Kupokea na kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya chama katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015

Imetolewa leo Jumatatu, Februari 29, 2016 na

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Red Brigade iimarishe sana ulinzi .
 
Nashangaa sana kuona wanachama wa chama chetu wakikaa kimya bila kuhoji ubakwaji wa katiba. Ni zaidi ya miezi saba sasa tunakaa bila ya kuwa na Katibu Mkuu ilhali katiba inasema muda usiozidi miezi mitatu
wewe si kada wa chadema , na ukiendelea kuleta uzushi hapa ntakulipua kwa kukuweka hadharani kwa majina yako yote matatu bila kupunguza hata herufi moja , mnafiki mkubwa sana , nakupa onyo la mwisho .
 
MKUU UNAJUA HAWA UVCCM BILA KUTAJA CHADEMA UJIRA HAUWEZI INGIA
 
Je Juma Duni Haji na Edward Lowasa wamealikwa kwenye hicho kikao?
waalikwe kwa tiketi gani ?? wale ni wanachama tu kama wengine, sema tu waliwahi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea uongozi. lakini kimsingi sio wajumbe wa kamati kuu wala halmashauri kuu
 
Back
Top Bottom