CHADEMA kuivaa ngome ya Lowassa na kuibua wanachama.. M4c

Cecy Emmanuel

Member
Jan 19, 2012
30
10
CHADEMA WAMSHUKIA LOWASSA JIMBONI KWAKE, WAVUNA WANACHAMA 700



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha kimeendelea na operesheni vua gamba vaa Gwanda ambapo wilayani Monduli imefanikiwa kuvuna wanachama wa chama cha mapinduzi (CM) zaidi ya 700 wakiwemo mabalozi na wajumbe wa serikali za mitaa na vijiji 25.



LOWASSA-Edward.jpg


Edward Lowassa

Aidha viongozi wa chama hicho wamemtaka mbunge wa jimbo hilo, Edward Lowassa (CCM) kuacha kuwahadaa wananchi sasa kwa kujionyesha anaguswa na tatizo la ajira la vijana wakati alishindwa kuyashughulikia kwa kipindi cha miaka 20 alichokuwa serikalini akishika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo uwaziri mkuu.


Pia wamedai waziri mkuu huyo aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond LTD hana nia njema na wapiga kura wake kwani ameshindwa kuwatatulia tatizo la ukosefu wa maji safi na salama huku akionekana akizunguka akigawa mamilioni ya fedha kwenye maeneo mbalimbali ya nchi fedha .


Viongozi wa Chadema waliyasema hayo juzi kwa nyakati tofauti kwenye kata za Esilalei na Mto wa Mbu wilayani Monduli walipokuwa wakifungua matawi na ofisi za kata za chama hicho ambapo jioni walifanya mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Shirika vilivyopo pembeni ya nyumba za polisi za kuishi.


DSC06712.JPG



MWENYEKITI WA BAWACHA MKOA WA ARUSHA
CECILLIAN NDOSSI (ALIYEVAA GWANDA) NA MLEZI WA MONDULI

Mwenyekiti wa Bawacha mkoani hapa, Cecilian Ndossi alisema kuwa Lowassa anakosa uhalali wa kulalamikia tatizo la ajira kwani licha ya yeye kushika nyadhifa nyingi serikalini lakini chama chake bado kipo madarakani hivyo anapaswa kuja na suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana na si kulialia kama anavyofanya.

DSC06694.JPG



Mwenyekiti wa Bavicha ambaye pia ni diwani wa kata ya Levelosi jimbo la Arusha Mjini Efata Nanyaro aliunga mkono kauli iliyotolewa na mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu kwa kile alichosema kuwa katiba ya nchi imempa mamlaka ya kusimamia na kuongoza nchi lakini ameshindwa na inadhihirishwa na vilio vya wananchi kila kona kuwa maisha magumu huku kila kukicha kunasikika taarifa za baadhi ya vigogo kujinufaisha kwa kuiba rasilimali za nchi.



Aidha kiongozi huyo wa vijana mkoa wa Arusha alikemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwataka kutowasema viongozi wa serikali ya CCM kwenye mkutano huo kwa kile alichosema kuwa huko ni kwenda kinyume na majukumu yao ya kusimamia usalama wa raia na mali zao.



DSC06705.JPG


Wananchi wakishikana mikono kuwezesha viongozi wa chadema kupita kwenda kufungua ofisi za kata ya mto wa mbu
" Chadema ni chama cha siasa kilichosajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo tuna wajibu wa kufanya siasa ikiwemo kukosoa pale tunapoona mambo hayaendi vizuri sasa leo jeshi la polisi kutuambia tuje hapa lakini tusiwakosoe viongozi halitawezekana, viongozi tumewapa madaraka ya kutuongoza hivyo wanapokosea lazima tuwaambie na naanza kuwasema hapahapa" alisisitiza Nanyaro huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza uwanjani hapo.

DSC06725.JPG



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Samson Mwigamba alisema kuwa ameshangazwa na kusikitishwa aliposikiliza risala aliyosomewa ikieleza kuwa wananchi wa mto wa mbu wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji hali inayowalazimu wakati mwingine kuchangia maji na mifugo huku kukiwa na mradi wa maji wa zaidi ya shilingi bilioni 45 ulitekelezwa kwenye eneo hilo lakini maji hamna.


Alisema kuwa mbunge wa jimbo hilo hawajali wananchi hao kwani alishindwa kusimamia fedha hizo za maji kuhakikisha wananchi wake wamepata maji safi na salama huku akisisitiza haiwezekani Monduli kukawa na kero nyingi kiasi hicho huku Lowassa akionekana kutojali kwani anaendelea kugawa mamilioni ya fedha kwenye maeneo mbalimbali nchi ambayo angeweza hata kuyaelekeza kwenye jimbo hilo kusaidia kupunguza kero hizo.

DSC06699.JPG



Mwigamba aliwataka polisi kutowasumbua vijana wanaofanya biashara ya kubeba abiria kwa pikipiki kwa sababu walihudhuria mkutano huo kwa wingi kwani kwa kile alichowaeleza kuwa wananchi wana haki ya kushiriki na kujiunga na chama chochote cha siasa hivyo waache kuwatisha ambapo aliagiza mtu yeyote atakayesumbuliwa bila sababu za msingi akatoe taarifa kwenye ofisi za Chadema ili waweze kuwapatia.



Naye Mwenyekiti wa Wilaya ya Monduli wa Chadema, Mchungaji Amani
Mollel, alimshukuru mlezi wa chama hicho wilayani Monduli, Cecillian Samson Ndossi kwa kuwasaidia kuliopia kodi ya pango kwa mwaka mzima kiasi cha shilingi 600,000.

DSC06723.JPG




Wakizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya viongozi wenzao waliojitoa CCM na kujinga Chadema, mjumbe wa serikali ya kijiji cha
barabarani, Dotto Mrisho na balozi wa nyumba kumi, Magadini chini,
Jumanne Mussa, walisema kuwa wamechoshwa na ufisadi unaoendelea ndani ya CCM kwani kwa sasa kinathamini wenye fedha huku kikiacha wananchi wa hali ya chini wakitese.

"Kwenye mkutano wa serikali kijiji tuko 25, pale ninapojaribu kutoa hoja ya kuwatetea wananchi wanyonge wenzangu ambao wote ni CCM wananipinga, nimetoka nimeona bora nije Chadema nikawapiganie wanyonge wenzangu" alisema Mrisho.


DSC06719.JPG


Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano makubwa ya pikipiki na magari ambayo yalipita kata hizo yakiwa na ulinzi mkali wa magari mawili ya polisi yaliyokuwa na askari polisi wa kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na mambomu ya machozi pamoja na askari waliovalia kiraia ingawa mpaka unamalizika mkutano huo hapakutokea vurugu yoyote.

DSC06715.JPG



POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIYEJIZUNGUSHIA MAMBOMU YA MACHOZI AKIWA AMESIMAMA KATIKATI YA BARABARA KUZUIA MSAFARA WA CHADEMA USIVUKE KUINGIA KATIKATI YA MJI​
 
patam sana hapo nilikuwepo na nilipenda saaaf peoples power!! Pamoja na kubana uwanja mkubwa ila wa2 walijaa
 
CHADEMA imekubalika mpaka kijijini Ngarash anakotoka Lowassa
 
Back
Top Bottom