CHADEMA kuiuza Nyamagana?

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,137
809
Wanabodi, mdudu anaekimaliza CCM tayari ameshaanza kuitafuna CHADEMA.

Jimbo la Nyamagana kuna mchezo mchafu sana unatumiwa na mwana CHADEMA mmoja ili kumtoa Wenje kwa maslahi ya umoja wa wafanyabiashara wa mjini Mwanza.

Kuna tetesi ya pesa nyingi sana zimechangwa kumchangia mgombea wa ubunge kupia CHADEMA ambaye ana influence kubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania, yeye ni mtu wa juu sana kwa umoja wa wafanyabiashara wa Tanzania.

Amefanikiwa sana hata kuiteka safu ya uongozi wa CHADEMA Wilaya na Mkoa kwa lengo la kummaliza Wenje kweye kura za maoni.

Kosa la Wenje ni kuwekeza kwa machinga na mama ntilie na kuwasahau wafanyabiashara wakubwa.
 
Acha kulalamika, kila mmoja ana uhuru kugombea jimbo hilo kupitia chadema as long as anakidhi vigezo vilivyowekwa na serikali na chama husika.

Usifikiri hilo jimbo kuna mtu ana hati miliki nalo.
 
Sasa kama anasifa kuna ubaya gani? Kwanza mwanza nyamagana hakuna mgombea aliyewai kumaliza miaka 10 so wenje akipigwa chini si ajabu ni mwendelezo tu wa Nyamagana kubadili wagombea kila baada ya miaka 5
 
Sasa hapo wameuzaje jimbo sasa? Kwanza ni vzr ili jimbo liwe salama zaidi,
 
Wenje hana mpinzani ndani ya CHADEMA na pia hakuna wa kumtoa Nyamagana. Wala usiwe na wasiwasi.
 
Kuna kosa gani hapo sindiyo demokrasia yenyewe kamanda.
Kosa lipo. Kama alivyosema mtoa mada kwamba pesa inatumika na huo sio utaratibu wa Chadema. Hayo mambo ya kutumia rushwa ni hukohuko CCM WASITULETEE HUKU.

Kama mtu anakuja na hoja safi na za dhati hakuna shida kama atamuangusha Wenje kwani chama hiki kinataka watu wenye hoja na ujasiri wa kuhoji basi, nasio mambo ya Rushwa.

Kama CCM yenyewe inakimbiwa na waadilifu kama Bulaya na Lembeni kwa ajili ya Rushwa itakuwaje tuiruhusu rushwa ije Chadema?
 
Mtaje kwa jina maana hapa jf hakunaga mambo ya kuficha ficha
 
Kosa lipo. Kama alivyosema mtoa mada kwamba pesa inatumika na huo sio utaratibu wa Chadema. Hayo mambo ya kutumia rushwa ni hukohuko CCM WASITULETEE HUKU.
Kama mtu anakuja na hoja safi na za dhati hakuna shida kama atamuangusha Wenje kwani chama hiki kinataka watu wenye hoja na ujasiri wa kuhoji basi, nasio mambo ya Rushwa.
Kama CCM yenyewe inakimbiwa na waadilifu kama Bulaya na Lembeni kwa ajili ya Rushwa itakuwaje tuiruhusu rushwa ije Chadema?
Kichangiwa pesa kwenye siasa jambo la kawaida kwa mujibu wa Mbowe alishasema Chadema walichangiwa pesa na Rostam Aziz na Nimrod Mkono mbona haukipinga na kuita rushwa?
 
Kichangiwa pesa kwenye siasa jambo la kawaida kwa mujibu wa Mbowe alishasema Chadema walichangiwa pesa na Rostam Aziz na Nimrod Mkono mbona haukipinga na kuita rushwa?
Mie sizungumzii kuchangiwa, nasema kama pesa hizo zitatumika kwenye rushwa basi sio utamaduni wa Chadema. Kutumia rushwa narudia tena, hiyo ni sera ya CCM tuu.
 
Mie sizungumzii kuchangiwa, nasema kama pesa hizo zitatumika kwenye rushwa basi sio utamaduni wa Chadema. Kutumia rushwa narudia tena, hiyo ni sera ya CCM tuu.
Hayo ya rushwa unayesema wewe mleta maada hamna sehemu kataja rushwa.
 
Back
Top Bottom