Wana JF.
Heshima kwa wote.
Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.
Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei, tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.
Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote, Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.
Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge, Watendaji Makao Makuu, Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo.
Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.
Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.
Nitaanza na Msafara wa kesho.
Aluta Continua
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Nina wasiwasi na Maandamano kama ndio njia sahihi ya Kujenga Chama. CCM wana Ofisi kila kata na kijiji, pamoja na daftari la wanachama, na mabalozi wa nyumba kumi. Mzingatie hayo kwanza, na mabadiliko ya Katiba yatakayotupa Tume Huru ya Uchaguzi. Vinginevyo, mtajachakachuliwa tena 2015...