CHADEMA Kuitikisa Nyanda za Juu Kusini; Safari Kuanza kesho

Ninawatakia kila la heri na Mungu aliye hai aonaye haki na ukweli awatangulie. Watasema mengi kuhusu mikutano ya chadema, watakebihi kuhusu uongozi, watawatangazia kwamba ni mafisadi. Mungu aonaye uchungu wa ukweli ulio ndani ya viongozi wa chadenana wanachadema atawaangaza siku moja. Neno ni moja tu. Haki ya mtu haipotei, mwanadamu mwenzio atajaribu kuichelewesha lakini siku ya siku ikifika; hata mbingu zinaachia. Mungu awe nanyi na tunaomba picha za kila tukio. Safari njema wote mnaoelekea huko pamoja na uongozi mzima Mungu aweke maneno vinywani mwenu.Peoples Power!!!
 
Ziara yote ya Kanda ya Ziwa niliweka picha ingawa zilikuwa zinachelewa.Refer my threads Kanda ya Ziwa.

ukweli ur the only 1 ambaye angalau tutapata picha,tunaomba zisichelewe tena, pata hata freelancer mmoja akusaidie hukohuko wapo wengi tu, pia nakushauri uwe na simu nzuri itarahisisha pia
 
Thank you dada Mtema, tunakuombea Kheri na baraka ili uweze kutujuza yatayojiri kwa usahihi na wakati.

I wish you all the Best! and be blessed.
 
Akhasante dada Regia kwa taarifa,ila nawakumbusha tu mikoa ya lindi na mtwara nayo mnatakiwa mfike,ikiwezekana baada ya bunge la bajeti.Mungu awabariki na kuwalinda viongozi,wanachama,wakereketwa na wapenda maendeleo.Aluta continua.
 
Wana JF.

Heshima kwa wote.

Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.

Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei, tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.

Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote, Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.

Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge, Watendaji Makao Makuu, Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo.

Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.

Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.
Nitaanza na Msafara wa kesho.

Aluta Continua

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

asante dada Regia. Ila nakuomba ukiwa mbeya na timu ya makamanda msisahau kuweka wazi dhambi na madudu ya yule jamaa aliyerudi ccm kuvaa magamba yaliyokimbiwa! Pia waeleze wananchi jinsi serikali ilivokula kodi yetu kwa kuzipamba barabara za nchi kwa album/picha za jk akiwa na nduguze! Pia gaweni kadi na kufungua matawi mapya. Ukumbuke pia ushauri wa kuwa na gazetì,tv na radio za chama. Mh.ukitoka mbeya fikiria pia kuweka picha zote kwenye page ya website ya chama,kama utakuwa bize nitafute ntafanya kazi iyo bure. Nakutakia mafanikio. Namuombea dr Slaa afya njema,na viongozi wote wapiganaji.
 
Kwa maneno mengine wameshaanza kukifisadi chao chao!

Hakuna ufisadi wala nini haya ni makubaliano halali ndani ya chama yakiwa na lengo la kukijenga chama.Makubaliano haya huwezi kuyalinganicha na ukwapuaji wa akounti ya EPA Benki kuu au Meremeta, Deep Green Finance,Richmond na Dowans.Chadema wanatumia vikao halali kuidhinisha fedha halali kuimarisha chama.Tofauti na ukwapuaji unaofanywa BOT kwaajili ya kuwanufaisha wachache ambao huo ndio ufisadi.
 
Mh Regia, uongozi wa CHADEMA na ndugu zangu wa Mbeya ninawatakia mafanikio mema kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa amani.

Mungu atakuwa nanyi na mbele yenu atawasha taa yakumulika kila upande. Nimefurahishwa sana uongozi wa chama kuwa pamoja na Mh Zitto akiwa ni mmoja wao.

Dr tunakuomba sana uwachunge kondoo wako asijepotea hata mmoja.:israel:
 
Mh. Waziri kivuli,
Naomba kujua kauli mbiu ya hayo maandamano. Itasaidia kuondoa sintofahamu kubwa iliyoko katikati ya watu wengi kwa sasa. Nitafurahi kupata jibu kutoka kwako au kwa mtu yeyote aliyenalo.
 
Wana JF.

Heshima kwa wote.

Ile Ziara ya Maandamano ya Nyanda za Juu Kusini imewadia.Maandalizi yanaendelea vizuri na kesho ndio msafara unaoondoka kwa Convoy kuelekea Mkoani Mbeya.

Maandamano yenyewe yatazinduliwa Mbeya Mjini Siku ya Ijumaa tarehe 6 Mei, tunatarajia kufanya Ziara kwenye Mikoa ya Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Iringa respectively.

Mkoa wa Morogoro tumeuondoa kwa sasa kwa kuwa kuna mvua nyingi na sehemu nyingine kuna mafuriko hivyo hatutaweza kufika maeneo yote, Morogoro tutakwenda baada ya Bunge la Bajeti.

Maandamano hayo kuongozwa na Viongozi Wakuu wa Chama. Makamanda Mbowe, Dr Slaa, Zitto na Arfi tukifuatiwa na Wabunge, Watendaji Makao Makuu, Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Majimbo.

Ziara inatarajiwa kuwa ya Siku 12 kila Mkoa ni siku tatu.

Kama kawaida nitajitahidi kuwahabarisha kila kitakachojiri kadiri ya uwezo wangu.
Nitaanza na Msafara wa kesho.

Aluta Continua

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
Mhe.Regia,tunashukuru sana kwa taarifa njema.Karibuni sana makamanda katika mkoa wetu wa Njombe.
Sisi makamanda wa Njombe tumejipanga kuwapokea kwa shangwe kubwa.Hapa Njombe ni jimboni kwa bibi mkora hivyo kazi itakuwa nyepesi sana.kila mtu amechoka.hapa Njombe pia ni mahala ambapo kuna mbunge ambaye amevunja rekodi ya kuingia bungeni kwa kuto kujua kusoma na kuandika.Wizi mtupu.
karibuni sana makamanda mje mtukomboe wenzenu vanyalukolo.
Huko ndiko kuliko na makamanda maarufu kama Thomas Nyimbo,Nyagawa,Lulandala na makamanda wengi wenye uchu mkubwa wa kuhakikisha CCM inafutika katika ramani ya nchi ya wabena,wakinga na wapangwa.
Mtapata mapokezi makubwa kuliko wakati mwingine wowote mliowahi kufika Njombe.:bange:
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Pamoja sn,sote mkono moja juu tukisema 'peoples power'!!mapambano bado yanaendelea(aluta continues
 
Mimi nitashiriki katika maombi ili maandamano ya kutoa elimu ya uraia yafanikiwe, kwanini nasema hivyo? nikwamba shetani anaweza kujiinua kupitia vyombo vya dola kutaka kuingilia kati ili waue watu ili waendelee na ule uzushi kwamba chadema inavuruga amani. "Mungu simamia hili zoezi ili Watanzania waijue kweli" amina
 
Kila la kheri katika mapambano ambayo yataikomboa Tanzania toka kwa mkoloni mzawa mweusi(CCM) ambaye amekuwa akatumia kila mbinu ili aendelee kuwanyonya na kuhakikisha watz wanaendelea kuwa masikini,kitaeleweka tu BAADA YA KUWATWANGA WAKAKOBOLEKA NA HATIMAYE UNGA KABISA "ili wawe rahisi kuwapeperusha wakafie mbali.
Safari Njema Mungu awe Pamoja na kila mtakachotumia.
Maneno Mabaya yatakayotamkwa juu yenu yakawe BARAKA Juu Yenu.
 
Mhe.Regia,tunashukuru sana kwa taarifa njema.Karibuni sana makamanda katika mkoa wetu wa Njombe.
Sisi makamanda wa Njombe tumejipanga kuwapokea kwa shangwe kubwa.Hapa Njombe ni jimboni kwa bibi mkora hivyo kazi itakuwa nyepesi sana.kila mtu amechoka.hapa Njombe pia ni mahala ambapo kuna mbunge ambaye amevunja rekodi ya kuingia bungeni kwa kuto kujua kusoma na kuandika.Wizi mtupu.
karibuni sana makamanda mje mtukomboe wenzenu vanyalukolo.
Huko ndiko kuliko na makamanda maarufu kama Thomas Nyimbo,Nyagawa,Lulandala na makamanda wengi wenye uchu mkubwa wa kuhakikisha CCM inafutika katika ramani ya nchi ya wabena,wakinga na wapangwa.
Mtapata mapokezi makubwa kuliko wakati mwingine wowote mliowahi kufika Njombe.:bange:
Hongereni wanauchungu na nchi yetu hakikisheni hakuna sisimizi malafi anafanya ajizi kwenye mkoa wenu wa njombe
 
Back
Top Bottom