Chadema kuishataki kampuni iliyochapisha karatasi za kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kuishataki kampuni iliyochapisha karatasi za kura

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Jun 14, 2011.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kuishtaki Kampuni ya Kalamazoo ambayo ilichapisha makaratasi ya kupigia kura chini ya kiwango, jambo ambalo limesabisha karatasi hizo kutosomeka hadi hivi.

  Kampuni hiyo ambayo inachapisha karatasi za siri nchini Uingereza, ilipewa zabuni ya kuchapisha makaratasi ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana.

  Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alisema kampuni hiyo ilichapisha karatasi hizo chini ya kiwango, jambo ambalo limesababisha kupoteza kumbukumbu za wapigakura. Dk Slaa alisema tayari wameishawasiliana na Serikali ya Uingereza na kuwasilisha malalamiko hayo.

  SOURCE: MWANANCHI JUN 14 2011
   
 2. E. J. Magarinza

  E. J. Magarinza Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wanaishitaka kwa nani sasa?? Mbona washawasilisha malalamiko yao serikali ya Uingereza kama bado hawajashitaki!!!!???
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chadema wanasema walishinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika OCT 31, mwaka jana, walitumia vigezo gani kujua kama walishinda, kwa mujibu wa Dk Slaa, a loser hiyo kampuni ambayo ilichapisha makaratasi ya kupigia kura imesababisha kupoteza kumbukumbuka za wapigakura
   
 4. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  wawashtaki tu
   
 5. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SERIKALI imekubali pendekezo la kutafakari na kuziangalia upya posho mbalimbali wanazolipwa watumishi wa umma, wakiwamo wabunge.

  Uamuzi huo wa Serikali ulitangazwa bungeni jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipokuwa akihitimisha mjadala wa makadirio na matumizi ya ofisi yake uliodumu kwa wiki moja.

  Pinda alitoa maelezo hayo wakati akijibu hoja za wabunge hususan wale wa kambi ya upinzani ambao tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti mwanzoni mwa mwezi uliopita, wamekuwa wakipinga malipo ya posho mbalimbali wanazolipwa watumishi wa umma.

  “Serikali italitafakari kwa undani na kuangalia posho zipi hazina tija na zipi zina tija na manufaa ya kuongeza ufanisi ili ikiwezekana zihuishwe na kujumuishwa ndani ya mishahara au vinginevyo kama itakavyoonekana inafaa,” alisema Pinda.

  Kauli ya Pinda aliyoitoa jana kuhusu posho, inatofautiana na ile aliyoitoa ndani ya Bunge wiki kadhaa zilizopita, wakati alipokuwa akijibu maswali ya wabunge kwenye kipindi maalum cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

  Katika kauli yake hiyo ya awali, Pinda alikaririwa akisema posho wanazolipwa watumishi wa umma wakiwamo wabunge zipo kisheria na hivyo taratibu zozote za kuziondoa zinapaswa kuzingatia taratibu zilizowekwa.

  Mbali ya hilo, Pinda alitetea posho hizo akisema kwa kiwango kikubwa zilikuwa zikiwasaidia wabunge kuwakirimu wageni wanaowatembelea bungeni.

  Katika hotuba yake ya jana, kabla ya kuhitimisha kwa kauli hiyo ya kutafakari na kuziangalia upya posho, Pinda alichambua aina mbalimbali ya posho wanazolipwa watumishi wa umma kisheria.

  Akizungumzia kuhusu hoja ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye aliwashutumu viongozi kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu wakati akichangia mjadala wa hotuba yake, Pinda aliitetea serikali ya awamu ya nne akisema ndiyo iliyofanya mambo mengi kuliko zote zilizotangulia.

  Akifafanua, Pinda alitoa mifano ya maamuzi magumu yaliyopata kuchukuliwa na serikali ya awamu ya nne kuwa ni kama yale ya ujenzi wa shule za kata na uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Mbali ya hayo Pinda alisema pia kwamba serikali katika kipindi hicho imejenga barabara nyingi, ikaanzisha mchakato wa Katiba mpya na akatoa mfano wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kama moja ya maamuzi magumu yaliyopata kufanywa.

  Hakuishia hapo, alikwenda mbele na kusema mfano mwingine wa maamuzi magumu ni ule wa kulivunja Baraza la Mawaziri ambao ulitokana na kujiuzulu kwa Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu.

  Hata hivyo Pinda hakueleza lolote kuhusu mapendekezo ya Lowassa ya aina ya maamuzi magumu aliyokuwa akitaka serikali iyafanye kama yale ya kujenga upya na kupanua bandari za Mtwara, Tanga na Dar es Salaam.

  Mbali ya hilo, Pinda hakueleza lolote kuhusu maoni mengine ya maamuzi magumu ya Lowassa ya kuitaka serikali ijenge upya Reli ya Kati na ile ya Tazara.

  Hotuba hiyo ya majumuisho ya Pinda ilitanguliwa na nyingine iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

  Katika mchango wake wa hotuba ya Waziri Mkuu, Lukuvi alikiri kwamba karatasi za kujumlishia kura zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, zilikuwa zinafutika kirahisi.

  Lukuvi ambaye katika mchango wake huo alikuwa akijibu hoja za wabunge kuhusu hotuba hiyo hiyo Waziri Mkuu, alidai karatasi hizo zilikuwa na ubora wa hali ya juu ambao ulipaswa kuziwezesha kudumu kwa muda mrefu bila kufutika.

  Alisema kwamba, kufutika kwa karatasi hizo kulitokana na waandishi kutogandamiza vizuri kalamu zao wakati wa kuandika idadi ya kura katika vituo vyao. Hata hivyo, hakusema kwanini, katika ubora huo aliosema, hali hiyo ya ‘kutogandamiza’ ilitokea nchi nzima.

  Alikuwa akijibu hoja ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, aliyehoji ubora wa karatasi hizo, ambazo zilifutika mara tu baada ya kupiga kura, hivyo kufanya kazi ya kuhakiki idadi ya kura kuwa ngumu.

  Hali hiyo ilimfanya Mbowe aitake serikali itangaze kuwa katika mazingira hayo, uchaguzi huo haukuwa huru na halali, kwani zoezi la kuhesabu lilikuwa na dosari ya msingi.

  Akitetea kufutika kwa karatasi hizo, Lukuvi alisema, “fomu hizo zilitengenezwa kwa namna ambayo ukijaza fomu ya mwanzo (original) nakala sita zinajitengeneza zenyewe (self copying forms). Ili fomu hizo zitoe nakala zinazosomeka mjazaji anatakiwa akandamize kalamu ipasavyo.

  “Kuna baadhi ya watendaji hawakukandamiza kalamu zao ipasavyo, na hivyo nakala zilizotengenezwa kutosomeka vizuri, ila original zilizotumika kujumlishia matokeo zilisomeka vizuri,” alisema Lukuvi.

  Alisema kampuni iliyotumika kuchapisha karatasi na fomu za matokeo ni Kalamazoo Secure Solution ya Uingereza, na kwamba ilipatikana baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa kwa kuzingatia sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004.

  Alieleza kuwa kampuni hiyo ina uwezo mkubwa wa uzoefu wa miaka 100 kuchapisha nyaraka nyeti na ilichapisha karatasi hizo za kura katika nchi mbalimbali ikiwemo Nigeria, Kenya, Malawi, Uganda na Uingereza.

  Pamoja na mambo mengine Lukuvi aliahidi kuwa serikali itato elimu ya kutosha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 ili wnaojaza fomu hizo wagandamize vizuri, wino usifutike.

  Walioshindwa CCM wachelewesha matokeo

  Akijibu hoja ya Mbowe kuhusu kuchelewa kutangaza matokeo katika maeneo mbalimbali nchini wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 hasa katika maeneo ambayo vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, walikuwa wameshinda, Lukuvi alitoa mfano wa majimbo ya Nyamagana, Ilemela, Ubungo, Moshi Mjini, Kawe, Hai na Arusha Mjini.

  Alisema hali hiyo ilitokana na ubishi wa wagombea walioshindwa au mawakala wao wakati wa kuhesabu kura, huku baadhi ya wagombea au mawakala wao wakitaka kura zihesabiwe upya, hata pale ilipokuwa dhahiri kwamba wameshindwa.

  Muundo wa serikali

  Kuhusu hoja ya Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (CCM), aliyetaka serikali kuangalia upya muundo huo wa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kupunguza urasimu na kupendekeza TAMISEMI kuwa Wizara inayojitegemea, Lukuvi alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 36 na 37, mamlaka ya kuunda wizara yamo mikononi mwa Rais.

  Pamoja na Lowassa, wengine waliokuwa wametoa hoja hiyo ni Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA, Regia Mtema na Susan Lyimo, na Mbunge wa Mbulu Mustafa Akonaay (CHADEMA).
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Walipane tuu posho wala wasishughulikie suala la umeme. Makusanyo ya kodi yatakaposhuka hadi sifuri kutokana na tatizo la umeme ndipo watakapoamka. Si unajua ukishiba kinachofuata ni kuzinzia?
   
 7. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hata bajeti ilichakachuliwa,
   
 8. M

  MdogoWenu Senior Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kama ni hivyo basi 2015 kila Chama kiwape wakala wake Carbon Papers. Wakala ataiweka juu ya karatasi ile atakayochukua kama kopi na chama kitakachokataa wazo hili basi wabaki hivyo hivyo.

  Vingineyo, basi kila karatasi iandikwe kwa kalamu. Kwa kituo kimoja kuandika hakuchukui zaidi ya nusu saa.

  Msipuu hili, ndiyo taratibu mbinu za kujiandaa na mwaka 2015.
   
 9. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  carbon paper ndio suhuhisho
  hiyo ya kila mtu kuandika kivyake ni rahisi kuyakana matokeo
  waweke carbone paper kwa kila kituo kulingana na idadi ya vyama wale wasiosimamisha mgombe
  sio tatizo zitaalibiwa lakini
  hizo paper ziwe standard kwa kila kituo
   
 10. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  wafikirie jambo la umeme jamani tumechoka na hii siasa ya mafisadi
   
 11. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Waziri mkuu apunguze ushabiki pale hoja zinapoletwa bungeni
  kwa mfano ili suhala la posho mpaka sasa ameshatoa kauli mbili tofauti katika kipindi cha mwezi mmoja
  hii ya mwisho inaonekana kuwa sahihi zaidi kuliko yale maneno CHADEMA WANAMEZEA POSHO MATE

  yeye kama waziri mkuu ni role model na kauli kama hizo za kubeza zinaleta ushabiki wa kisiasa na kuathiri utendaji wake kiserikali
  kwa mfano hakienda kwenye majimbo yenye wapenzi wa chadema wanamuona mamluki haka kama anaongea kama serikali.

  TAIFA KWANZA
   
 12. b

  bulunga JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haaingii akilini kuwa watengenezaji wa karatasi za kupigia kura(kalamazoo) hawakuweza kutoa tahadhari (remedies) jinsi ya kutumia karatsi za kupigia kura,eti wasimamizi walitakiwa kugandamiza kwa nguvu ilizisifutike, kama hawa watengenezaji wana sifa kuwa ni mahiri wa kutengeneza karatasi na wametengeneza sehemu mbalimbali dunia kwanini matatizo hayo yatokee tanzania tu, i smell fishy here. nafikiri itabidi credibility yao iwe questioned
   
 13. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mgao wa Umeme sasa Umeboreshwa zaidi, kuna wakati utakuwa 24hrs na hapo shirika litaitwa shirika la ugawaji wa giza. Bado natafuta maana ya neno NGELEJA
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Final wax coating bleed kwa wajuzi wa printing na publishing wanaijua sana. Hatua hiyo hufanyika kwenye document muhimu ambazo wax coat huhifadhi maandishi yaliyochapwa kwenye karatasi kwa miaka mingi bila kufifia kutokana na hali ya hewa, mwanga na hata mikwaruzo. Njia hii ni bora na gharama nafuu na hufanywa wakati huo huo karatasi zinapochapwa baada ya ink coat then final wax coat bleed. Document nyingi za serikali huchapwa kwa utaratibu huo, lakini si muhimu kwa karatasi za kura kwa kuwa si document za kutunza muda mrefu, ila hufanya ujanja huo kwa maslahi ya kufanikisha zoezi linalokusudiwa kisiasa.

  Kuna aina nyingi za wax, zipo kwa ajili ya kuhifadhi muda mrefu maandishi, zipo za kufanya unapoandika maandishi mengine juu yake huteleza na kutoshika wino na kuna wax ambayo maandishi huonekana muda tu unapoandika na hupauka muda mchache tu na hivyo kupotea kabisa taswira kwenye karatasi lakini maandishi ya awali yaliyochapwa kabla ya final wax coat bleed hayafutiki.

  Texture kwenye karatasi ni muhimu, fine or grossy texture ndio mbaya zaidi kwa vile pours kwenye karatasi ni ndogo sana kutoweza meza wino. Lakini texture kwenye karatasi ikiwa course ambayo si laini hushika wino na hivyo kutofutika haraka na kwa rahisi. Ukijua taaluma hii unaweza kuwa mwepesi wa kugundua kwa macho na kuigusa kwa mikono texture ya karasi na kujua kama inaweza kushika wino kirahisi unapoandika au la, vinginevyo wengine wanaona mradi ni karatasi unaweza andika juu kitu ambacho si kweli.

  Mfano ni karatasi maalum ya picha ambayo upande taswira ya picha paper texture ni very fine and grossy na ukijaribu kuandika kwa peni ya kawaida unaona inateleza, nadhani hapa unaweza pata picha vizuri. Imefanywa hivyo kwa ajili ya kuhifadhi taswira ya picha. Mtindo huo huo ndio unaotumika kutengeneza karatasi za kura kwa nia mbaya ya kufanya maandishi yapotee haraka ili kutotoa ushahidi wa ujanja uliofanyika. Mataifa yaliyoendelea mchezo huo uklikuwepo sana lakini kutokana na kukuka kwa teknolojia na njia za kupambana na ujanja huo mchezo huo haufui dafu tena.

  Njia ya kushinda mchezo huo mbaya ni wakati wa kupiga kura kutumia pen maalum ambazo hutoa wino wa majimaji badala ya wino mkavu kama tulivyozoea. Hii ni kwa sababu wino wa majimaji juu ya karatasi ni full coat kama ule unaotumika kuchapa karatasi mitamboni, na kamwe haufutiki kama ule wino mkavu toka kwenye pen za kawaida. Peni ya wino maji unaweza kufutika tu kwa kusugua iwepo ni karatasi yenye grossy texture, hilo haliwezi kutokea kwa karatasi cha kupigia kura kwa vile karatasi zake zimeandaliwa za texture ya kawaida ili kushika wino.

  Mataifa yaliyoendelea katika upigaji kura lazima kutumia peni maalumu zinazotoa wino maji badala ya peni za kawaida. Hata wakati wa kutia sahihi document zo zote za kiserikali au kisheria hutumika penni za aina hiyo ili kuondoa dhana ya taswira kupotea.

  Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wasitegemee tu njia ya waangalizi wao kwa macho tu, wanatakiwa kujua mbinu kama hizi zinazotumiwa na serikali ili kuiba kura kwa malengo ya kuendelea kushika dolla. Kwani karatasi zikishapoteza taswira ya kura si rahisi uhakiki kufanyika na pengine kuonekana kura nyingi zimeharibika.

  Karatasi za kupiga kura zinapochapwa kwenye mitambo inayoendeshwa kwa robot kama Roscam Robotical Interface System ni bora kwa vile wax coat huwa vigumu kwa vile wino na wax coat bleed zipo kwenye mfumo mkubwa kama matanki ya mafuta kwenye vituo vya gas station na wino au waxi hufanya kazi kwa mfumo wa circle kuingia mitamboni na kurudi kwenye reserve, njia hii ni kwa mitambo mikubwa ambapo hutumia mfumo wa Engrave Printing. Lakini utumiaji wa mitambo ya kawaida ambayo wino ni toka kwenye makopo au ndoo au mapipa ujanja huu wa wax coat ni rahisi kucheza kamali.

  Nimejaribu kutumia lugha ya kawaida sana ili ujumbe huu ueleweke kwa wengi, maana nikitumia zaidi lugha ya kitaaluma inaweza isieleweke vema kwa baadhi ya watu wasio na taaluma katika ulimwengu wa publishing industries. Na tujitahidi kuelimishana ili kujenga demokrasi ya kweli ndani ya taifa letu.
   
 15. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mkuu ulikuwa wapi siku zote hizi? Du nimekulewa sana
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Natazamia wengine wenye dondoo zaidi kuendeleza mjadala huu, kwani ulimwengu wa leo watanzania wamepanuka kwa kiwango kikubwa kimawazo, kiitikadi na kitaaluma, na hivyo tuungane kujenga nchi yetu kwa moyo mmoja bila ubinafsi.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nilikuwepo ila tu hatukujua jeuri waliyokusudia uchaguzi uliopita, sasa tunakuwa na tahadhari kubwa sana tu mchezo huo usiendelee kubaka demokrasi yetu.
   
 18. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mkuu big up, 2015 hakuna kulala karatasi za kura lazima tuzithibitishe kwanza na ikiwezekana hayo makampuni ya kuzichapa.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kabla ya karatasi za kura kutumiwa lazima zihakikiwe na wajumbe maalum kutoka kila chama shirika katika uchaguzi na kufanya majaribio kuona kama zinashika wino muda mrefu au la. Pia kuhakikisha wapiga kura wanatumia peni zinazotoa wino maji badala ya wino mkavu.
   
 20. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Bonge la Point mkuu
   
Loading...