Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Salaam,
Karne ya 21, ni karne ya kugeuza changamoto kuwa fursa katika kila sekta.
Vyama vya siasa ni miongoni mwa taasisi ambazo zinatakiwa ziwe zinageuza changamoto kuwa fursa.
CHADEMA NA MIPANGO MIKAKATI.
Ili chama chochochote cha siasa kiweze kufanya mambo makubwa ni lazima kiwe ni mipango mikakati madhubuti na inayosimamiwa kikamilifu.Na ili kuwa na mipango hiyo, ni lazma kuwepo na rasilimali watu inayojiweza kweli kweli katika eneo hilo.
Ni wazi kwamba ndani ya CHADEMA mpaka sasa kuna watu wachache sana wenye uwezo mkubwa katika eneo hili la mipango mikakati na pengine waliopo wangetumika vizuri na wakapatikana na wengine, CHADEMA ingefanya vizuri zaidi.
DR.KITILA MKUMBO NA MIPANGO MIKAKATI.
Ni wazi kwamba Dr Kitila Mkumbo ni miongoni mwa wanachama wachache ndani ya CHADEMA wenye uwezo mkubwa sana katika eneo la kupanga mipango mikakati.Waraka wa mabadiliko unaonesha uwezo wake wazi kabisa (japo waraka huo haukuandaliwa katika wakati sahihi na wakati fulani ulitumia lugha kali mno).Waraka ule unadhihirisha kwamba ni kwa jinsi gani chama kina vipaji lakini haki vitumii hadi vipaji hivyo vinaishia kutumika vibya.
Wakati fulani ikitokea wananchi wanatengeneza silaha za moto na wanawinda wanyama mbugani, wakikamatwa badala ya kufungwa , wanaweza kuingizwa kwenye majeshi na kutumia vipaji vyao kuunda zana za kivita.(changomoto kugeuzwa kuwa fursa)
Ni bora atakayechangia aweke emotion pembeni na awe "opportunist" Tehe! tehe!
Asubuhi njema.
Karne ya 21, ni karne ya kugeuza changamoto kuwa fursa katika kila sekta.
Vyama vya siasa ni miongoni mwa taasisi ambazo zinatakiwa ziwe zinageuza changamoto kuwa fursa.
CHADEMA NA MIPANGO MIKAKATI.
Ni wazi kwamba ndani ya CHADEMA mpaka sasa kuna watu wachache sana wenye uwezo mkubwa katika eneo hili la mipango mikakati na pengine waliopo wangetumika vizuri na wakapatikana na wengine, CHADEMA ingefanya vizuri zaidi.
DR.KITILA MKUMBO NA MIPANGO MIKAKATI.
Ni wazi kwamba Dr Kitila Mkumbo ni miongoni mwa wanachama wachache ndani ya CHADEMA wenye uwezo mkubwa sana katika eneo la kupanga mipango mikakati.Waraka wa mabadiliko unaonesha uwezo wake wazi kabisa (japo waraka huo haukuandaliwa katika wakati sahihi na wakati fulani ulitumia lugha kali mno).Waraka ule unadhihirisha kwamba ni kwa jinsi gani chama kina vipaji lakini haki vitumii hadi vipaji hivyo vinaishia kutumika vibya.
Wakati fulani ikitokea wananchi wanatengeneza silaha za moto na wanawinda wanyama mbugani, wakikamatwa badala ya kufungwa , wanaweza kuingizwa kwenye majeshi na kutumia vipaji vyao kuunda zana za kivita.(changomoto kugeuzwa kuwa fursa)
DR.KITILA AONGEZEWE ADHABU.
Ningependa kupendekeza kwamba Dr.Kitila aongezewe adhabu. Badala tu ya kufukukuzwa ujumbe wa kamati kuu, pia apewe adhabu ya kuandaa mipango mikakati mikubwa miwili yenye maslahi kwa chama na Taifa kwa muda atakaopewa (kwa kuwa imeonekana wazi kwamba ana kipaji na uwezo mkubwa wakufanya hivyo).Hapo tutakuwa tumegeuza changamoto kuwa fursa kwa kumpa adhabu yenye manufaa kwa CHAMA na Taifa.Baada ya hapo Dr.Kitila atumike kusanifu "Strategic plan" nyengine za chama kwa kushirikiana na wenzake kwa maslahi ya chama na taifa.Tukichezea raslimali watu tutakuwa tunachezea mali na mtaji.