CHADEMA kugeuza Changamoto kuwa Fursa: Dr. Kitila aongezewe adhabu!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Salaam,

Karne ya 21, ni karne ya kugeuza changamoto kuwa fursa katika kila sekta.
Vyama vya siasa ni miongoni mwa taasisi ambazo zinatakiwa ziwe zinageuza changamoto kuwa fursa.

CHADEMA NA MIPANGO MIKAKATI.

Ili chama chochochote cha siasa kiweze kufanya mambo makubwa ni lazima kiwe ni mipango mikakati madhubuti na inayosimamiwa kikamilifu.Na ili kuwa na mipango hiyo, ni lazma kuwepo na rasilimali watu inayojiweza kweli kweli katika eneo hilo.

Ni wazi kwamba ndani ya CHADEMA mpaka sasa kuna watu wachache sana wenye uwezo mkubwa katika eneo hili la mipango mikakati na pengine waliopo wangetumika vizuri na wakapatikana na wengine, CHADEMA ingefanya vizuri zaidi.

DR.KITILA MKUMBO NA MIPANGO MIKAKATI.

Ni wazi kwamba Dr Kitila Mkumbo ni miongoni mwa wanachama wachache ndani ya CHADEMA wenye uwezo mkubwa sana katika eneo la kupanga mipango mikakati.Waraka wa mabadiliko unaonesha uwezo wake wazi kabisa (japo waraka huo haukuandaliwa katika wakati sahihi na wakati fulani ulitumia lugha kali mno).Waraka ule unadhihirisha kwamba ni kwa jinsi gani chama kina vipaji lakini haki vitumii hadi vipaji hivyo vinaishia kutumika vibya.

Wakati fulani ikitokea wananchi wanatengeneza silaha za moto na wanawinda wanyama mbugani, wakikamatwa badala ya kufungwa , wanaweza kuingizwa kwenye majeshi na kutumia vipaji vyao kuunda zana za kivita.(changomoto kugeuzwa kuwa fursa)

DR.KITILA AONGEZEWE ADHABU.

Ningependa kupendekeza kwamba Dr.Kitila aongezewe adhabu. Badala tu ya kufukukuzwa ujumbe wa kamati kuu, pia apewe adhabu ya kuandaa mipango mikakati mikubwa miwili yenye maslahi kwa chama na Taifa kwa muda atakaopewa (kwa kuwa imeonekana wazi kwamba ana kipaji na uwezo mkubwa wakufanya hivyo).Hapo tutakuwa tumegeuza changamoto kuwa fursa kwa kumpa adhabu yenye manufaa kwa CHAMA na Taifa.Baada ya hapo Dr.Kitila atumike kusanifu "Strategic plan" nyengine za chama kwa kushirikiana na wenzake kwa maslahi ya chama na taifa.Tukichezea raslimali watu tutakuwa tunachezea mali na mtaji.

Ni bora atakayechangia aweke emotion pembeni na awe "opportunist" Tehe! tehe!

Asubuhi njema.
 
Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,180
2,000
Umanikumbusha muvi moja ya vita ambapo askari walikamata adui yao akiwa na silaha ambayo hawakujua kuitumia. Basi wakamwambia awaonyeshe jinsi ya kutumia ile silaha ili waifaidi wao akakubali... Akaikoki silaha akawaambia hivi ndivyo inavyotumika, huku akiwa amewageuzia.... Nadhani unajua nini kilitokea.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Betlehem umeandika vizuri sana. Tatizo lipo kwa hawa wahafidhina ambao wanadhani kuwa wasomi hawana mchango katika mafanikio ya CHADEMA. Ni hasara kubwa kwa chama kuwafukuza watu wenye upeo mkubwa kama Dr Kitila Mkumbo eti kwa vile tu Mwenyekiti hawapendi
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,548
2,000
Kitendo tuu cha kuzibaini fursa tayari hiyo ni fursa. Kujua namna ya kuitumia hiyo fursa nayo pia ni fursa na kisha kuichangamkia kuitumia nayo pia ni fursa!. Very unfortunately Chadema hawana watu wenye uwezo huo!.
Pasco
 
AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Hiyo mipango mikakati kwann isiwe kwa CCM au CUF lakin nyie ni CHADEMA tu? Jaman hamna vyama vingine kama CHAUMA TLP DP vya kuvishauri hiyo mipango mikakati yenu?
 
utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,000
Hiyo mipango mikakati kwann isiwe kwa CCM au CUF lakin nyie ni CHADEMA tu? Jaman hamna vyama vingine kama CHAUMA TLP DP vya kuvishauri hiyo mipango mikakati yenu?
kwa sababu ina ubaguzi ndio mana hatuachi kuisema mpaka iache hiyo tabia mbaya ya kunuka
 
kisiringyo

Member
Feb 9, 2012
89
70
We ni genius mkuu, kwa mwenye akili atafaham point ulizo zungumza, ila kwa mtu anaeongozwa na hisia atakurupuka na matusi hapa.
 
Bujigile

JF-Expert Member
May 18, 2011
251
225
Kitila!! Hongera umepata watetezi....... betlehem maoni yako ni mazuri sana lakini CDM hawayahitaji kwa sasa labda wapelekee CCM ili wawape adhabu MIZIGO iweze kurekebisha kwenye Wizara zao.
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,178
2,000
Mkuu unajua kujenga hoja vizuri,

Hiyo mipango mikakati hata chauma wanaihitaji kwa hiyo anaweza kuipeleka huko pia!
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Umanikumbusha muvi moja ya vita ambapo askari walikamata adui yao akiwa na silaha ambayo hawakujua kuitumia. Basi wakamwambia awaonyeshe jinsi ya kutumia ile silaha ili waifaidi wao akakubali... Akaikoki silaha akawaambia hivi ndivyo inavyotumika, huku akiwa amewageuzia.... Nadhani unajua nini kilitokea.
mkuu Tuko , movie hasa za kuuana si za ukweli.Kwa mfano kuna movie moja Ray alimuua mzee Magari.Tehe! sasa tukisema tuwe tunatumia movie kutafakari hoja za msingi, itakuwa kazi kweli kweli.
 
Last edited by a moderator:

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Hiyo mipango mikakati hata chauma wanaihitaji kwa hiyo anaweza kuipeleka huko pia!
Hallow Sir! you are in the world of emotion instead of been in the world of reasoning. "The world of emotion is in the realm of change while the world of reasoning is the word of permanence" Haya ni maneno ya mwanafalsafa ambaye nimemsahau jina.Sijui kama wewe unaweza kumkumbuka?

FTP

JF-Expert Member
Jun 6, 2013
515
195
Salaam,

Karne ya 21, ni karne ya kugeuza changamoto kuwa fursa katika kila sekta.
Vyama vya siasa ni miongoni mwa taasisi ambazo zinatakiwa ziwe zinageuza changamoto kuwa fursa.

CHADEMA NA MIPANGO MIKAKATI.

Ili chama chochochote cha siasa kiweze kufanya mambo makubwa ni lazima kiwe ni mipango mikakati madhubuti na inayosimamiwa kikamilifu.Na ili kuwa na mipango hiyo, ni lazma kuwepo na rasilimali watu inayojiweza kweli kweli katika eneo hilo.

Ni wazi kwamba ndani ya CHADEMA mpaka sasa kuna watu wachache sana wenye uwezo mkubwa katika eneo hili la mipango mikakati na pengine waliopo wangetumika vizuri na wakapatikana na wengine, CHADEMA ingefanya vizuri zaidi.

DR.KITILA MKUMBO NA MIPANGO MIKAKATI.

Ni wazi kwamba Dr Kitila Mkumbo ni miongoni mwa wanachama wachache ndani ya CHADEMA wenye uwezo mkubwa sana katika eneo la kupanga mipango mikakati.Waraka wa mabadiliko unaonesha uwezo wake wazi kabisa (japo waraka huo haukuandaliwa katika wakati sahihi na wakati fulani ulitumia lugha kali mno).Waraka ule unadhihirisha kwamba ni kwa jinsi gani chama kina vipaji lakini haki vitumii hadi vipaji hivyo vinaishia kutumika vibya.

Wakati fulani ikitokea wananchi wanatengeneza silaha za moto na wanawinda wanyama mbugani, wakikamatwa badala ya kufungwa , wanaweza kuingizwa kwenye majeshi na kutumia vipaji vyao kuunda zana za kivita.(changomoto kugeuzwa kuwa fursa)

DR.KITILA AONGEZEWE ADHABU.

Ningependa kupendekeza kwamba Dr.Kitila aongezewe adhabu. Badala tu ya kufukukuzwa ujumbe wa kamati kuu, pia apewe adhabu ya kuandaa mipango mikakati mikubwa miwili yenye maslahi kwa chama na Taifa kwa muda atakaopewa (kwa kuwa imeonekana wazi kwamba ana kipaji na uwezo mkubwa wakufanya hivyo).Hapo tutakuwa tumegeuza changamoto kuwa fursa kwa kumpa adhabu yenye manufaa kwa CHAMA na Taifa.Baada ya hapo Dr.Kitila atumike kusanifu "Strategic plan" nyengine za chama kwa kushirikiana na wenzake kwa maslahi ya chama na taifa.Tukichezea raslimali watu tutakuwa tunachezea mali na mtaji.

Ni bora atakayechangia aweke emotion pembeni na awe "opportunist" Tehe! tehe!

Asubuhi njema.

mpango mkakakati kama huu au ?
attachment.php
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
Kitila!! Hongera umepata watetezi......
Hivi kwa mfano kama wewe na wenzako mna hisa kwenye kampuni fulani, mtu mmoja akaibuka kushauri jinsi ambavyo kampuni inaweza kumtumia mtu fulani ili kunufaisha kampuni, je! huyo mtu anamtetea yule mtu aliependekeza kwamba kampuni imtumie, au anatetea kampuni au vyote?
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,815
2,000
betlehem unachekesha sana.. Ndio maana akina Lizabon wanakuunga mkono.
Kuhusu kuchekesha;nadhani ni jambo zuri tu maana watu kununiana siku zote nayo haina maana. Kuhusu kuungwa mkono na Lizaboni , narudia tena;

Si sahihi kuunga mkono hoja kwa kuwa tu imeungwa mkono na fulani, si sahihi kupinga hoja kwa kuwa tu imepingwa na fulani, wala si sahihi kutoa hoja ili kumfurahisha fulani na wala si sahihi kutoa hoja ili tu kumuudhi mtu fulani. Kufanya kinyume na hivyo ni kuongozwa na hisia badala ya fikra.Ubaya wa kuruhusu hisia zikuongoze, ni kwamba hisia hupanda na kushuka na hivyo ni rahisi sana kukupoteza.Ni bora kuchagua kuongozwa na fikra kwa kujenga hoja, kwa kuwa tunaamini ni hoja sahihi na si vinginevyo. Au wewe unasemaje mkuu?

Last edited by a moderator:

Mathias Lyamunda

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,369
2,000
Betlehem umeandika vizuri sana. Tatizo lipo kwa hawa wahafidhina ambao wanadhani kuwa wasomi hawana mchango katika mafanikio ya CHADEMA. Ni hasara kubwa kwa chama kuwafukuza watu wenye upeo mkubwa kama Dr Kitila Mkumbo eti kwa vile tu Mwenyekiti hawapendi
betlehem ukiona Lizaboni anakusifia ujue umekosa goli..
 
Last edited by a moderator:

Mathias Lyamunda

JF-Expert Member
Apr 4, 2013
1,369
2,000
Kuhusu kuchekesha;nadhani ni jambo zuri tu maana watu kununiana siku zote nayo haina maana. Kuhusu kuungwa mkono na Lizaboni , narudia tena;

Si sahihi kuunga mkono hoja kwa kuwa tu imeungwa mkono na fulani, si sahihi kupinga hoja kwa kuwa tu imepingwa na fulani, wala si sahihi kutoa hoja ili kumfurahisha fulani na wala si sahihi kutoa hoja ili tu kumuudhi mtu fulani. Kufanya kinyume na hivyo ni kuongozwa na hisia badala ya fikra.Ubaya wa kuruhusu hisia zikuongoze, ni kwamba hisia hupanda na kushuka na hivyo ni rahisi sana kukupoteza.Ni bora kuchagua kuongozwa na fikra kwa kujenga hoja, kwa kuwa tunaamini ni hoja sahihi na si vinginevyo. Au wewe unasemaje mkuu?

CCM na Chadema ni Giza na Nuru havichangamani..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom