CHADEMA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI WA UMEYA ARUSHA. (Mbunge apingwa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KUPINGA UCHAGUZI WA UMEYA ARUSHA. (Mbunge apingwa)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 19, 2010.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  UCHAGUZI wa Meya na Naibu wa Manispaa ya Arusha umechukua sura mpya baada ya kuibuka vurugu zilizosababisha Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kukamatwa na Jeshi la Polisi na kupigwa hadi kupoteza fahamu na kulazwa katika Hospili ya mkoa huo Mount Meru.Vurugu hizo zilizodumu kwa takribani saa sita, zilisababisha askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha kuwatawanya maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chadema waliokuwa wamezingira ofisi za Manispaa hiyo na kufunga kwa muda Barabara ya Mkuu wa Mkoa na ya New Arusha Hotel.


  Vurugu hizo zilibuka baada Lema pamoja na madiwani wa Chadema kufika katika ofisi ya Manispaa hiyo, kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ambao uliitishwa na kinyemela bila kuwashirikisha madiwani wa chama hicho.

  Uchaguzi huo umedaiwa kufanyika kwa kuwashirikisha madiwani na wabunge wa CCM na wa TLP wawili ambao walimchagua Diwani wa Kata ya Olorien (CCM), Gaudence Lyimo, kuwa Meya na naibu Meya wake Michael Kivuyo ambaye ni Diwani wa Kata ya Sokoni kwa tiketi ya TLP.

  Kufuatia hali hiyo baadhi ya askari wa jeshi polisi waliokuwepo eneo hilo wakiwa wamevalia zana mbalimbali za kutuliza ghasia, walimzuia mbunge huyo kuingia ndani huku wakimwamuru atoke nje ya eneo hilo.

  Alipokataa askari hao walianza kumpa kipigo na kusababisha kupoteza fahamu kwa dakika saba kisha wakampakia katika gari lao hadi Kituo Kikuu cha Polisi mjini Arusha na kumweka rumande.

  Hali hiyo ilisababisha mamia ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kujikusanya na kukizingira kituo hicho, huku wakiwatuhumu polisi kujiingiza katika masuala ya siasa ya kuisaidia CCM.

  Majira ya saa 9 Alasiri, mbunge huyo aliachiwa kwa dhamana na kurejea katika ofisi za Manispaa akiwa na kundi kubwa la wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakirusha maneno makali huku wengine wakitishia kuchoma moto ofisi ya manispaa.

  Katika ofizi hizo, FFU waliibuka tena na kurusha mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha, hali iliyosabisha Lema ambaye alikuwa akizungumza na madiwani wa Chadema kukimbia kisha kuanguka na kupoteza fahamu kwa dakika kama tano na kukimbizwa katika Hopitali ya Mount Meru kwa matibabu zaidi.

  Mwananchi Jumapili ilishuhudia jana jioni Lema akiwa amelazwa katika moja ya wodi katika hospitali ya Mount Meru akiwa na mkewe.

  Wakati Lema akiwa amelazwa katika wodi hiyo umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema ulikuwa umetanda nje ya hospitali hiyo wakisubiri kujua hatima ya afya ya mbunge wao.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Tobias Adengenye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba kukamatwa kwake kunatokana na Lema kukaidi amri ya polisi.

  Awali Lema aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa kipigo alichopata, kilimsababisha matatizo ya mbavu pamoja na mkono wa kulia kuumia.

  “Pamoja na mambo mengine, nina maumivu makali sana katika sehemu za mbavu pamoja na mkono wa kulia,” alisema Lema.

  Kiongozi wa kambi ya upinzani Arusha ambaye ni Diwani wa Chadema, Kata ya Elerai, John Bayo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kwenda mahakamani kesho (Desemba 20) kufunuga kesi kupinga uchaguzi huo kutokana na baadhi ya kanuni kutofuatwa.

  Bayo alifafanua kwamba mojawapo ya kanuni iliyokiukwa ni kutozingatiwa kwa idadi ya theluthi mbili ambao ni madiwani 20 wenye mamlaka ya kumchagua meya na naibu wake.

  Katika Manispaa hiyo, CCM ina jumla ya madiwani 14 huku Chadema ikiwa na jumla ya madiwani 16 huku TLP ikiwa na wawili.

  “Jumatatu (kesho), tunaenda mahakamani kupinga uchaguzi huo, kwanza hatukupewa barua ya kuhudhuria uchaguzi leo baada ya jana kuhairishwa, lakini pili idadi yao haikutimia kumchagua meya na naibu wake kwani sheria inasema ni theluthi mbili itakamilisha uchaguzi, wao walikuwa 15,” alisema Bayo.


  Hata hivyo, uteuzi Diwani wa TLP wa Naibu Meya umezua utata kwa vile awali alikuwa akiwaunga mkono Chadema na kwamba hadi saa 5 asubuhi alikuwa katika mkutano wa madiwani wa upinzani.

  “Alituaga kuwa anakwenda ndani ya ofisi za Manispaa kujua nini hatma ya uchaguzi, lakini hakurudi hadi tulipopata taarifa kuwa amechaguliwa kuwa Naibu meya,’’ kilisema chanzo chetu.

  Alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, Katibu wa Itikani na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema: “Uchaguzi si wa kinyemela unajulikana nchi nzima, lakini siwezi kuzungumza lolote kwa sasa kwa kuwa bado sijapata taarifa rasmi kuhusu hali hiyo”.

  Uchaguzi huo ulikuwa ufanyike juzi, lakini uliahirishwa na Msimamizi wa Uchaguzi, Estomi Chang'a ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha kufuatia kutokea malumbano baada ya madiwani wa Chadema kupinga kitendo cha CCM kumteua, Mary Chatanda ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga na Katibu wa CCM mkoani Arusha kuwania nafasi hiyo ya umeya.

  Sababu nyingine ni kambi ya upinzani kupinga kitendo cha msimamizi wa uchaguzi kumzuia Diwani wa viti maalumu wa TLP, Mwamvua Wahanza kutopiga kura kwa madai ya kutothibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

  Katika hatua nyingine, askari waliokuwa wakilinda ofoso manispaa hiyo waliwazuia baadhi ya waandishi wa habari kuingia ndani kwa madai kuwa hawana mwaliko rasmi huku isipokuwa mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Leornad Manga.

  Pamoja na waandishi kuwasomea kanuni za kudumu za mikutano na shughuli za manispaa, walikataliwa kuingia.

  Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Chang'a kuzungumzia suala hilo zilishindikana kutokana na simu yake ya mkononi kushindwa kupokelewa hadi tunakwenda mtamboni.

  Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei aliiambi Mwananchi Jumapili jana kuwa analaani sana kitendo hicho cha kukamatwa mbunge wao na kwamba kinaonyesha wazi kuwa CCM bado imechaganyikiwa kutokana na kupoteza majimbo mengi katika uchaguzi mkuu.

  Jambo la kushangaza uchaguzi wa mameya umekuwa na matatizo makubwa katika maeneo yote ambayo upinzani una madiwani wengi huku wakurugenzi wa halmashauri hizo, ambao ndiyo wasimamizi kwaikidaiwa kuhusika kupanga njama za kukipendelea Chama Cha Mapinduzi kwa kukiuka taratibu.
   
 2. m

  mams JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tuachane na itikadi za kisiasa, kitendo kilichofanyka dhidi ya CDM si cha kiungwana katika Tanzania tuliyozaliwa tunaiona.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCM ni washenzi sana ...shae on you andengenye...sishangai maana umeanzia uhausi bi kwa kamishna shomvi miaka hiyo kakupeleka ccp leo umekuwa rpc kwa ajili ya kubebwa bebwa tu...You are not a RPC enough kwa kuwa huna akili bado unawaza kama hausiboi tu
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hali hii inasikitisha sana wandugu! Haya mambo ya Ivory Coast yameshaanza kufika huku kwetu Tanzania taratibu!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Walichokifanya polisi kimewaharibia sana na itashangaza sana kama wataendelea kukitetea kitendo chao
   
 6. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kilichofanyika ni uhuni na kina agenda ya kuibeba CCM! Kwa mtu yeyeto makini ambaye hana ukame wa fikra au udhaifu wa ubongo katika kufikiria uchaguzi huo ni batili na hofu ya CCM inaonekana wazi kuwa wanaogopa kuachia jiji hilo lishikwe na CDM kama ilivyotokea kwa upande wa mbunge. Chadema kama inamdiwani 16, CCM 14 na TLP 2 kwa nini usifikirie kuwa kufanya kwao mkutano wa kumchagua Mayor kinyemela bila ya kuwataarifu wenzao ni hujma na wasiwasi?!

  Tumeamka na tunajua mbinu zote chafu za CCm na hiyo ni mojawapo ya ishara kuwa hata ushindi wao kwenye baadhi ya majimbo ni wakutilia mashaka na hata ushindi wenyewe umefanye pia huenda umekuwa wa ujanja ujanja kama walivyofanya kwenye manispaa ya Arusha. Tuwakatae kwa uhuni wanao ufanya maana unatupeleka kwenye machafuko na kuvuruga amani aliyoiasihihi Mwl Nyerere.

  Naomba kuwasilisha.
   
 7. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote nasema Watanzania tuache upumbavu. Haya mambo yamefikia hapa kwa kuwa tumeyaacha yafikie hapa. CCM ni ngenge la mafisadi wasiojali wengine. Ni wakati sasa watanzania tuhamasishane kukataa na kupinga udhalimu huu wa CCM. Nina wasiwasi na huko mahakamani kwani kesi hii haita sikiliza kwa kipindi cha miaka 5
   
 8. cumshot

  cumshot Member

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani muda wa longolongo umeisha isha inatupasa watanzania tuamke kulipagania taifa letu dhidi ya serikali ya kidhalimu na kidikteta ya chama cha mafisadi(ccm)
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hilo jina lako tu daaah
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Huuyu Andengeye amefika hapo kwa kubebwa .....u RPC alipewa enzi za mahita ..kisa alikuwa msaidizi maalum wa mahita...mahita alipoona anakaribia kustaafu akampandisha vyeo haraka haraka kufikia hapo alipo......wenzake wenye elimu moja na uwezo sawa bado wanasota ..walioenda sana wamefikia u OCD.

  Kitendo kilichofanyika Arusha sio uungwana kabisa ....kwa namna yeyote ile kiongozi wa umma...kuna utaratibu wake wa kumkamata ndio maana yule OCD aliyepewaga amri amkamate mbunge wa simanjiro ...na mkuu wa mkoa hakuitekeleza kwa kuwa kuna utaratibu wa kumkamata kiongozi ,....sio kwa kumpiga.....hiii ilikuwa inahatarisha maisha ya wote waliokuwapo hapo kwa OCd kukosa busara...wewe fikiria wananchi wangeamua kuchoma moto jengo la manispaa ,nani angebakia????

  Yakitokea haya kikwete alikuwa umbali mfupi toka hapo city council kwenye ikulu ya Arusha..alienda arusha kufungua hoteli ya mount meru......kwanini watu wasiamini kuwa haya yoote yana baraka za rais........kwani kuna ubaya gani CHADEMA wakiongoza halmashauri arusha mbona wameshafanya hivyo maeneo mengine kwa amani...

  nadhani sasa mtagundua tishio la kuvunjika amani linaletwa na nani .....amani inatishiwa tu pale CCM inapoelekea kushindwa....sasa siku wakishindwa urais si watauwa watu hawa???
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Watendaji wote wa mkoa wa Arusha wapo kwenye hofu ndio maana wapinzani hawawezi kupata haki......

  kabla hata ya uchaguzi kufanyika walimfyeka mkurugenzi Raphaele Mbunda...baada ya uchaguzi wakamfyeka RPC basilio matei...ambaye alikuwa ameumudu mkoa....tangu enzi za mkutano wa sullivan...,kwa hiyo watendaji waliobakia wana hofu kubwa ya kupoteza kazi zao ....
  Lakini wanatakiwa wajuwe tabia za watu wa arusha wamasai ,wachagga ,warangi na makabila mengine yenye idadi kubwa pale .......hawakubali kuonewa na wanazijuwa vurugu kweli kweli...kwa kilichotokea tutapata aibu hasa kama mashirika ya kimataifa yenye makao makuu arusha yakipeleka taarifa kwao ....tutapeteza fursa nyingi muhimu kwa mkoa ule kwa kukosa demokrasia rahisi kama ya kuchagua meya[wapiga kura hawazidi 40 ..bado tunachakachua]......
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Tunayo safari ndefu ya kufikia kwenye malengo tunayotaka kuyatimiza kupitia mgongo wa siasa, lakini kama tutaungana pamoja ninaamini hata polisi wataona aibu. CCM bado wana fikra mgando za miaka ya 40. Watanzania wa leo sio wale wa nyakati zile, japo wapo baadhi walioaminishwa na ccm kwa faida ya mafisadi.
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Cha msingi ni kuendeleza mapambano mbaka mwisho ili kuondoa ubabaishaji wa CCM na serikali yake!!
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,870
  Trophy Points: 280
  Hawa ccm wanajiona wako juu ya sheria lakini wamesahau kuwa watu sasa wameamka na wanajua haki zao. Mungu akupe nafuu mbunge na swala hili lisiishie hapa hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya unyanyasaji wa polisi.
   
 15. K

  Kiwete JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  CHADEMA nchi nzima anzisheni civil disobedience.Naamin wengi tutaunga mkono kwa namna tunavyoweza kuanzia wafanyakazi wa umma,wakulima,makonda na madereva na hata mittani.
  Mahakama gani iko huru kuweza kutoia haki kwa upinzani?Hakimu huyo hataki ujaji,kama ni Jaji hataki ubalozi au uenyekiti wa tume akistaafu?anataka aishie kama Mwalusanya?
  Achenoi uoga?Tunatakiwa twende hatua nyingine sasa,tunakosa mwongozo tu.
   
 16. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2010
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Jamani Wamuogope hata Mungu,wakumbuke hakuna kidumucho chini ya jua,hata hayo madaraka wanayolazimisha yanamwisho,na yatakapo fika mwisho lazima watarudi kuishi nasi kwenye jamii,ndipo aibu na ukosefu wa amani mioyoni mwao vitakapotawala,.. Kwenye haya maisha ni bora kukosa yote na si kukosa amani..ni rahisi kufa kabla ya siku zako.. ukweli mipango ilianza kufanyika kitambo kubatilisha uchaguzi kwa haraka nafikiria sababu ya kuamishwa kwa Matei..
   
 17. D

  DENYO JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kitendo hiki cha kulaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani na waliohusika nguvu ya umma iwachukulie hatua. Bado tuna wakoloni hivi ccm wanadhani wataburuza watanzania mpaka lini???? Polisi wajinga imekuwa mtaji kwao kitendo cha kumkamata kwa nguvu mbunge aliyekuwa anasimamia haki ni ushetani na udikiteta wa halli ya juuuu. Kitendo kinathibitisha mwisho wa ccm pia kinaonesha kukosekana kwa amani kabisa -ni hatari na lazima tupambane na dhuluma hii -unyanyasaji wenye mibaraka ya serikali. Huku ni kuonewa sana ndani ya nchi yetu. Pole kaka lema lakini tunahitaji viongozi kama wewe endelea kusimamia umma na watanzania tupo na wewe
   
 18. P

  Patupetu Shekiu Member

  #18
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  well...tusubiri hiyo mahakama itasemaje. Kama sheria inasema idadi ni 2/3 na haikufika hiyo...jibu ni simple...huyo Meya hawezi kusimama.
  hii itakuwa ishu ikiwa mahakama itagoma kwenye hii ishu!
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Dec 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145


  Inaelekea hii tabia kaitoa kwa Rtr IGP Mahita.............unakumbuka ile tafrani ya Polisi Moshi under RPC Mahita Vs Mrema..........Pamoja na kubebwa.........kusema kweli huyu jamaa ni smart sana........nakuhakikishia angekuwa ni "selule".....Mwema asingemuamini na kumpa baadhi ya majukumu nyeti aliyompatia so far.........na hata akampandisha Cheo.........Tobias (PhD Candidate) ni future ndani ya Jeshi la Polisi.........WATCH his pace..............

  Pole sana Mbunge Lema............nakutakia afya njema upone haraka..............turudi kutafuta haki ya wengi..............
   
Loading...